Aaron Wan-Bissaka: Man Utd yathibitisha kumsajili mlinzi wa Crystal Palace


Aaron Wan-Bissaka

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Aaron Wan-Bissaka ameiwakilisha Crystal Palace marakatika mechi 35 za ligi kuu ya England msimu wa mwaka 2018-19

Manchester United wamemsajiili beki wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka kwa mkataba wa pauni milioni 50.

Kiungo huyo wa miaka 21 amekubali kutia saini mkataba wa miaka mitano utakaomwezesha kulipwa hadi pauni 80,000 kwa wiki.

United tayari imelipa £45m kumnunua Wan-Bissaka amabye anatajwa kuwa mchezaji wa tano mkubwa kusainiw ana klabu hiyo baada yaPaul Pogba, Romelu Lukaku, Angel di Maria na Fred.

“Siamini nimejiunga na Ma Utd kwa kweli najivunia sana usajili huu,” Wan-Bissaka alisema.

Manchester United imethibitisha usajili wake leo Jumamosi.

Kocha wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer amesema Wan-Bissaka ni “mmoja wa walinzi wakuu wanaoibuka katika ligi ya Premia”.

Aliongeza kuwa: “Ana eshiku kazi yake, ana talanta kubwa inayomwezesha kuchezea Manchester United na ana vigezo vyote vya mchezaji tunayemtaka ajiunge na kikosi chetu na bila shaka atatusaidia kufikia malengo.”

Mlinzi huyo ni ni wa pili kusajiliwa na klabu hiyo, baada ya usajili wa kiungo wa kimataifa wa Wales Daniel James, 21, ambao alijiunga na United kutoka Swansea kwa £15m.

United wana nafasi ya kurefusha mkataba wa miaka mitano wa Wan-Bissaka hadi miaka sita.

Haki miliki ya picha
Manchester United

Image caption

Aaron Wan-Bissaka ametiia siani mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo

Wan-Bissaka, ambaye alikuwa akitekeleza wajibu wake wa kimataifa mwezi huu katika michuano ya Ulaya ya wachezaji wa chini ya miaka 21 alijiunga na chuo cha mafunzo ya mpira ya Palace akiwa na miaka 11.

Nyota huyo alikuwa akilipwa pauni £10,000 kwa wiki katika uwanja wa Selhurst Park, kiwango ambacho ni cha chini kulipwa mchezaji wa kikosi cha kwanza.

Uhamisho wake ulicheleweshwa na mashauriano ya mwisho kati ya vilabu hivyo, hatua ambayo iliiwezesha Eagles kupata 10% ya mauzo ya Wan-Bissaka ikwa kujiunga na United kwa zaidi ya pauni £50m.

Huku hayo yakijiri United ina pania kumpatia mkataba wa muda mrefu mshambuliaji Marcus Rashford.

Mkatama wa sasa wa mchezaji huyo wa miaka 21-unakamilika 2020 na mazungumzo ya kurefusha mkataba wakeyamekuwa yakiendelea kwa miezi kadhaa sasa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *