David de Gea: Kipa wa Man United aliyejeruhiwa atiliwa shaka katika mechi dhidi ya Liverpool


David de Gea limps off injured

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

David de Gea aliichezea Sweden baad aya kuachwa kwenye benchi dhidi ya Norway wiki iliopita

Kipa wa man United David de Gea anatiliwa shaka kushiriki katika mechi ya ligi kuu England au Premier League dhidi ya Liverpool Jumapili baada ya kujeruhiwa katika kibarua huko Uhispania.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alionekana kuumiza msuli wake wa paja wakati wa mechi ya kufuzu taifa lake katika mashindano ya Euro 2020 dhidi ya Sweden.

Kepa Arrizabalaga wa Chelsea alilazimika kuichukuanafasi yake baada ya saa moja huku upande wake ukifungwa 1-0.

Bao la lala salama la Rodrigo lilisawazisha na mechi kuishia kwa sare ya 1-1 na kuipa fursa Uhispania kujikatia tiketi kwa mashindnao hayo ya Euro 2020.

Jeraha la De Gea halikutokana na hali ya kuumizwa – alijishikilia nyuma ya mguu ghafla baada ya kupokea pasi ya nyuma kutoka kwa mchezaji mwenzake.

Alikaa chini kwenye lango lake kabla ya kusaidiwa kuondoka uwanjani na wahudumu wa afya.

United ipo katika nafasi ya 12 kwenye Premier League na haijafanikia kupata ushindi katika mchi tatu zilizopita za juu.

Itakabiliana na Liverpool inayopania kupata ushindi wa 18 katika ligi hiyo, jumla itakayo kuwa sawa na rekodi inayoshikiliwa na Manchester City.

De Gea alikosoa mchezo wa timu yake msimu huu baada ya mechi ya mwisho iliyoishia kwa kufungwa 1-0 na Newscastle – akisema: “Msimu mzima haukubaliki kwetu.

“Tuna wachezaji waliojeruhiwa lakini hicho sio kisingizio. Sisi ni Manchester United. Tunahitaji kufanya mazoezi sana ili kuweza kuendelea kupambana na turudi kushinda mechi.”

Iwapo De Gea hatoweza kushiriki mechi Old Trafford mwishoni mwa juma, Argentine Sergio Romero – aliyeshirikishwa katika ligi ya Uropa na kombe la Carabao msimu huu – huenda akawekwa kuichukua nafasi yake.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *