Bobi Wine kurejelea kampeni zake Jumatatu licha ya kupingwa kwa mikutano ya hadhara


Ugandan riot police detain a supporter of presidential candidate Robert Kyagulanyi, also known as Bobi Wine, in Luuka district, eastern Uganda, 18 November 2020

Maelezo ya picha,

Supporters of presidential candidate Bobi Wine were detained on Wednesday and Thursday

Mgombea urais nchini Uganda wa chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP) Robert Kyagulanyi Ssentamu ambaye pia anajulikana kama Bobi Wine atarejelea shughuli zake za kampeni Jumatatu.

Kampeni za Bobi Wine zilikatizwa Jumatano baada ya kukamatwa katika eneo la Luuka na kupelekwa kituo cha polisi cha Nalufenya.

Katika ujumbe aliouweka hii leo kwenye mtandao wa Twitter, Bobi Wine ameashiria kutokata tamaa ya kile anachotaka kufikia.

Kwa mujibu wa msemaji wa chama chake cha NUP Joel Ssenyonyi, Bobi Wine atarejelea kampeni zake Jumatatu 23, Novemba katika eneo la Kyenjojo na Fort portal.

Pia inasemekana kwamba kuna mipango ya kupanga tena kampeni katika maeneo alikotakiwa kufika kabla ya kukamatwa.

Baada ya kuchiwa huru, Bobi Wine alisema wafuasi wake wamejitolea kuendelea kupigania mabadiliko nchini humo na kuongeza kuwa hatua ya kuongezwa kwa maafisa wa usalama ni ishara ya uoga, hofu na ukosefu wa matumiani.

Maelezo ya picha,

Waandamanaji walikusanya na kuchoma tairi za magari katika mji mkuu wa Kampala, mapema wiki jana

Bobi Wine alifanya maombi maalum na kutuma rambi rambi zake kwa familia zilizopoteza wapendwa wao wakati wa vurugu zilizotokea wiki jana baada ya kukamatwa kwake.

Jumamosi asubuhi, magari ya vikosi vya usalama yaliegeshwa katika maeneo tofauti mjini Kampala huku polisi wakishika doria katika maeneo karibu na makao makuu ya chama cha upinzani cha People’s Power.

Polisi imetangaza kuwa ni watu 28 waliofarika katika maandamano ya siku ya Jumatano na Alhamisi, japo vyombo vya habari nchini Uganda vinanukuu vyanzo vya hospitali kuu kwamba idadi ya waliofariki ni watu 37.

Bobi Wine aliachiwa kwa dhamana siku ya Ijumaa, baada ya kushtakiwa kwa kukiuka kanuni za kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka saba gerezani akipatikana na makosa.

Maelezo ya picha,

Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Kwa upande wake Rais Yoweri Museveni, ameweka wazi kwamba hakuna haja ya kuahirisha uchaguzi mkuu nchini Uganda.

Bwana Museveni ameongeza kuwa kutofanya mikutano ya kampeni sio mwisho wa dunia na hilo halitakubalika kipindi hiki cha janga la virusi vya corona.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *