Chama cha ACT-wazalendo chasusia uchaguzi serikali za mitaa Tanzania


zitto

Image caption

kiongozi wa chama cha ACT-wazalando Zitto Kabwe

Chama kingine cha upinzani chenye ushawishi nchini Tanzania kimejitoa kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa wa nchi hiyo.

Wamejitoa katika Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanywa 24 Novemba 2019.

”Takribani, wananchi 173,593. Hata hivyo, kati ya wagombea wetu hao 173,593 waliochukua na kurejesha fomu za uteuzi, 166,649 walienguliwa katika mchakato wa Uchaguzi nchi nzima kwa sababu mbalimbali za kipuuzi na zisizo na mashiko kabisa kama ilivyoelezwa na Viongozi wetu katika nyakati mbalimbali za mchakato huu. Wanachama wa ACT waliobakizwa kwenye Uchaguzi mpaka saa Sita kamili mchana leo ni 6,944 tu sawa na 4% ya wagombea wote tulioweka.” Anasema Zitto Kabwe kiongozi wa chama cha ACT wazalendo katika mkutano na waandishi wa habari.

UnawUnaweza pia kusoma

Kamati ya Uongozi ya Chama Taifa ilikutana hii leo kujadili hali na mwenendo wa uchaguzi huo nchini Tanzania.

Lakini pia chama hiko kimedai kutumika vibaya kwa jeshi la polisi la nchini Tanzania kuingia mchakato wa uchaguzi huo.

Image caption

bendera ya chama cha ACT ikipepea

”Kumekuwepo na vitendo viovu vinavyofanywa na Jeshi la Polisi na watendaji wa Serikali kuwabughudhi Wagombea wetu, wanachama na viongozi wetu maeneo mbalimbali nchini. Serikali ya Rais Magufuli isitufikishe kuvuka mstari wa Uvumilivu.” Anaongeza Zitto Kabwe katika taarifa yake.

Mapema leo, Mbunge huyo Kigoma Mjini na kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo aliandika katika aliandika katika ukurasa wake wa twitter kuomba ushauri kwa umma kuwa wachukue hatua gani? katika mchakato unaondelea wa serikali za mtaa?

Unaweza pia kusoma:

Zitto Kabwe alitoa kauli hiyo mara baada ya chama kikuu cha upinzani nchini humo Chadema kutangaza kuwa kimejitoa katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa.

Aidha serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi imesema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika kama ulivyopangwa tarehe 24 mwezi Novemba mwaka huu.

Ufafanuzi huo umetolewa mapema hii leo katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni, Dodoma ambapo Mbunge wa Singida Kaskazini Justice Monko alitaka ufafanuzi wa serikali hasa baada ya Chama kikuu cha Upinzani nchini Tanzania Chadema kutangaza kujitoa rasmi katika mchakato wa Uchaguzi huo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *