Afrika Kusini yatangaza maambukizi 10,107 kwa siku mojaWaziri wa Afya Zwelini Mkhize alitangaza Jumamosi usiku kuwepo maambukizi hayo mapya.

Vyanzo vya Habari vimeeleza maambukizi hayo hivi sasa ni zaidi ya asilimia 50 ya maambukizi yote yaliyoripotiwa barani Afrika katika nchi 54.

Afrika Kusini sasa ina jumla ya watu 503,000 wenye maambukizi ya COVID-19.

Takwimu zinaonyesha watu 8,153 wamekufa kutokana na COVID -19 nchini humo. Afrika Kusini ina idadi ya watu milioni 58.

Kwa mujibu wa ripoti za tafiti mbalimbali duniani taifa hilo hivi sasa linashika nafasi ya tano duniani kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya Covid-19.

Nchi ambazo zina maambukizi ya juu zaidi duniani ni Marekani, Brazil, Urusi na India.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *