Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan atakosa fainali ya ligi ya Europa dhidi ya Chelsea


Henrikh Mkhitaryan

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Henrikh Mkhitaryan ameichezea Arsenal mechi 11 katika Ligi ya Europa msimu huu

Kiungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan hatacheza mechi ya fainali ya Ligi ya Europa dhidi Chelsea Mei 29.

Inasemekana kuwa Muarmenia, huyo wa miaka 30, amehofia usalama wake uwanjani Baku, Azerbaijan.

“Baada ya kutathmini njia zote,ilibidi tufanye uamuzi huo mgumu wa mimi kutosafairi na kikosi kitakachoshiriki fainali ya Ligi ya Europa,” alisema Mkhitaryan.

“Ni aina ya mchezo ambao ni nadra sana, kwa kweli nasikitika sana kuwa sitacheza.”

Kutokana na mzozo wa kisiasa kati ya Azerbaijan na Armenia, Mkhitaryan amekosa mechi kadha za klabu zilizochezwa Azerbaijan aiku zilizopita.

“Tumeandikia Uefa kuelezea hofu yetu kuhusu hali hiyo,” alisema taarifa ya Arsenal.

“Tumejaribu mbinu zote ili Micki ajumuishwe kwenye kikosi hicho lakini baada ya kujadiliana na Micki na familia yake tulikubaliana kwa pomoja kuwa ajiondoe kwenye msafara huo.

Haki miliki ya picha
Getty Images

“Micki amekuwa kiungo muhimu kuelekea fainali hii kwa kweli ni pigo kubwa kwa timu nzima.

“Pia tunasikitika kuwa atakosa mechi kubwa kama hiyo barani Ulaya kutokana na hali kama hii, ikizingatiwa kuwa ni furasa adimu katika mchezo wa kandanda.”

Uefa iliijibu Arsenal kupitia taarifa ya maandishi iliyosema: “Tukishirikiana na Arsenal FC, Uefa imepata hakikisho kutoka kwa mamlaka ya juu ya nchi kuwa usalama wa mchezaji nchini Azerbaijan utaimarishwa.

“Kutokana na hakikisho hilo, mpango madhubuti wa usalama ulifanywa na kupewa klabu hiyo.

“Japo Klabu imeridhishwa na juhudi za Uefa na serikali ya Azerbaijan, tunaheshimu uamuzi wa kibinafsi wa mchezaji kutosafiri.”

Shirikisho la soka la Azerbaijan FA limeelezea “masikitiko” yake kuwa Mkhitaryan hatujiunga na klabu yake kishiriki mechi hiyo muhimu ya fainali.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Henrikh Mkhitaryan ni nahodha wa Armenia na ameifungia timu hiyo mabao 27 katika mechi 82

Katika taarifa yake shirikisho la AFFA lilisema: “Tunasikitika sana na uamuzi uliyochukuliwa. Japo tunaheshimu uamuzi wa kibinafasi kuhusu suala hili, tunasisitiza kuwa Azerbaijan kama mwenyeji wa fainali hizo imeweka mikakati yote ya kiusalama inayohitajika na Uefa kuhakikisha usalama wa kibinafsi wa Bw. Mkhitaryan unalindwa.

“Hakuna haja ya kutilia shaka hakikisho lililotolewa na Azerbaijan.”

Arsenal, amabo walimaliza ligi ya Primia katika nafasi ya tano, watafuzu kwa Champions League msimu ujao wakiishinda Chelsea.

Itakuwa kombe lao la kwanza la ulaya tangu mwaka 1994.

Meneja wa Arsenal Unai Emery amesema: “Alitaka kucheza, alakini alipozungumza na familia yake akaamua kubadili msimamo huo..

“Ni uamuzi wa kibinafsi sana na tunahitaji kuheshimu uamuzi wake. Sina ufahamu kuhusu tatizo la kisiasa lakini lazima niheshimu uamuzi wake.”

Siku ya Jumatatu Balozi wa Azerbaijan nchini Uingereza, Tahir Taghizadeh, alisema hakuna haja ya kuwa na hofu kuhusu usalama wa nyota huyo raia wa Armenia.Source link

Sudan waitisha maandamano makubwa zaidi


Viongozi wa maandamano ya Sudan walifanikiwa kufikia makubaliano na baraza la kijeshi la kuhusu masuala kadhaa ya kipindi hicho cha mpito. Lakini mapema Jumanne, majenerali waliomuondoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir mwezi uliopita wamepinga madai ya waandamanaji, ya kutaka kiongozi wa nchi awe wa kiraia na idadi kubwa ya raia wa kawaida kuwamo katika baraza jipya lililokubaliwa kuongoza kipindi hicho cha mpito cha miaka mitatu hadi itakapopatikana demokrasia kamili wakati utakapoitishwa uchaguzi.

Chama cha Wanataaluma wa Sudan kinachoongoza maandamano hayo ya miezi minnne ya nchini kote, yaliyopelekea al-Bashir kuondoka madarakani, kimesema ili kupata ushindi kamili wanawataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maandamano makubwa zaidi. Mmoja wa waandamanaji kwa jina la Moujahed Mohamed amesema hawatokubali abadan kuachana na madai yao ya kutaka serikali ya kiraia.

“Baraza la kijeshi limekuwa likikawia sana, hatutoachana na madai yetu ya kutaka serikali ya kiraia. Nahisi nimebanwa sana kwavile majadiliano yamesimamishwa na sijizungumzii mimi mwenyewe tu, lakini wengi hapa wanakasirishwa na huku kuchelewa kwa baraza la kijeshi bila ya sababu za msingi,” amesema Mohamed.

Sudan Militärrat Abdel Fattah al Burhan (picture-alliance/AA)

Mwenyekiti wa Baraza la Kijeshi la Mpito, Jenerali Abdel Fattah al Burhan

Baraza la kijeshi chini ya shinikizo

Pande hizo mbili zilifanya kile kilichoelezwa kuwa ni duru ya mwisho ya mazungumzo Jumapili jioni. Baraza la kijeshi la mpito limekuwa chini ya shinikizo kutoka nchi za magharibi na Umoja wa Afrika, kukubali madai ya waaandamanaji ya kutaka serikali ya kiraia katika kipindi cha mpito cha miaka mitatu. Na kwa hakika hilo ndiyo dai kubwa kutoka kwa maelfu ya waandamanaji, wanaokita kambi kwa wiki kadhaa sasa nje ya makao makuu ya kijeshi mji mkuu wa Sudan wa Khartoum.

Baada ya mazungumzo kuvunjika mapema Jumanne, hamna upande uliosema watarudi lini tena katika meza ya mazungumzo.

Kiongozi wa maandamano hayo Siddiq Yousef amewaambia waandishi habari kwamba mazungumzo yamesitishwa na kipengele kikuu cha mzozo ni kuhusu idadi ya wawakilishi kutoka upande wa kiraia na wa kijeshi itakayounda baraza jipya la mpito, na nani atakuwa kiongozi wa baraza hilo litakaloiongoza Sudan.

Baraza la kijeshi linataka mwenyekiti wake Jenerali Abdel Fattah al-Burhan awe kiongozi wa baraza hilo jipya la mpito, lakini waandamanaji wanataka kiongozi mpya awe ni wa kiraia.

Mwandishi: Yusra Buwayhid (rtre,afp)

Mhariri: Sekione KitojoSource link

Wanawake wa Korea Kaskazini wageuzwa watumwa wa ngono China


Wataalamu wamesema kuwa maelfu ya wanawake na wasichana kutoka Korea Kaskazini, wanapojaribu kukimbia umaskini na ukandamizaji nchini mwao, wanasafirishwa kimagendo kuelekea China ambapo wanageuzwa kuwa watumwa wa kingono.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali kwa jina Korea Future Initiative lenye makao yake mjini London, ukandamizaji wa kingono unaofanywa dhidi ya Wakorea wa Kaskazini huyapa magenge ya China faida ya dola milioni 105 kila mwaka. Hiyo ikiwa ni kando na mateso wanayoyapitia wanawake wanaosafirishwa kimagendo.

Waathirika ambao ni wanawake na wasichana, wengine wakiwa na umri mdogo wa miaka 9, hushirikishwa kwenye ukahaba na kulipwa pesa kidogo dola 4.30.  Wengine huuzwa kuolewa kwa yuan 1000. Wanatumikishwa kingono na video zao za ngono husambazwa kwenye mitandao. Amesema Yoon Hee-soon aliyeiandika ripoti hiyo.

Ameongeza kuwa wengine huuzwa zaidi ya mara moja na hulazimishwa katika utumwa wa kingono angalau kwa mwaka mmoja wakiwa nje ya nchi yao.

Wengi wa waathiriwa husafirishwa China Kimagendo

Ripoti yasema baadhi ya wanawake wamekufa kutokana na magonjwa ya zinaa au mateso.

Ripoti yasema baadhi ya wanawake wamekufa kutokana na magonjwa ya zinaa au mateso.

Kulingana na ripoti ambayo inapaswa kuzinduliwa Jumatatu katika bunge la Uingereza, inakadiriwa kuwa asilimia 60 ya wasichana na wanawake wa Korea Kaskazini walioko China husafirishwa kimagendo kutumikishwa kwenye biashara ya ngono.

Watafiti wameeleza kuwa nusu ya wanawake na wasichana hao hulazimishwa kwenye ukahaba. Theluthi moja huuzwa ili kuolewa na wengne wengi hushirikishwa kwenye ngono kupitia intaneti.

Shirika la habari la Reuters limesema hakukuwa na afisa yeyote wa China katika ubalozi wao mjini London kuzungumzia suala hilo.

Ripoti hiyo imeeleza kuwa Wakorea wengi wa Kaskazini ni watumwa katika madanguro katika wilaya za kaskazini mashariki mwa China iliyo na wahamiaji wengi.

Waathiriwa wafariki kutokana na magonjwa ya zinaa

Waathiriwa wa biashara hiyo haramu wanasema makahaba mjini Shangai waliwekewa tattoos za michoro kama ya simba na vipepeo kuonyesha nani anawamiliki na pia kuwaepusha dhidi ya kutekwa na magenge pinzani.

Waliohojiwa walieleza visa vya baadhi ya wanawake kufariki kutokana na magonjwa ya zinaa na mateso.

Wasichana wanaoshirikishwa kwenye ngono mitandaoni aghalabu huwa na umri wa kati ya miaka 12 na 29, lakini wakati mwingine hata walio na umri wa miaka ya chini zaidi. Ripoti hiyo imeeleza.

Wanalazimishwa kufanya vitendo vya ngono au wanadhulumiwa kingono huku video zao zikichukuliwa. Wakati mwingine visa hivyo hupeperushwa moja kwa moja katika tovuti za ngono.

Vyanzo: Reuters

 Source link

Je, tunajifunza chochote kutokana na majanga ya majini


ajali hiyo ya kivuko cha MV Nyerere.

Image caption

Ajali ya kivuko cha MV Nyerere ambayo iliua zaidi ya watu 200

Ni miaka 23 tangu kisa cha ajali ambayo inatajwa kuwa mbaya zaidi katika karne kutokea barani Afrika katika ziwa victoria nchini Tanzania.

Ni janga ambalo lilisababisha idadi kubwa ya watu wapatao 1000 kupoteza maisha baada ya meli ya Mv Bukoba kuzama.

Sababu ambayo ilitajwa kusababisha ajali hiyo ilikuwa idadi ya abiria kuzidi, chombo kuwa na itilafu, pamoja na vifaa vya ukozi kuwa vichache.

Pamoja na ajali hiyo kubwa kuacha simanzi kwa baadhi ya familia hadi sasa, na fundisho kwa kisa cha namna hiyo kutotokea tena.

Lakini bado Tanzania na Afrika mashariki na kati wanaendelea kushuhudia ajali ambazo sababu ya kutokea au watu kupoteza maisha zikiwa zinafanana.

Mwaka jana , septemba 2018 jumla ya watu 224 walifariki na watu wengine 41 wakiokolewa wakiwa hai katika ajali hiyo ya kivuko cha MV Nyerere.

Tanzania iliweza kushuhudia pia ajali za maji ikiwemo za habari ya hindi Mv Skagit na Mv Spice Islander na kupoteza idadi kubwa ya watu

Ni wiki moja tu imepita ambapo ajali nyingine ya maji imetokea na kuua watu tisa huku wengine wakiwa hawajulikani walipo huko nchini Uganda.

Boti iliyokuwa imebeba wacheza mpira 50 wakiwa na mashabiki wao huko Magharibi mwa Uganda.

Huku ikikumbukwa kuwa mwaka 2016 , wachezaji 30 wakiwa na mashabiki wao walizama na maji katika ziwa Albert na watu 20 walifariki.

Mwaka 2018 nchini Uganda, watu 29 walifariki kufuatia ajali ya mashua iliyotokea ziwa Victoria.

Mashua hiyo iliyokuwa na watu zaidi ya 90 waliokuwa wanaelekea sherehe, ilipata ajali katika kaunti ndogo ya Mpatta wilaya ya Mukono.

Wasanii kadhaa na watu wengine mashuhuri waliaminika kuwa kwenye mashua hiyo..

Maafisa walisema kwa mashua mbili za uvuvi ambazo ziliwasili kuokoa nazo zilifurika watu na kuzama.

Mwaka 2014, Umoja wa Mataifa umesema kuwa takriban watu 98, wamekufa maji baada ya boti walimokuwa wanasafiria kuzama katika Ziwa Albert Magharibi mwa Uganda.

Boti iliyozama ilikua imebeba zaidi ya wakimbizi 100.

Aliyekuwa anaendesha boti hiyo amekamatwa na jeshi la polisi na inadaiwa kuwa alikua mlevi.

Hii sio mara ya kwanza ajali ya boti kuua watu katika Ziwa Albert kutokana na kujaza abiria na mizogo kupita kiasi.

Watu 50 wamefariki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya boti kuzama kwenye mto kaskazini mwa nchi hiyo.

Mwaka 2010, ajali ya boti nchini Uganda iliuwa watu zaidi ya 70 baada ya mashua waliokuwa wakisafiria kuzama katika ziwa Albert nchini Uganda.

Ajali hii ilitokea eneo lijulikanalo kama Kakoma katika kijiji cha Runga, Wilaya ya Hoima.

Mwaka huu, Aprili 2019, takriban watu 150 wametoweka baada ya boti kuzama katika ziwa moja mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na watu 33 wakaokolewa katika ajali hiyo.

Kulingana na Reuters mwaka uliopita , boti moja lilipinduka katika mto kaskazini mwa DR Congo , na kusababisha watu 49 kufa maji huku idadi kama hiyo ya watu wakiokolewa.

Mwaka wa 2015, zaidi ya watu 100 walitoweka baada ya maboti mawili kugongana katika mto Congo nchini DR Congo kulingana na shirika la afya duniani WHO.

Mnamo mwezi Julai 2011, zaidi ya watu 100 walifariki baada ya boti mbili kugongana katika mto katika eneo la mkoa wa Equateur la DR Congo.Source link

Uchaguzi wa rais waendelea Malawi


Malawi inafanya uchaguzi wake mkuu leo kumchagua rais mpya pamoja na wabunge. Shughuli za upigaji kura zilianza mapema leo katika vituo vya upigaji kura. Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika aliye na umri wa miaka 78 anawania muhula wa pili huku akikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa makamu wake na mgombea wa chama kikuu cha upinzani.

Vituo vya upigaji kura vilifunguliwa mwendo wa saa kumi alfajiri majira ya nchi hiyo, na inatarajiwa kuwa wapiga kura milioni 6.8 waliosajiliwa watashiriki kwenye uchaguzi huo wa rais, wabunge na madiwani.

Wapiga kura wameelezea matumaini ya kuwachagua viongozi wanaowapenda kuleta maendeleo.

Wachambuzi wanatarajia ushindani kuwa mkali kati ya rais Peter Mutharika, makamu wake Saulos Chilima na kutoka kwa Lazarus Chakwera ambaye anaongoza kundi la vyama vya upinzani Malawi Congres Party.

Wapiga kura kwenye foleni katika kituo cha kupiga kura karibu na mji mkuu Blantyre.

Wapiga kura kwenye foleni katika kituo cha kupiga kura karibu na mji mkuu Blantyre.

Rais Mutharika mwenye umri wa miaka 78 alitekeleza maendeleo ya miundombinu na alipunguza viwango vya mfumuko wa bei ya bidhaa nchini humo katika muhula wake wa kwanza madarakani. Lakini wakosoaji wanamshutumu kwa kuendeleza ufisadi na upendeleo, madai ambayo Mutharika hukanusha.

Chilima mwenye umri wa miaka 46 na ambaye ni mkuu wa zamani wa kampuni ya mawasiliano, alijiondoa kwenye chama cha Mutharika Democratic Progressive Party mwaka uliopita na akaanzisha chama chake ili kushindana na Mutharika. Chilima amewaambia waandishi wa habari kuwa anatumai watu wengi watajitokeza kupiga kura na amani itadumu katika kipindi cha upigaji kura. 

“Ninatumai kwamba watu watajitokeza kwa wingi. Kufikia sasa watu wengi wamejitokeza na tunatumai wengi watajitokeza zaidi katika vituo vyote vya kupiga kura nchini kote siku ya leo.” Amesema Chilima.

Chilima haswa amewalenga vijana ambapo aliimarisha kampeni zake kupitia mitandao ya kijamii huku akichapisha video za muziki aina ya kufoka au hip-hop. Asilimia 54 ya wapiga kura Malawi ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 na 34, huku wanawake wakiwa ni asilimia 56. Licha ya asilimia kubwa ya wapiga kura kuwa wanawake, hakuna mgombea yeyote wa urais ambaye ni mwanamke.

Wapiga kura kwenye foleni katika kituo cha kupiga kura karibu na mji mkuu Blantyre.

Tume inayosimamia uchaguzi Malawi imesema mfumo wao wa uchaguzi upo imara na hauwezi kudukuliwa.

Chakwera ambaye ana umri wa miaka 64 alishindwa na Mutharika katika uchaguzi uliopita mwaka 2014. Wakati huu amejiunga na rais aliyekuwa mtangulizi wa Mutharika Joyce Banda kwa lengo la kushinda. Chilima pamoja na Chakwera wameahidi kupambana na ufisadi nchini Malawi.

Tume inayosimamia uchaguzi Malawi imewaahidi wananchi kuwa mfumo wao wa upigaji kura upo salama na hauwezi ukadukuliwa. Mwenyekiti wa tume hiyo Jane Ansa amesema kuwa hakuna mitandao ya mawasiliano ambayo itafungwa wakati wa kipindi cha uchaguzi.

Malawi hutegemea pakubwa misaada ya kigeni na mara kwa mara hukumbwa na ukame ambao hutishia maisha ya maelfu ya watu.

Vyanzo: AP, RTRE, AFPESource link

Maafisa wa Kenya waenda Dubai kufuatilia kashfa ya dhahabu bandia


Wakati huohuo, pirikapirika zinaripotiwa bungeni za kusaka saini ili kumtimua waziri wa usalama wa taifa, Fred Matiangi, kwa madai ya kuwalinda watuhumiwa wa kashfa hiyo.

Polisi nao wanashikilia kuwa maafisa wao waliokuwako kwenye eneo ilikopatikana dhahabu hiyo bandia walikuwa wanawalinda wanadiplomasia na wala sio wahalifu.

Maafisa wa idara ya ujasusi walitazamiwa kusafiri jioni ya Jumanne (21 Mei) kuelekea Dubai ili kuchukuwa taarifa ya mwakilishi wa Umoja wa Falme za Kiarabu kuhusu sakata hilo la dhahabu bandia linalochunguzwa.

Majasusi hao walitazamiwa kumhoji Ali Zandi anayemuwakilisha Sheikh Mohammed bin Rashid Al Maktoum na kampuni ya Zlivia inayofanya biashara ya dhahabu Dubai.Source link

Timu ya La Liga Sevilla FC kutua Tanzania kwa mpambano wa kirafiki dhidi ya Simba SC


Sevilla celebrate

Haki miliki ya picha
EPA

Timu ya La Liga Sevilla FC ipo njiani kuelekea Tanzania kwa mpambano wa kirafiki dhidi ya vinara wa ligi ya Tanzania Simba SC.

Mapema leo, timu hiyo ya ligi ya Uhispania imeondoka kuelekea Tanzania kwa mchuano wa kirafaiki dhidi ya timu ya Tanzania Simba SC Alhamisi wiki hii.

Mpambano huo ni sehemu ya kampeni ya ‘LaLiga World Challenge’ inayonuiwa kusambaza soka ya Uhispania duniani kutokana na kuongezeka kwa ushabiki wa ligi kuu ya Uhispania LaLiga.

Mashabiki sugu wa soka Tanzania wanasubiria mchauno huo kwa shauku kubwa.

Katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii Instagram kikosi cha Sevilla kimetuma ujumbe kwamba kipo njiani:

Kikosi hicho inaarifiwa kinajumuisha Vaclík, Juan Soriano, Sergi Gómez, Kjaer, Gnagnon, Jesus Navas, Aleix Vidal, Escudero, Arana, Amadou, Roque Mesa, Banega, Franco Vazquez, Nolito, Promes, Bryan, Ben Yedder na Munir.

Simba SC ni mabingwa mara 19 Tanzania na wamefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kusubiri kwa miaka 25.

Moja ya chachu ya ushindi kwa Simba wakiwa nyumbani ni nguvu kubwa ya mashabiki wao ambao wamekuwa wakiujaza Uwanja wa Taifa unaoingiza mashabiki 60,000.

Baadhi wakionekana tayari kunoa makali kufuatia kuwadia kwa mchuano huo wiki hii katika uwanja wa taifa Dar es Salaam.

Sevilla FC ni klabu ya kwanza ya Uhispania kuizuru Tanzania kucheza mechi ya kirafiki na ni ya pili Ulaya baada ya Everton kushuka pia mnamo 2017 ilipochuana na timu bingwa Gor Mahia kutoka Kenya katika mashindano ya Sport Pesa.Source link

Javad Zarif: Vitisho vya Marekani haviwezi 'kuangamiza' Iran


waziri wa maswala ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif (24 April 2019)

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Mohammad Javad Zarif amesisitiza kuwa Iran haitaki vita na Marekani

Waziri wa maswala ya kig ni nchini Iran Javad Zarrif amepuuzilia mbali madai ya rais Donald Trump ya kuiangamiza Iran na kumuonya kutolitishia taifa hilo.

Huku kukiwa na hali ya wasiwasi , bwana Trump alituma ujumbe wa Twitter siku ya Jumapili akisema: Iwapo Iran inataka kupigana hiyo ndio utakuwa mwisho wake.

Bwana Zarif alisema kuwa rais huyo wa Marekani anafaa kutazama historia. ” Iran imeshinda vita vyote dhidi ya wachokozi wake …jaribu kuwa na heshima -utafanikiwa!

Marekani imeongeza idadi ya meli na ndege zake za kivita katika eneo la mashariki ya kati katika siku za hivi karibuni.

Ujumbe huo wa Bwana Trump unaadhimisha mabadiliko ya matamshi yake baada ya kusema kuwa hakutakuwa na vita kati ya Marekani na Itran.

Alipoulizwa na maripota siku ya Alhamisi iwapo Marekani itaelekea katika vita , alisema: Sidhani.

Vyombo vya habari vya Iran viliripoti siku ya Jumatatu kwamba taifa hilo limeongeza mara nne uzalishaji wa madini ya Uranium ambayo yalikuwa yamepunguzwa hadi kilo 300 na mpango wa kinyiuklia wa 2015 kati ya Iran na mataifa yenye uwezo mkubwa duniani.

Msemaji wa shirika la kawi ya Atomiki Behrouz Kamalvandi, amesema kuwa Iran itazidisha kiwango cha uzalishaji wa madini ya Uranium na kupitisha kiwango ilichowekewa katika siku za usoni.

“Iwapo wanataka sisi kusalia na kiwango tulichokubaliana katika makubaliano ya mpango huo wa kinyuklia , basi itakuwa vyema kwa mataifa ya Ulaya kuchukua hatua inazotaka ili kutekeleza haraka iwezekanavyo.

Bwana Trump aliiondoa Marekani katika mkataba huo ,mwaka uliopita , lakini mataifa ya Ulaya yanasema kuwa bado yanaheshimu makubaliano hayo.

Onyo la rais huyo wa Marekani siku ya Jumapili lilitolewa saa chache baada ya roketi kurushwa katika eneo linalolindwa sana katika mji mkuu wa Iraq, baghdad na kupiga jengo moja yapata mitaa 500 kutoka katika ubalozi wa Marekani.

Marekani hivi majuzi iliwaondoa wafanyikazi wake nchini Iraq katka kile ilichokitaja kuwa tishio kutoka kwa vikosi vinavyoungwa mkono na Iran nchini Iraq.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Roketi ilianguka mita 500 kutoka kwa ubalozi wa Marekani uliopo mjini Baghdad Iraq

Akiandika siku ya Jumatatu , waziri wa maswala ya kigeni nchini Iran alisema kuwa rais huyo wa Marekani alikuwa akishinikizwa na kile alichokiita Kundi B – mshauri wake wa Usalama John Bolton, Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mwanamfalme wa Saudia Mohammad bin Salman.

”Bwana Trump anataka kupata mafanikio pale ambapo Alexander The Great, Genghis[Khan} na wachokozi wengine walishindwa kufanya. Raia wa Iran wamesimama huku wachokozi wakianguka.

”Uchokizi wa ugaidi wa kiuchumi na uchokozi mwengine wa kuangamiza watu hautaimaliza Iran”, aliongezea.

”Usijaribu kuitishia Iran ,jaribu kuiheshimu utafanikiwa”.

Je chanzo cha uhasama huo ni nini?

Uhasama huo ulianza mapema mwezi huu , wakati Marekani iliondoa msamaha wake wa vikwazo kwa mataifa yanayonunua mafuta kutoka kwa Iran.

Uamuzi huo ulilenga kusitisha uuzaji wa mafuta wa Iran katika mataifa ya kigeni hatua ambayo ingelinyima taifa hilo chanzo cha mapato.

Bwana Trump aliirudishia vikwazo Iran baada ya kujiondoa katika mpango wa kinyuklia wa 2015 kati ya Iran na mataifa yenye uwezo mkubwa duniani ambao anataka ujadiliwe tena.

Siku chache baadaye, rais wa Iran Hassan Rouhani alisema kuwa taifa linasitisha vikwazo ilivyowekewa katika makubaliano hayo na kutishia kuongeza uzalishaji wa madini ya Uranium iwapo mataifa ya magharibi hayatachukua hatua za kulinda mafuta yake na sekta yake ya benki kutokana na athari za vikwazo vya Marekani kwa miezi miwili.

Baadaye ikulu ya Whitehouse ilitangaza kwamba Marekani ilikuwa inatuma meli ya kubeba ndege za kivita B-52 pamoja na kifaa cha kutungua makombora angani katika eneo la mashariki ya kati kutokana na vitisho vya Iran.

Je mataifa mengine yanasema nini?

“Ningeishauri Iran musidharau ari ya Marekani , alisema waziri wa maswala ya kigeni wa Uingereza Jeremy Hunt.

”hawataki vita na Iran. lakini iwapo maslahi ya Marekani yatashambuliwa , watalipiza kisasi”.

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Meli ya kubeba ndege ya marekani USS USS Abraham Lincoln

“Tunataka hali ya wasiwasi kupungua , kwasababu huu ni ulimwengu ambao mambo yanaweza kuchochewa kwa urahisi” ,aliongezea.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Saudia Adel al-Jubeir alisema kuwa Ufalme wa Saudia hautaki vita na utatumia kila njia kusitisha vita.

“lakini upande mwengine iwapo utataka vita , Ufalme huo utajibu na nguvu zake zote kujitetea na kulinda maslahi yake”.

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Oman ambayo ilisimamia mazungumzo ya kisiri hapo zamani kati ya Marekani na Iran, alizuru Iran ili kujadiliana kuhusu maswala ya kieneo na waziri wa maswala ya kigeni nchini Iran Javad Zarif siku ya Jumatatu.Source link

Huawei kutotumia Android: Afrika inaathirika namna gani?


Huawei

Haki miliki ya picha
Getty Images

Bara la Afrika kuna takriban watu milioni 400 wanaotumia mtandao na kati ya hao kuna 60% wanatumia mfumo wa Android ambao ndio unatumikwa kwa simu kama za Huawei.

Ikiwa na soko lenye ukubwa wa takribani asilimia kumi na sita duniani, kampuni hiyo inatajwa kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa kubwa zaidi ya utengenezaji simu.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na hofu kutoka baadhi ya wadadisi kwamba huenda kampuni hiyo inatumiwa na Uchina kufanyia serikali za nje na pia wananchi wake ujasusi.

Lakini barani Afrika, kampuni hiyo pamoja na ile ya ZTE zimehusika sana katika ujenzi wa miundo mbinu nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, miongoni mwa mataifa mengine.

Nchini Nigeria kwa mfano, Huawei ilishinda kandarasi ya dola milioni themanini kutengeneza mtandao wa dijitali wa simu wa GSM mnamo mwaka 2004.

Kwa kutathmini ukubwa wa uwepo wa kampuni hiyo Afrika wadadisi wanasema mzozo unaoshuhudiwa sasa inamaanisha kwamba biashara nyingi zitaathirika kutokana na changamoto ambazo Huawei inakumbana nazo.

Barrack Otieno ambaye ni mtaalamu wa maswala ya sera za mtandaoni anaeleza kwamba, ‘Waafrika wengi wanapokea mikopo midogo kupitia programu tumishi za simu ambazo zinatumia mfumo huo wa Android. Huenda sasa ikachangia watu wengi wakakosa mikopo na hivyo kuumia sana katika sekta za kibiashara’.

Huawei pia imezindua zaidi ya mitandao hamsini ya 3G, na kutengeneza mitandao ya huduma za zaidi ya serikali thelathini. Aidha kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika teknolojia zinazokua za 4G na 5G.

Mauzo ya Huawei yamekuwa katika kila bara

Mapato ni ya mabilioni ya dola za Marekani

Je kuna namna ya kuiepuka athari?

Wananchi wengi hununua simu za Huawei kwasababau ni za bei nafuu katika masoko ya simu Afrika.

Wanauchumi wanaonya ikiwa simu hizo sasa zitaondolewa katika soko kutokana na athari ya yanayoshuhudiwa, ina maana itaathiri pia uchumi wa kieneo, na zaidi ‘nchi ambazo hazina nguvu kiuchumi’.

Serikali nyingi Afrika zinatumia teknolojia na miundo mbinu ya Huawei. Je zinapaswa kuwa na wasiwasi?

Barrack Otieno anasema huenda biashara nyingi zikasambaratika kwasababu biashara nyingi zimeundwa kwa msingi wa biashara ya Huawei.

‘Kusema kwamba biashara hizo zibadilishwe kwa muda mfupi kama inavyopendekeza Marekani itakuwa sio jambo la rahisi’ anaeleza.

Image caption

Barrack Otieno ambaye ni mtaalamu wa maswala ya sera za mtandaoni

Marufuku iliyoidhinishwa kwa Huawei kutotumia mfumo wa Android unagubika uzinduzi hii leo kwa simu mpya za kampuni hiyo ya China.

Huawei imealikwa waandishi wa habari wa kimataifa kushuhudia uzinduzi wa simu mpya za Honor 20 Series.

BBC inafahamu kwamba simu hizo zitakuwa na uwezo wa kutumia kikamilifu Android.

Mwaka jana, Huawei iliunda simu milioni mia mbili na nane, huku nusu ya simu hizo zikiuzwa nje ya Uchina.

Huawei inaunda simu zaidi kushinda Apple

Hisa ya soko ya kampuni za kutengeneza simu (%)

Julai mwaka huo huo, kampuni hiyo iliipiku mshindani wake Apple na kuchukua nafasi ya pili katika utengenezaji simu janja duniani, huku Samsung ikisalia kileleni.

Lakini mpaka pale tofuai za kibiashara na Marekani zitakapotatuliwa, huenda simu zitakazo zinduliwa katika miaka ijayo zikawa na manufaa kidogo – iwapo hazitotumia mfumo huo wa Android.

Na pia haijulikani wazi iwapo marufuku ya Google kwa Android ni ya muda mrefu.Source link

Uchaguzi wa rais waendelea nchini Malawi


Malawi inafanya uchaguzi wake mkuu leo kumchagua rais mpya pamoja na wabunge. Shughuli za upigaji kura zilianza mapema leo katika vituo vya upigaji kura. Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika aliye na umri wa miaka 78 anawania muhula wa pili huku akikabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa makamu wake na mgombea wa chama kikuu cha upinzani.

Vituo vya upigaji kura vilifunguliwa mwendo wa saa kumi alfajiri majira ya nchi hiyo, na inatarajiwa kuwa wapiga kura milioni 6.8 waliosajiliwa watashiriki kwenye uchaguzi huo wa rais, wabunge na madiwani.

Wapiga kura wameelezea matumaini ya kuwachagua viongozi wanaowapenda kuleta maendeleo.

Wachambuzi wanatarajia ushindani kuwa mkali kati ya rais Peter Mutharika, makamu wake Saulos Chilima na kutoka kwa Lazarus Chakwera ambaye anaongoza kundi la vyama vya upinzani Malawi Congres Party.

Wapiga kura kwenye foleni katika kituo cha kupiga kura karibu na mji mkuu Blantyre.

Wapiga kura kwenye foleni katika kituo cha kupiga kura karibu na mji mkuu Blantyre.

Rais Mutharika mwenye umri wa miaka 78 alitekeleza maendeleo ya miundombinu na alipunguza viwango vya mfumuko wa bei ya bidhaa nchini humo katika muhula wake wa kwanza madarakani. Lakini wakosoaji wanamshutumu kwa kuendeleza ufisadi na upendeleo, madai ambayo Mutharika hukanusha.

Chilima mwenye umri wa miaka 46 na ambaye ni mkuu wa zamani wa kampuni ya mawasiliano, alijiondoa kwenye chama cha Mutharika Democratic Progressive Party mwaka uliopita na akaanzisha chama chake ili kushindana na Mutharika. Chilima amewaambia waandishi wa habari kuwa anatumai watu wengi watajitokeza kupiga kura na amani itadumu katika kipindi cha upigaji kura. 

“Ninatumai kwamba watu watajitokeza kwa wingi. Kufikia sasa watu wengi wamejitokeza na tunatumai wengi watajitokeza zaidi katika vituo vyote vya kupiga kura nchini kote siku ya leo.” Amesema Chilima.

Chilima haswa amewalenga vijana ambapo aliimarisha kampeni zake kupitia mitandao ya kijamii huku akichapisha video za muziki aina ya kufoka au hip-hop. Asilimia 54 ya wapiga kura Malawi ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 18 na 34, huku wanawake wakiwa ni asilimia 56. Licha ya asilimia kubwa ya wapiga kura kuwa wanawake, hakuna mgombea yeyote wa urais ambaye ni mwanamke.

Wapiga kura kwenye foleni katika kituo cha kupiga kura karibu na mji mkuu Blantyre.

Tume inayosimamia uchaguzi Malawi imesema mfumo wao wa uchaguzi upo imara na hauwezi kudukuliwa.

Chakwera ambaye ana umri wa miaka 64 alishindwa na Mutharika katika uchaguzi uliopita mwaka 2014. Wakati huu amejiunga na rais aliyekuwa mtangulizi wa Mutharika Joyce Banda kwa lengo la kushinda. Chilima pamoja na Chakwera wameahidi kupambana na ufisadi nchini Malawi.

Tume inayosimamia uchaguzi Malawi imewaahidi wananchi kuwa mfumo wao wa upigaji kura upo salama na hauwezi ukadukuliwa. Mwenyekiti wa tume hiyo Jane Ansa amesema kuwa hakuna mitandao ya mawasiliano ambayo itafungwa wakati wa kipindi cha uchaguzi.

Malawi hutegemea pakubwa misaada ya kigeni na mara kwa mara hukumbwa na ukame ambao hutishia maisha ya maelfu ya watu.

Vyanzo: AP, RTRE, AFPESource link