Coronavirus: Kwanini rais Trump ana imani na dawa ya Hydrochloroquine 'kutibu' virusi vya corona?


Tembe za Hydroxicloroquine

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Hydroxicloroquine ni dawa ya gharama ya chini abayo imetumika kutibu magonjwa kama vile ya malaria

Jina lake ambalo ni gumu kulitamka limekuwepo katika kinywa cha rais Trump, mara kwa mara rais huyo wa Marekani alitaja dawa aina ya hydroxychloroquine.

Rais huyo anaamini kwamba dawa hii inaweza kuleta tofauti kubwa duniani katika vita dhidi ya virusi vipya vya ugonjwa wa covid-19 katika mwili wa mwanadamu.

”Inaonekana kuwa na matumaini baada ya kutoa matokeo mazuri. Na tutahakikisha kwamba dawa hiyo inapatikana kila mahali mara moja”, alisema katika mkutano na vyombo vya habari wiki iliopita.

”Nafikiria huenda ikaleta manufaa na pengine hata kushindwa lakini nadhani inaweza., kutokana na kile ninachoona inaweza kubadilisha mambo”.

”Dawa hiyo ina uwezo mkubwa , ina uwezo mkubwa” , aliongezea.

Ijumaa iliopita alisisitiza uwezo wake na kusema kwamba idara ya chakula na dawa ilikuwa ikiifanyia majaribio.

Na siku ya Jumamosi alisisitiza kupitia mtandao wake wa Twitter ‘ Hydroxychloroquine na azithromycin zikitumika kwa pamoja zinaweza kuleta mafanikio makubwa katika historia ya tiba.

Idara ya chakula na dawa FDA imefanya kitu muhimu na natumai zote mbili zitaanza kutumika mara moja. Watu wanafariki , harakisheni na Mungu ambariki kila mmoja, aliandika.

Rais huyo alisema kwamba, tayari dawa hiyo imeidhinishwa na Idara hiyo ya chakula na dawa na kwamba kwa kuwa ni maarufu inaweza kutengenezwa kwa urahisi.

Hatahivyo idara hiyo ya chakula ilitoa taarifa ambapo ilisema kwamba dawa hiyo inafanyiwa majaribio katika maabara hivyo basi matumizi dhidi ya wagonjwa walioambukizwa virusi vya corona hayajaruhusiwa.

Dawa hiyo imetumika kwa miongo kadhaa katika tiba ya ugonjwa wa malaria.

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Rais Trump amekuwa na matumaini makubwa ya matumizi ya ya dawa ya hydroxychloroquine kutibu cirusi vya corona

Idara ya dawa nchini Marekani FDA inaamini kwamba ijapokuwa dawa hiyo ina uwezo mkubwa dhidi ya virusi vipya , ni lazima ifanyiwe majaribio ili kubaini iwapo ndio dawa inayoweza kukabiliana na virusi hivyo ambavyo tayari vimesababisha zaidi ya vifo 10,000 duniani.

”Ni dawa ambayo rais huyo ametaka kuiangazia kwa karibu ili kuona iwapo matumizi yake yanaweza kupanuka na iwapo itawasaidia wagonjwa”, alisema kamishna wa FDA Stephen Hahn.

Na wametoa wito wa dawa hiyo kutotumika bila ushauri wa mtaalam kwa kuwa tayari imeripotiwa kwamba baadhi ya waliotumia walitumia kiwango cha juu.

Mtu mmoja alifariki tarehe 23 mwezi Machi baada ya kutumia dawa inayotumiwa kutibu vidimbwi vya maji ambayo imechanganywa na chloroquine phosphate, na ina viungo vya dawa ya hydroxychloroquine.

Visa vingine vya watu kutumia dawa hiyo kwa kiwango cha juu pia vimeripotiwa nchini Nigeria.

Je, hydroxychloroquine ni nini?

Hydroxychloroquine ni dawa ya kulinda kinga ambayo imetumika kwa miongo kadhaa katika kutibu malaria, hatua inayoifanya kujulikana kama dawa ya kukabiliana na malaria.

Pia inatumika kutibu yabisi.

Huitwa kwa kiungo chake cha chloroquine , licha ya kwamba dawa zote mbili zina kemikali na matumizi ya kimatibabu ambayo hayafanani kabisa.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Hydroxychloroquine hupatiwa wagonjwa kupitia ushauri wa madaktari

Pia hutumiwa kutibu erythematosus na arheumatoid kwa wagonjwa ambao hawajaimarishwa na matibabu mengine.

Matumizi yake ni ya kutumia mdomo na inadhibitiwa na maagizo yaliyotolewa na madaktari.

“Kwa sababu imetumika kwa muda mrefu, usalama wake na wasifu wake unajulikana, tayari imeidhinishwa na FDA na EMA (Shirika la Dawa la Ulaya),” anasema Morse.

Walakini, matumizi ya chloroquine na hydroxychloroquine pia yana athari mbaya kwa wagonjwa wengine.

Hii ni pamoja na maumivu ya kichwa, kuhisi kisunzi , kupoteza hamu ya kula, kuharisha ,kutapika, na kuwa na upele katika ngozi.

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

China ilianzisha utengenezaji wa dawa ya chloroquine baada ya kipindi cha miaka 15

Je, inaweza kutibu Virusi vya corona?

Daktari George Rutherford, na profesa katika chuo kikuu cha California , San Francisco anaelezea BBC kwamba ijapokuwa dawa hiyo ina uwezo wa kutibu magonjwa kama vile Covid 19 ulimwengu unafaa kusubiri kupata matokeo muafaka.

“Unapoifanyia majaribio dhidi ya virusi vya corona huzuia virusi hivyo kutoingia katika seli na kusababisha metaboliki mwilini hatua inayozuia uwezo wa virusi hivyo kuongezeka” , anasema.

Hatahivyo anasema kwamba inapofanya kazi dhidi ya malaria haimaanishi kwamba inaweza kufanya kazi dhidi ya Covid-19 .

Na kwamba hata ijapokuwa inafanya kazi vizuri katika majaribio haimaanishi kwamba itafanikiwa katika mwili wa mwanadamu, anaongezea.

Mtaalamu huyo anasema kwamba dawa hiyo inafaa kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kuelewa jinsi inavyoweza kufanya kazi vyema hatua inayoweza kuchukua kati ya mwezi mmoja hadi mwaka mmoja.

Ripoti kutoka gazeti la The New York Times na Washington Post zinasema kwamba dawa hiyo imefanyiwa majaribio miongoni mwa wagonjwa nchini Marekani huku chombo cha habari cha Xinhua kikiripoti kwamba imetumika katika hospitali kumi mjini Beijing na mikoa mingine miwili.

Swali la kujibiwa ni kwamba ni katika hatua gani ya ugonjwa huo ambapo mtu ambaye tayari ameambukizwa virusi vya corona anaweza kusaidika?

Kwa kuwa athari yake haiwezi kuwa sawa mwanzoni katikati ama katika hatua za mwisho.

Morse hatahivyo anasema kwamba WHO haijaidhinisha matumizi ya hydroxychloroquine na chloroquine kama tiba ya virusi vya corona.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Utafiti unaweza kuchukua muda wa kati ya mwezi mmoja hadi mwaka ikitegemea idadi ya wagonja wanaofanyiwa vipimoSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *