Coronavirus: Uganda yawatumia $60m wanafunzi wake waliokwama Wuhan China


Jinsi watu wanavypata chakula Wuhan

Haki miliki ya picha
MEITUAN

Image caption

Jinsi watu wanavypata chakula Wuhan

Serikali ya Uganda imesema kwamba inatuma dola elfu sitini ili kuwasaidia wanafunzi wake waliokwama katka mji wa Wuhan nchini China uliotengwa kufuatia mlipuko wa virusi vya corona.

Mamlaka inasema wasafiri 265 kutoka China – wote raia wa China na wenzao wa Uganda wametakiwa kujitenga kwa wiki mbili .

Licha ya kuongezeka kwa viwango vya wasafiri kutoka Afrika kwenda China hakuna kisa kilichothibitishwa kuhusu ugonjwa huo barani kulingana na mwanahabari wa BBC Catherine Byaruhanga.

Raia wa Uganda wameanzisha kampeni chini ya alama ya reli Evacuate Ugandas in Wuhan {waondosheni raia Waganda mjini Wuhan} kufuatia ushuhuda wa wanafunzi waliozungumza kuhusu kukosa chakula na vifaa kama mask za usoni.

Mamlaka inakadiria kwamba kuna takriban raia 105 wa Uganda mjini humo ambao ndio chanzo cha mlipuko wa virusi vya corona.

Waziri wa afya nchini Uganda aliambia bunge, takriban dola elfu sitini zimetumwa ijapokuwa haijulikani kila mwanafunzi anapata pesa ngapi.

Fedha hizo zitatumwa kwa njia ya kielektroniki kwa simu zao.

Serikali inadai kwamba kuwarudisha nyumbani raia wake kutoka Wuhan kunaweza kusababisha maambukizi hayo kufika Uganda huku ikiongezea kwamba miundo mbinu ya taifa hilo haiwezi kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo.

Kama mataifa mengi vipimo vya virusi hivyo vimewekwa katika uwanja wa ndege . Na abiria wanaowasili kutoka China wametakiwa kusalia nyumbani kwa wiki mbili kama tahadhari.

Hatahivyo kumekuwa na maswali kuhusu mikakati iliowekwa na serikali huku kukiwa na ripoti kwamba watu wanaingia nchini humo bila ya ukaguzi mwafaka wa kiafya kufanywa.

Je nchi za Afrika ziko tayari kukabiliana na janga hili?

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Ukaguzi wa virusi vya corona ukiendelea katika maeneo mbali mbali kote duniani

Afrika ni moja ya mabara mwili ambayo bado hayajathibitisha kisa chochote cha virusi vya corona ingawa wataalamu wameonya kuwa hilo huenda lisiendelee kwa kipindi kirefu kwasababu ya uhusiano wa bara hilo na China.

Karibia watu 565 wameaga dunia huku visa vingine zaidi ya 28,000 vikithibitishwa kote duniani, idadi kubwa ikiwa ni kutoka China.

Wiki iliyopita, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kwamba mlipuko wa virusi vya corona ni ugonjwa wa dharura kwa dunia nzima kwasababu ya hofu kwamba nchi maskini huenda zikashindwa kukabiliana na mlipuko huo.

Ni vifaa gani vilivyopo kwasasa vya kukabiliana na mlipuko wa virusi hivi?

Hadi mapema wiki hii, kulikuwa na maabara mbili pekee zenye uwezo wa kuchunguza virusi hivi barani Afrika – Senegal na Afrika Kusini – zenye vifaa maalumu vinavyohitajika wakati wa kuchunguza virusi hivyo.

Maabara hizo zimekuwa zikitumika na nchi nyingine katika eneo hilo.

Moja ya maabara hizo, Institut Pasteur de Dakar, nchini Senegal kwa kipindi kirefu imekuwa mstari wa mbele katika ubunifu wa tiba Afrika ikiwemo utafiti wa homa ya manjano.

Hata hivyo wiki hii, Ghana, Madagascar, Nigeria na Sierra Leone zimetangaza kwamba pia nazo zina uwezo wa kufanya vipimo vya virusi vya corona.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Maabara ya Institut Pasteur de Dakar nchini Senegal ni moja yenye vifaa stahiki vya kupimia virusi vya coronaSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *