Coronavirus: Hakuna mabadiliko ya mlipuko wa virusi vya corona licha ya kuongezeka China, kulingana na WHO


Vietnam imewatenga takriban watu 10,000 katika karantini katika vijiji vilivyopo kaskazini mwa Hanoi

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Vietnam imewatenga takriban watu 10,000 katika karantini katika vijiji vilivyopo kaskazini mwa Hanoi

Visa vya uogonjwa wa Coronavirus haviongezeki kwa kiwango cha juu nje ya China licha ya ongezeko la ugonjwa huo katika mkoa wa Hubei , kulingana na shirika la afya duniani.

Ongezeko la pekee ni lile la meli ya kitalii nchini Japan ambapo visa 44 vipya viliripotiwa na hivyobasi kuweka jumla ya walioambukizwa kuwa 218.

Pia imebainika kwamba hakuna mfumo wa jinsi watu wanavyoaga kulingana na WHO. Takwimu mpya kutoka katika mkoa wa Hubei sasa imefikia vifo 116 na visa 4,823.

Hilo ni ongezeko la chini ikilinganishwa na siku iliopita wakati kulipokuwa na ongezeko ambapo takriban vifo 240 viliripotiwa mbali na visa 15,000 vipya .

Hatahivyo visa vingi vinatoka Hubei ambapo watu wengi walipatikana na virusi hivyo hatari kulingana na Mike Ryan , mkuu wa mpango wa afya inayohohitaji dharura.

Hii haionyeshi mabadiliko makubwa kuhusu mtindo wa mlipuko huo alisema. Nje ya China kumekuwepo vifo viwili na visa 447 katika mataifa 24, alisema.

Siku ya Alhamisi Japan ilitangaza kifo chake cha kwanza cha virusi vya corona – ambaye alikuwa mwanamke mwenye umri wa miaka 80 ambaye alikuwa akiishi Kanagawa kusini magharibi mwa mji mkuu wa Tokyo.

”Mwanamke huyo alipatikana na virusi hivyo baada ya kifo chake na kwamba hakuwa na uhusiano wowote na mkoa wa Hubei nchini China ambao ndio chanzo cha mlipuko wa corona”., vilisema vyombo vya habari vya Japan.

Siku ya alhamisi wizara ya maswala ya nchi za kigeni nchini Marekani ilisema kwamba ilikuwa ina wasiwasi kuhusiana na athari za mlipuko huo nchini Korea kaskazini, ambayo kufikia sasa haijaripoti kisa chochote.

Marekani imesema kwamba itatoa usaidizi katika taifa hilo kulingana na wizara hiyo.

Ni nini kinachofanyika ndani ya meli ya Diamond Princess?

Meli hiyo imetengwa mjini Yokohama .

Sio abiria wote 3,700 waliofanyiwa vipimo. Watu wenye virusi hivyo wanapelekwa hospitalini katika nchi kavu ili kutibiwa huku wale walio ndani wakizuiliwa katika vyumba vyao

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Meli ya Diamond Princess ina abiria 3,700 – sio wote waliofanyiwa vipimo.

Hatahivyo siku ya Alhamisi Japan ilisema kwamba itaruhusu wale walio na umri wa miaka 80 ama zaidi ambao hawajapatikana na ugonjwa huo kutoka.

Waziri wa afya Katsunobu Kato amesema kwamba huenda wakaruhusiwa kutoka mapema siku ya Ijumaa lakini watalazimika kusalia katika nyumba watakazopewa na serikali , lilisema gazeti la Japan Times.

Wakati huohuo meli ya kitalii – MS Westerdam – iliokuwa ikibeba abiria 2000 ilitia nanga nchini Cambodia baada ya kufurushwa na bandari za Japan, Taiwan, Guam, Ufilipino na Thailand licha ya kukosa kuwa na mgonjwa ndani yake.

Njia gani mpya ya utambuzi iliotumika?

Jimbo ambalo linachukua zaidi ya 80% ya maambukizi nchini China – sasa linajumuisha “visa vilivyogunduliwa kliniki” katika idadi ya visa vilivyothibitishwa.

Hii inamaanisha ni pamoja na zile zinazoonesha dalili, na kuwa na skani ya CT inayoonesha mapafu yaliyoathirika, badala ya kutegemea tu vipimo vya nucleic acid.

Kati ya vifo vipya 242 mjini Wuhan, 135 ni vile vilivyotambulika kwa vipimo vya kliniki.

Hii ina maanisha kuwa, hata bila njia mpya, idadi ya vifo Hubei siku ya Jumatano ilikuwa 107, ikiwa ni idadi kubwa kwa jimbo hilo.

Kwa ujumla jimbo la Hubei lina maambukizi ya watu 48,206 yaliyothibitishwa.

Huwezi kusikiliza tena

Meli ya Utalii ya The Westerdam iliruhusiwa kutia nangaSihanoukville, Cambodia

Nini kilichosababisha ongezeko hilo Hubei?

Hadi kufikia ongezeko la siku ya Jumatano, idadi ya watu walioambukizwa virusi hivyo imeongeza idadi ya vifo nchini China kufikia 1350 huku takriban watu 60,000 wakiambukizwa kwa jumla.

Mshauri wa kiuchumi wa ikulu ya Whitehouse Larry Kudlow alisema kwamba kumekuwa na mshangao wa visa vipya nchini Marekani.

”Tunashangazwa na ukosefu wa uwazi unaotoka nchini China, hii idadi inaongezeka”, alisema.

”Utawala wa rais Trump pia haukufurahishwa kwamba China haikukubali ombi la Marekani kutuma wataalam ili kuisaidia China kukabiliana na mliupuko huo”, alisema bana Kudlow.

China iliwafuta kazi maafisa wawili katika mkoa wa Hubei saa chache baada ya takwimu mpya kufichuliwa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *