Afghanistan: Marekani yajitolea kuwafidia jamaa za wahasiriwa wa shambulio ndege Kabul


Matokeo ya shambulio la ndege isiyo na rubani katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul
Maelezo ya picha,

Matokeo ya shambulio la ndege isiyo na rubani katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul

Serikali ya Marekani imejitolea kuwafidia jamaa za wahasiriwa waliouawa kimakosa katika shambulio la ndege isiyo ya rubani iliyofanywa na majeshi yake dhidi ya mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, mwezi Augosti.

Mfanyakazi wa kutoa msaada na jamaa tisa wa familia yake, wakiwemo watoto saba, walifariki katika shambulio hilo.

Pentagon ilisema inafanya kazi kusaidia jamaa wa familia hiyo walionusurika kuhamia Marekani.

Shambulio hilo lilifanyika kabla ya Marekani kuondoa vikosi vyake nchini humo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *