Afghanistan: Viongozi wa Taliban wazozana Ikulu, vyanzo vimeeleza


Mullah Abdul Ghani Baradar alisaini makubaliano ya Doha kwa niaba ya Taliban kuhusu kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani

Chanzo cha picha, AFP

Mzozo mkubwa ulizuka kati ya viongozi wa Taliban kuhusu muundo wa serikali mpya ya kundi hilo nchini Afghanistan, maafisa wakuu wa Taliban wameiambia BBC.

Mabishano kati ya mwanzilishi mwenza wa kundi hilo, Mullah Abdul Ghani Baradar na mjumbe wa baraza la mawaziri yalitokea kwenye ikulu ya rais, walisema.

Kumekuwa na ripoti ambazo hazijathibitishwa za kutokubaliana ndani ya uongozi wa Taliban tangu Bwana Baradar alipopotea katika siku za hivi karibuni.

Madai haya yamekanushwa rasmi.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *