Coronavirus: Mahakama kuu ya Kenya imeagiza kusitishwa kwa ndege zote kutoka China


Shirika la ndege ya China

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mahakama kuu ya Kenya imeagiza kusitishwa kwa ndege zote kutoka China

Mahakama kuu ya Kenya imesitisha kwa muda ndege zote kutoka China kuja kufuatia kesi kuhusu coronavirus iliyowasilishwa na chama cha mawakili wa Kenya.

Akitoa hukumu yake Ijumaa jaji James Makau amemuamrisha waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i na waziri wa zamani wa afya Sicily Kariuki kuwatafuta abiria wote 239 waliowasili nchini kutoka China kupitia uwanja wa ndege wa wa Kimataifa wa Jomo Kenyata mnao Februari 26, na kuwatenga katika hospitali ya kijeshi.

Huku hayo yakijiri Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoaagizo la rais kuhusu kuhusu coronavirus kufuatia malalamiko ya umma kutoka kwa Wakenya kuhusiana na jinsi serkali inavyoshughulikia virusi hatari vya corona ambavyo vinaendelea kutikisa mataifa duniani.

Katika agizo lake bw. Kenyatta anataka kamati ya kitaifa ya kushughulikia hali ya dharura kushughulikia mlipuko wa coronavirus.

Rais pia ameamrisha kukamilishwa kwa kituo cha kitaifa cha kuwatenga na kuwatibu wagonjwa mjini Nairobi katika kipindi cha siku saba.

Magazeti ya Kenya yameangazia ghadhabu ya Wakenya baada ya serikali kuruhusu ndege kutoka China kutua nchini.

Hatua hiyo pia imelalamikiwa sana katika mitandao ya kijamii baada ya kuwasili nchini siku ya Jumanne, ambapo ndege ya shirika la Southern kuruhusiwa nchini ikiwa na abiria 239.

Saa kadhaa kabla ya hatua hiyo, maafisa wa Kenya walikuwa wame tangaza kurejelewa kwa safari za ndege kuenda China, licha ya hofu ya kusambaa kwa virusi vya Covid-19.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *