Coronavirus: Kenya yathibitisha mtu wakwanza amepona kabisa covid-19


Ushuru wa ziada utapunguzwa kutoka asilimia 16% hadi 14% kuanzia Aprili 2020

Image caption

Ushuru wa ziada utapunguzwa kutoka asilimia 16% hadi 14% kuanzia Aprili 2020

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa mtu wa kwanza amepona kabisa ugonjwa wa corona.

”Hii inamaanisha kuwa ugonjwa huu unaweza kukabiliwa”alisema rais Kenyatta katika hotiba yake kwa taifa.

Idadi ya walioambukizwa ugonjwa wa corona nchini Kenya imefikia 28.

Rais pia ametangaza hatua kadhaa ambazo zitasaidia serikali yake kukabili janga la corona ikiwa ni pamoja na amri ya kutotoka nje kuanzia Ijumaa Machi 27 kuanziasa moja usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi.

”Orodha kamili ya watu wanaotoa huduma muhimu ambao hawatathiriwa na amri hio itatolewa na wizara ya ya usalamma wa ndani” alisema rais Kenyata

Ushuru wa ziada utapunguzwa kutoka asilimia 16% hadi 14% kuanzia Aprili 2020.

Rais ametangaza hatua ya kupunguza mshahara wake kwa asilimia 80 huku mawaziri wake wakipunguza mshahara wao kwa asilimia 30.

Tunaendelea kukupatia maelezo zaidi juu ya taarifa hii…Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *