Binadamu walianza lini kuongea, na kwa nini?


A row of people holding speech bubble posters

Haki miliki ya picha
Getty Images

Watu wa kale walianza kujifunza lini kuzungumza? Je, inawezekana kufahamu asili ya maelfu ya lugha zinazozungumzwa leo kutoka kwa mtu mmoja wa kale?

Mwandishi na mtaalamu wa lugha Michael Rosen anatafit

Maendeleo

Haki miliki ya picha
Getty Images

Binaadamu ni viumbe ambao wana lugha, kitu kinachotufanya kuwa wa kipekee miongoni mwa wanyama wote, ” anasema Maggie Tallerman, Profesa wa masuala ya lugha katika chuo cha Newcastle.

Uwezo huu wa kuwasiliana unaonekana kama moja ya mabadiliko makubwa, kuliko mengine yeyote, na kwa sababu hii, watu wamekuwa na shauku ya kufahamu asili za lugha.

”Lugha ni moja kati ya vitu vinavyotufanya kuwa binaadamu, ” anasema Robert Foley, mwana anthropologia na profesa wa stadi za historia ya binaadamu katika Chuo cha Cambridge.

Hisia 5 za binadamu walizonazo baadhi ya wanyama

Lugha inaweza kuwa na umri wa miaka nusu milioni

Haki miliki ya picha
Getty Images

Kuna lugha zaidi ya 6,500 duniani siku hizi, lakini ni kwa namna gani wana sayansi watafahamu lugha ya kwanza kuliko zote?

Ikiwa tutaulizwa kuhusu kutaja ”lugha ya kale”, tunaweza kufikiri kuwa ni ya Babylon,Sanskrit au ya wamisri wa kale.

Profesa Tallerman anasema lugha nyingi tunazoziita kuwa za kale hazina zaidi ya umri wa miaka 6,000, umri sawa na lugha nyingine zozote zinazozungumzwa siku hizi.

Chanzo cha lugha kinaweza kuwa miaka takriban 50,000 iliyopita, na wataalamu wengi wa lugha wanafikiri ni miaka mingi zaidi nyuma.

”Wengi wetu tunaamini tunaweza kurudi nyuma miaka nusu milioni iliyopita anasema Profesa Tallerman.

Mtu wa kale

Haki miliki ya picha
Getty Images

Ingawa kuna utajiri wa lugha mbalimbali , ”inawezekana kuwa lugha zetu za sasa zinatokana na lugha za watu wa kale,”anasema profesa Foley.

Ingawa kunaweza kuwa na lugha nyingine nje ya vizazi vilivyotangulia, lugha tunazoziona sasa pengine zinatoka kwenye lugha hiyo hiyo.

Ushahidi wa mabaki ya watu wa kale

Haki miliki ya picha
Getty Images

Mabaki ya watu wetu wa kale, yanatupa viashiria vichache kufahamu lini tulianza kuzungumza.

”kuzungumza, kwa namna nyingine ni kupumua, ” anasema Profesa Foley, ”tunapumua tukitoa sauti mbalimbali.”

Ili kuweza kufanya hivyo, tunahitajika kuwa na uwezo wa kudhibiti misuli yetu zaidi ya miili yetu kama ”mapafu yetu yaliyojengeka na yenye neva nyingi zinazokwenda.

Binadamu wa dhahabu kuzikwa tena

Neva hizi zote zinamaana kuwa ”uti wetu wa mgongo ni mwembamba kiasi kwenye eneo hilo Julio ya sokwe, na mifupa yake inapaswa kuwa mipana pia.”

Ukitazama viumbe wa kale walioishi miaka takribani 600,000 iliyopita, wana eneo la uti wa mgongo lililotanuka.

Hii inatupa viashiria kufahamu ni lini mwanadamu alianza kutumia lugha.

Ushahidi wa kijenetiki

Haki miliki ya picha
Getty Images

Mbali na rekodi kuhusu mabaki ya watu wa kale,stadi za jenetiki pia zinatoa ishara namna ya kufahamu lugha ilianza lini.

Kuna jeni ziitwazo FOXP2, ambazo ziko kwa viumbe vyote,”anasema prof Foley, ”lakini sisi binadamu tunazo kwa kiasi kidogo”.

Mabadiliko ya jeni hii ”yanaweza kusaidia kueleza kwa nini binadamu wanaweza kuzungumza na solte hawawezi.Tunajua ushahidi huu ni muhimu kwenye maendeleo ya lugha na mazungumzo.

Ukubwa wa ubongo

Haki miliki ya picha
Getty Images

Je ubongo wa watu wa zamani husaidia kujua lugha ilianza lini? Hapana.

Kwa sababu ndogo tu kuwa hatujui ukubwa gani wa ubongohusaidia kuunda lugha.

”Ukweli ni kuwa viumbe sokwe ubongo wao ni mkubwa kuliko wa binadamu kwa kuwa walikuwa wanyama wakubwa,”anasema Prof Tallerman, mtafiti.

Neno la kwanza la binadamu pengine ni ”hey!

Haki miliki ya picha
Getty Images

Tunapozungumzia lugha ya kale-lugha iliyokuja kaabla ya lugha unayosoma sasa-tunaweza kusema maneno ya kwanza yalikuwa nini?

”Jibu la kweli kabisa ni kuwa hatufahamu” anasema Profesa Foley.

Tukitazama viumbe kama sokwe, wana kile wanaprimatolojia wanakiita ”maneno” kwa wanyama-hutoa sauti ambazo wanyama wengine watazibaini kama ”mwewe” ”chui” au tazama!”.

Mji wa kale wa ‘majitu’ wagunduliwa Ethiopia

Unaweza kujenga hoja kuwa vitu vidogovidogo kwenye mazingira yetu vingekuwa maneno ya kwanza kuzungumzwa na binadamu.

Maneno ya awali yangekuwa kama maneno ya kawaida tuliyonayo hivi leo kama vile “shh”, “psst”, “ooh”, “asante ” au “kwaheri”.

Maneno note haya hujitokeza kwenye lugha zote, lakini jambo moja kwa pamoja , maneno yakipangwa hayatengenezi sentensi yenye maana kwenye lugha.

Muda wa chakula pengine ni sababu ya kuwepo kwa maendeleo ya lugha

Haki miliki ya picha
Getty Images

Binaadamu wa zamani ”huenda walianza kushirikiana-na kuzungumza zaidi ili kunufaika katika mazingira yao na kula vyakula tofauti,” anasema profesa Tallerman.

Wazee wetu wa kale walianza kuchambua kinachofaa katika mizoga iliyoachwa na wanyama wakali.

”Lakini kama unataka kupata mabaki ya mizoga ambayo ni haki ya fisi basi unalazimika kuwa na wenzako karibu, kwa kuwa itakuwa hatari sana,” anasema profesa Tallerman.

Lugha pia ni muhimu”ikiwa unataka kupata mzoga mzuri, na unahitaji kuwaeleza wenzio kwamba kuna kitu kinachofaa kuliwa karibu.”

Hii ni sifa nyingine ya mawasiliano ya mwanadamu;unapotumia lugha kueleza wengine vitu ambavyo havipo kwa wakati huo, kwa sababu inawezekana kuwa inaweza kuwa kilitokea katika eneo jingine-au hata wakati mwingine.

Wito wa kula na kuishi unaweza kuwa chachu ya binaadamu kuwa na uwezo wa kuambizana kuhusu ”vitu wasivyoweza kuviona, lakini vipo,” kama vile uwepo wa chakula cha bure, anasema Profesa Tallerman.

Umbea pia pengine una mchango wake

Haki miliki ya picha
Getty Images

Hivyo kuboresha uwezo wetu wa kufanya kazi pamoja ni jambo la umuhimu kwenye maendeleo ya lugha.

”Ushirikiano ni chanzo- na pengine ushirikiano wa kijamii hufanya jamii ikue.

Thamani ya mazungumzo ya kawaida haiwezi kupuuzwa: ”kupiga soga, kuongea umbea ni afya kwa mazungumzo,” mtaalamu wa historia ya lugha, Dokta Laura Wright kutoka chuo kikuu cha Cambridge anaeleza.

Wakati mwingine, zaidi ya kuwafanya watu wafanye vitu, nia kuu ya lugha ni kujua kuhusu vitu.

lini tulianza kupeana simulizi?

Haki miliki ya picha
Getty Images

”Tunapaswa kuwa na maneno mengi ya lugha ili kuweza kutengeneza sentensi, kueleza hadithi,” anasema profesa Tallerm

Hili linawezekana kuwa lilianza miaka mingi-pengine maelfu ya miaka baada ya hatua za kwanza kabisa za kuanza kuzungumza.

Hatua ya kutoka lugha ya kale mpaka lugha ya kisasa ni hatua kubwa sana, ”lakini lugha zote zinazozungumzwa hii leo zina uhusiano,” anasema Profesa Foley.an.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *