Coronavirus: Tanzania yathibitisha kuwa wagonjwa 13 wa corona


korona

Tanzania imetangaza idadi mpya ya mambukizi ya Covid19 kuwa jumla ni 13 nchini .

Wagonjwa 11 wakiwa wamepatikana Tnzania bara na huku kisiwani Zanzibar kukiwa na wagonjwa wawili.

Kwa mujibu wa waziri wa afya, bi. Ummy Mwalimu amesema kuwa hakuna maambukizi yaliyopatikana ndani ya nchi mpaka sasa.

Kesi mpya ni ya dereva wa maroli makubwa yanayotokea Burundi kuja Tanzania, na alikutwa na maambukizi hayo akiwa mkoa wa Kagera.

Wagonjwa wote 13 kasoro mmoja wao walisafiri nje ya nchi katika siku 14 zilizopita kabla ya kuthibitika kuwa na virusi hivyo, na mgonjwa ambaye hakusafiri nje ya nchi alikutana na muathirika anayetoka nje ya nchi.

Kwa hivyo, kulingana na ripoti ya Waziri wa Afya, hakuna maambukizi ya ndani ya nchi mpaka sasa.

Ripoti hiyo pia imesema kuwa toka Ugonjwa wa Virusi vya Corona ulipoibuka Tanzania, zaidi ya watu 273 wamepimwa na kati yao ni watu 13 tu waliokutwa na virusi hivyo.

Maambukizi ya mtu mmoja aliyepata akiwa ndani ya nchi, aliyapata kutoka kwa mtu aliyetoka nje ya nchi.

Haki miliki ya picha
IKULU TANZANIA

Image caption

Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli

Wiki iliyopita Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametangaza kuwa nchi hiyo ina wagonjwa 12 walioambukizwa ugonjwa wa corona.

Wanane kati ya wagonjwa hao ni raia wa Tanzania na wengine wanne ni raia wa kigeni.

Akihutubia taifa rais Magufuli alisema: ”Tumetishana sana Tanzania kana kwamba hakuna mogonjwa yanayouwa watu”

”Nimeanza kuwa na wasiwasi kwamba imefika mahali hata watu wanamsahau mungu kwamba Mungu ndiye mponyaji wa kweli katika maisha yetu, ile tuweze kushinda hili balaa lakini pia tunachukua tahadhari.” aliongezea kusema.

Aidha Bw. Magufuli alisema kuwa ana matumaini kuwa janga hilo litapita.

”Tuchape kazi, tuendelee kumuomba mungu. Tusitishane, tusiogopeshana. Natoa wito kwa ndugu zangu wanaoandika mitandaoni kwa sababu kila mmoja amekuwa akiandika lake. Mengine wanapeleka kama mzaha. Huu ugonjwa sio wa kufanyiwa mzaha.”

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Watanzania wanahimizwa kunawa mikono kudhibiti maambukizi ya coronavirus

Shirika la Afya Duniani (WHO) liliutangaza ugonjwa wa Covid-19 kuwa Dharura ya Kimataifa (yaani Global Health Emergency).

Hata hivyo, kutokana na kasi ya kusambaa kwake, tarehe 11 Machi, 2020,WHO iliutangaza ugonjwa huu kuwa Janga la Kimataifa.

Katika juhudi za kudhibiti kuenea kwa maaambukizi Rais Magufuli amesema kuanzia Jumatatu, wageni wote watakaoingia nchini humo kutoka mataifa yaliyo na visa vya ugonjwa huo watatengwa kwa siku 14 kwa gharama zao.

Agizo hilo linawajumuisha Watanzania wanaorejea nyumbani kutoka nchi zingine.

Ugonjwa wa Corona mpaka sasa hivi haujauwa mtu nchini Tanzania.

Hatua zingine zilizochukuliwa kudhibiti maambukizi ni zipi?

  • Shule zote zimefungwa kwa siku 30 ikiwa ni hatua ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya corona nchini humo.
  • Pamoja na kuzuia mikusanyiko yote ya watu wengi yakiwemo matamasha ya muziki, mikutano ya hadhara mbalimbali ikiwemo ya kisiasa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *