Daniel Sturridge: Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool aungana na mbwa wake aliyepotea


Sturridge and dog

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Daniel Sturridge’s dog Lucci has been safely returned to the former England international

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Daniel Sturridge amesema ana furaha isiyo kifani kwa kumpata mbwa wake aliyepotea aitwaye Lucci.

Sturridge, 29, alisema yupo tayari kutoa kiwango chochote cha pesa ili kumpata mbwa huyo ambaye alipotea baada ya nyumba yake nchini Marekani kuvunjwa na wezi.

Video na picha za mbwa huyo zilichapishwa mitandaoni na baada ya hapo akarejeshwa kwa mmiliki wake halali.

“Siamini,” Sturridge amesema katika video aliyochapisha kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

“Nataka tu kusema asante kwa kila mtu mitandaoni aliyeniunga mkono na kupaza sauti. Ninashukuru sana.”

Sturridge hata hivyo ahakusema kama alitoa pesa kwa mtu aliyemrejesha.

Haki miliki ya picha
Twitter

Awali mchezaji huyo alisema tukio hilo limetokea alipokuwa kwenye matembezi Jumatatu usiku.

“Tutalipa kiasi chochote kile ili kumpata mbwa wetu,” amesema Sturridge.

“Yoyote atakayemrudisha mbwa wangu (atapata) elfu 20, elfu 30 (pauni), kiasi chochote kile.”

Sturridge pia ametuma picha nne za mbwa huyo na pia video zinazoonesha wanaaume watatu waliojifunika uso wakiingia kwenye nyumba hiyo.

Sturridge, kwa saasa anahusishwa na uhamisho kuelekea klabu ya Aston Villa ambayo inarejea EPL msimu ujao utaoanza Agosti.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *