Covid-19: Ibaada za barazani zapata umaarufu Kenya


Nje kidogo ya jiji la Nairobi, mchungaji Paul Machira anahubiri watu kupitia ubaraza wa ghorofa,huku akitumia vipaza sauti vinavyowavutia hasa watoto wanaocheza pamoja na wazazi wao.

Licha ya marufuku za ibada lakini mchungaji Paul Machira na kuni linalosindikiza hawajasitisha mahubiri kwa watu walioko kwenye maghorofa. Akijiita mwenyewe kuwa mhubiri wa watoto,Machira amekuwa akiwahubiria injili watoto kupitia nyimbo.

Alianzisha shughuli zake hizo za « Balcony to Balcony »toka kutangazwa kwa kisa cha kwana cha ugonjwa wa Corona nchini Kenya katikati mwa mwezi Machi. Hivi sasa Machira ambae ni kutoka kwenye kanisa la kianglikani ni maarufu.

Amesema toka kutangazwa kwa ugonjwa huo,kitu cha kwanza kilichositishwa ni mikusanyiko ya kidini.

Amesema hali hiyo ilimpa fursa ya kwenda kuhubiri barabarani,amesema Yesu alikuwa akienda kanisani lakini mara nyingi kazi yakeaikuwa akiifanya nje na barabani. Mchungaji Machira amesema kwamba nchini Kenya watoto wengi hawana fursa yakusikiliza iabada kwa njia ya mtandao.

Afrika Kenia - Gelb gestrichene Kirchen als Symbol des Friedens (picture-alliance/AA/R. Canik)

Kufuatia mripuko wa janga la covid-19, maeneo yote ya ibaada yalifungwa nchini Kenya.

Amesema wazo la kuanzisha ibada hiyo kwenye mabaraza ya ghorofa ilitoka kwa Lilian Mbere,mwalimu wa shule ya jumapili,anayewafunza watoto kupitia nyimbo kila juma tatu kwenye mabara ya maghorofa ilikuwaondolea ukinaifu wa kubaki manyumbani.

Mbere amesema kwaba ameridhishwa na shughuli zake hizo na kamtolea mwito Machira kufanya hivyo pia.

Lilian Mbere amesema mara akichelewa watoto huanza kuuliza ikiwa hakuna mafunzo leo.Mara nyingi watoto hao huimba nyimbo waliofunzwa na Lilian Mbere.

Kenya tayari imerekodi visa zaidi ya 1000 vya wagonjwa wa Corona. Wengi hasa wafanya kazi wanaotegemea kulisha failia zao kila siku, wamekerwa na hatua zilizochukuliwa katika kupunguza ueneaji wa virusi hivyo.

Machira amesema kwamba ibada yake ya « Balcony to Balcony » tayari imetembelea majengo 16 na timu yake inaweka masharti kadhaa kabla ya kutembelea jengo flani. Sharti ya kwanza ni nyumba kuwa na balkoni kwa ajili ya kuheshimu kanuni za usafi.

Chanzo: AP

 Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *