Algeria: Wananchi wapinga kufanyika uchaguzi, wadai mageuzi kwanzaIkiwa imebaki wiki sita kabla ya uchaguzi huo kila upande unachukulia siku hiyo kama mtihani wa kupimana nguvu kuhusu mageuzi, kila upande unadai mageuzi makubwa yafanyike kabla ya uchaguzi huo.

Kwa mwezi wa tisa mfululizo sasa, kila wiki wanaharakati wanaandamana wakidai kuwepo utawala wa mpito kuchukua nafasi ya serikali iliyopo ya enzi ya Rais Abdelazizi Bouteflika iliyokuwa madarakani tangu Algeria kunyakua uhuru 1962.

Maandamano ya Alhamisi yanafanyika pia kuadhimisha kuanza kwa vita vya uhuru vilivyodumu miaka minane dhidi ya utawala wa kikoloni wa Ufaransa.

Kuna karibu wagombea 22 walojiandikisha kwa uchaguzi wa urais na kwa mara ya kwanza hakuna mgombea kutoka chama tawala cha muda mrefu cha FNL .

Jeshi la taifa lenye ushawishi mkubwa katika siasa za Algeria halimuungi mkono mgombea yeyote katika juhudi za kuwahakikishia wananchi kwamba uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Lakini wengi kati ya wanaoandamana hawaamini kama msimamo huo utaleta mabadiliko yeyote.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *