Benjamin Griveaux: Video ya ngono yamfanya mshirika wa Macron kujiuzulu


Former government spokesperson and La Republique en Marche (LREM) candidate for the upcoming Paris 2020 mayoral election Benjamin Griveaux on 14 Feb

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Wakati anajiuzulu, Bwana Griveaux alisema hakuna anayestahili kuharibiwa sifa

Video ya ngono imemaliza ndoto ya mgombea wa chama tawala cha Ufaransa Benjamin Griveaux ya kuwa meya wa mji wa Paris.

Aliyekuwa msemaji wa serikali ya Rais Emmanuel Macron, ambaye tayari alikuwa anayumba yumba kwenye kinyang’anyiro alilengwa na msanii wa Urusi aliyemshtumu kwa unafiki.

“Hakuna ambaye anastahili kupitia unyanyasaji huo,” amesema Bwana Griveaux, 42.

Video hiyo inaonesha mwanamume akiwa katika hali tatanishi, ilisambaa kwa haraka katika mitandao ya kijamii Alhamisi jioni.

Petr Pavlensky, raia wa Urusi aliyeomba hifadhi ya ukimbizi, alisema kwamba ameweka video hiyo mtandaoni.

Wanasiasa Ufaransa wamesema nini?

Wapinzani kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa walionyesha hasira yao.

Meya wa sasa Anne Hidalgo alitoa wito wa kuheshimu maisha binafsi ya watu, huku kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto Jean-Luc Mélenchon akishtumu tukio hilo na kulitaja kama la kuchukiza.

Kiongozi wa mrengo wa kulia Marine Le Pen alisema kwasababu ya demokrasia, Bwana Griveaux hakuwa na haja ya kujiuzulu.

Benjamin Griveaux

AFP

My family doesn’t deserve this. I’m not prepared to expose my family and myself any more when all these attacks are allowed. This goes too far

Waziri Mkuu Edouard Philippe ameonesha kumuunga mkono aliyekuwa mfanyakazi mwenzake na waziri wa ndani Christophe Castaner na kuonya kwamba kuweka mtandaoni video kama hizo bila idhini ya mhusika ni kosa ambalo mtendaji anaweza kuadhibiwa na kutozwa faini kubwa na kifungo cha hadi miaka miwili jela.

Video hiyo ilionekana kwenye tovuti ambayo haifahamiki na wengi na kuandamana na wasifu wa Griveaux na malengo yake ya kisiasa pamoja na imani yake kali katika maadili ya familia.

Kisha makala iliyoandikwa iladai kwamba bwana Griveaux alikuwa amebadilishana ujumbe wa mapenzi kwa njia ya simu na mwanamke kijana na kumtumia video binafsi.

Kiunganishi cha kwenye mtandao ya kijamii kilisambazwa na mbunge ambaye alilazimika kujiuzulu kutoka kwa chama cha Macron mwishoni mwa mwaka 2018.

Bwana Griveaux amekiambia kituo cha BFMTV kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, yeye na familia yake wameharibiwa sifa, wamesemwa kwa maneno ya uwongo, uzushi, kushambuliwa na watu wasiowafahamu na hata kupata vitisho vya kifo.

“Uchafu huu umeniathiri mimi na zaidi kuumiza watu ambao ninawapenda.”

Wakili wa Griveaux amesema kuwa atawasilisha mashtaka dhidi ya video iliyowekwa mtandaoni ambayo alisema inakiuka faragha ya mtu.



Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *