Afcon 2019: Nigeria kupambana na Algeria huku Senegal ikichuana na Tunisia


Ivory Coast yashindwa kufuruka mbele ya Algeria

Haki miliki ya picha
Reuters

Tunisia ilifika katika nusu fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza tangu 2004 baada ya kuilza Madagascar.

Mwewe hao wa Carthage , ambao sasa watapambana na Senegal siku ya Jumapili katika nusu fainali waliongoza kupitia bao la Ferjani Sassi .

Youssef Msakni baadaye alifunga goli la pili baada ya shambulio la Wahbi Khazri kupanguliwa na Melvin Adrien.

Naim Sliti aliipatia Tunsia bao la tatu katika muda wa lala salama na kuwakata makali wachezaji wa Madagascar ambao walikuwa wakilivamia lango la Tunisia kama nyuki waliotoka katika mzinga.

Wakati huohuo Algeria ilitinga nusu fainali ya Kombe la mataifa ya Afrika baada ya kuilaza Ivory Coast 4-3 kupitia penalti baada ya sare ya 1-1 baada ya muda wa zaida.

Algeria ilichukua uongozi kupitia winga wa zamani wa klabu ya West Ham Sofiane Feghouli kabla ya kupoteza mkwaju wa penalti.

Baghdad Bounedjah ambaye alikuwa amechezewa visivyo katika lango la Ivory Coast aligonga mwamba wa goli alipozawadiwa penalti hiyo.

Ivory Coast ililazimisha muda wa ziada baada ya mshambuliaji wa Aston Villa Jonathan Kodja kufunga bao zuri.

Na baada ya sare hiyo uamuzi wa kupiga penalti ulitolewa.

Algeria ambayo inatafuta ushindi wa kwanza wa kombe hilo tangu 1990 sasa itakutana na Nigeria mjini Cairo siku ya Jumapili.

Ivory Coast ilikuwa imekaribia kufunga wakati ambapo timu zote zilikuwa hazijaona lango la mpinzani huku kipa Rais M’bolhi akipangua shambulio la Max Gradel.

Mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha alikaribia kufunga kufunga goli lake la tatu.

Haki miliki ya picha
Reuters

Hatahivyo raia huyo wa Ivory Coast alipewa kadi ya njano baada ya kuzua mgogoro na Bensabaini.

Zaha na mshambuliaji wa Algeria Riyad Mahrez walitolewa kufikia mwisho wa dakika 120 na hawakushiriki katika upigaji wa penalti.

Wakati huohuo Madagascar ambao wanaorodheshwa wa 108 duniani na Fifa waliwawacha wengi vinywa wazi baada ya kufika robo fainali licha ya kushiriki kwa mara ya kwanza.

Waliwalaza Nigeria na DR Congo katika mchuano ya muondoano.

Kikosi chao kinashirikisha wachezaji wanaosakata kandanda Reunion, na ligi ndogo za Ufaransa na Thailand.

Mkufunzi wao Nicolas Dupuis ndiye kocha wa klabu ya daya la nne ya Fleury.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *