AFCON 2019: Mataifa manne yanashuka dimbani, mawili kusonga fainali


Riyad Mahrez

Haki miliki ya picha
Reuters

Tayari kivumbi kimeshaanza katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Afcon 2019 baina ya Senegal na Tunisia.

Wengi wanatazamia Senegal ambaye hajawahi kuchukua kombe la Afcon kumfunga bingwa wa zamani Tunisia.

Si mchezo mwepesi, kwani timu zote zimeonesha kiwango cha juu mpaka kufikia hatua hii.

Itakapotimu nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki, nusu fainali ya pili baina ya Algeria na Nigeria pia itapigwa hapa hapa jijini Cairo.

Nigeria ndiyo timu pekee kati ya zilizosalia ambazo imeshinda kombe hilo zaidi ya mara moja.

Hata hivyo usiku wa leo, watakuwa na kibarua kizito mbele ya Algeria ambayo wengi wanaipigia upat kutoka na ushindi.

“Timu zote nne zinauwezo wa kushinda,” mshambuliaji wa Nigeria Alex Iwobi amaiambia BBC “Wote tuna wachezaji wazuri. Siwezi kujua nani ambaye ana nafasi kubwa zaidi ya kuwa bingwa kwa wakati huu.”

Haki miliki ya picha
Getty Images

Bingwa asiyetarajiwa?

Haki miliki ya picha
Reuters

Timu tatu zenye mafanikio makubwa zaidi Afrika – Misri, Cameroon na Ghana – ziling’olewa kwenye hatua ya mtoano, na kuicha Nigeria pekee katika mashindano kama timu yenye mafanikio zaidi.

Kombe la mwisho kunyanyua ilikuwa mwaka 2013, na ulikuwa uchampioni wao wa tatu.

Senegal, ambao wameshawahi kufika hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia, hawajawahi kushinda Afcon.

Kivumbi kutifuka nusu fainali ya Afcon

Mwaka bora zaidi kwao ulikuwa ni 2002 walipocheza fainali dhidi ya Cameroon na kupoteza kwa ikwaju ya penati.

Tunisia wameshinda mara moja mwaka 2004, huku Algeria ikishinda 1990.

Fainali itapigwa Ijumaa katika Dimba la Kimataifa la Cairo kuanzia saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Nani anapigiwa chapuo?

Haki miliki ya picha
EPA

Senegal ndio chaguo la wacheza kamari wengi, wakifuatiwa na Algeria.

Kwa maana hiyo, itakuwa fainali ya timu zilizotoka kwenye kundi C.

Kundi ambalo yalikuwemo mataifa ya Tanzania na Kenya.

Cheza: Nani mshindi AFCON kwa mambo mengine kando na soka?

Algeria ndiyo timu ambayo imekuwa na mashindano mazuri mpaka sasa, kwa kushinda michezo yote – ikiwemo ushindi wa 1-0 dhidi ya Senegal katika hatua ya makundi.

Baada ya hapo wakaitandika Guinea 3-0 kwenye hatua ya mtoano, na kisha kuwaondoa Ivory Coast kwa penati kwenye robo fainali.

Senegal ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi C na kisha kuwatoa Uganda kwenye hatua ya mtoano na kisha Benin katika hatua ya robo fainali.

Nigeria ilimaliza nafasi ya pili kwenye makundi nyuma ya Madagascar, wakawavua ubingwa Cameroon kwenye hatua ya mtoano na kuindoa Afrika Kusini kwenye robo fainali.

Tunisia walipenya kutoka Kundi E kwa kutoka sare michezo mitatu, kisha kuwatoa Ghana kwenye hatua ya 16 bora kabla ya kuwang’oa Madagascar katika hatua ya robo fainali kwa goli 3-0.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *