Amnesty International yalaani uamuzi wa Tanzania kuzuia raia kuishtaki Mahakama ya Afrika


Mahakama ya Afrika nchini Tanzania, ilisimamia kesi za kimbari za Rwanda

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mahakama ya Afrika nchini Tanzania, ilisimamia kesi za kimbari za Rwanda

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limesema uamuzi wa wa Tanzania kujitoa katika kifungu kinachowawezesha raia na mashirika yasiyo kuwa ya kiserikali kuishtaki serikali katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binaadamu inahatarisha ongezeko la ukandamizaji nchini humo.

Amnesty imesema kujitoa huko kunawanyima watu na mashirika mbali mbali uwezo wa kupata haki zao za kisheria.

Msemaji wa Amnesty barani Afrika , Japhet Biegon amesema ”kitendo hicho moja kwa moja kinageuka na kuwa kikwazo kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutokwenda mahakamani kutafuta haki zao kwa makosa ya ukiukwaji wa haki za kibinadamu, jambo ambalo ni dhahiri kuwa wanataka kukwepa wajibu wao.”

Mahakama hiyo inapatikana mkoani Arusha, kaskazini mwa Tanzania. Na nchi hiyo sasa itakuwa ya pili baada ya Rwanda kujiondoa kwenye kipengele hicho cha mkataba ulioanzisha mahakama hiyo.

Kwa muujibu wa shirika la Amnesty International, hatua hiyo inaweza kuzua wasiwasi kuhusiana na nchi hiyo ambayo rekodi za haki za kibandamu zimekuwa zikimulikwa ndani ya miaka michache iliyopita.

Katika barua kwa Umoja wa Afrika, ambao wanachama wake ndio waanzilishi wa mahakama hiyo, Tanzania ilielezea kuwa ilikuwa inajiondoa kwa kuwa mahakama hiyo imeshindwa kufanyia kazi maombi yake juu ya ruhusa ya watu na mashirika kushtaki serikali katika mahakama hiyo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *