Bunge la EAC kuchukua hatua kali kwa wanachama wasiolipa michangoKwa mujibu wa taarifa ya jumuiya Burundi inadaiwa dola milioni 13, Tanzania dola milioni 9, Kenya Dola milioni 8, Rwanda dola milioni 7 na Uganda dola milioni 2.

Bunge hilo Jumatano, limetaka Baraza la Mawaziri katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuelezea changamoto ya uhaba wa fedha unaoikabili sekretarieti hivi sasa na kuzihimiza nchi wanachama kutoa michango yao kwa wakati ili kufanikisha shughuli za jumuiya.

Sudan Kusini, ambayo ni mwanachama wa jumuiya hiyo, imepewa muda wa hadi mwisho wa mwezi wa Oktoba, 2019 kuwasilisha malimbikizo ya michango yake ya dola milioni 27.

Hoja hiyo imeibuka baada ya hivi karibuni Jukwaa la Asasi za Kiraia katika ukanda Afrika Mashariki (EACSOF) kutaka kufungua shauri katika mahakama ya jumuiya hiyo kutaka ufafanuzi wa kisheria kuhusu uhalali wa wanachama wasolipa ada zao kuendelea na uanachama wao.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *