CAG: ATCL imeingiza hasara ya bilioni 150 kwa miaka mitano


Ndege ya Dreamliner ilipowasili Tanzania Julai 2018

Chanzo cha picha, IKULU TANZANIA

Maelezo ya picha,

Ndege ya Dreamliner ilipowasili Tanzania Julai 2018

Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini Tanzania, Charles Kicheere, amesema Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeingiza hasara ya takribani Shilingi Bilioni 150 kwa miaka mitano iliyopita.

Kwa mujibu wa CAG, kwa mwaka mmoja uliopita, ATCL imeingiza hasara ya Shilingi bilioni 60. Bw. Kicheere ameyasema hayo leo Alhamisi alipokuwa akiwasilisha ripoti ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 Bungeni mjini Dodoma.

“Nilifanya ukaguzi wa kiutendaji katika shirika la ndege na kubaini yafuatayo; Hadi kufikia Juni serikali ilikuwa imenunua ndege nane kwa gharama ya shilingi trilioni 1.28 katika juhudi za kufufua kampuni ya ndege…Pamoja na kununua ndege hizo, kwa miaka mitano serikali imeisaidia kampuni ya ndege kiasi cha shilingi bilioni 153 kwa ajili ya shughuli za uendeshaji na maendeleo…kampuni imekuwa ikiingiza hasara kwa miaka mitano mfulululizo ya shilingi bilioni 150,” ameeleza.

CAG pia amezitaja changamoto zinazoikabili ATCL na kushauri zishughulikiwe na serikali ili kampuni hiyo ili kuimarisha utendaji kazi wake.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *