Dawa bandia: Je tatizo la dawa bandia Afrika ni la kiwango gani?


Government officials taking away fake drugs in Abidjan, Ivory Coast Maafisa wa serikali wakibeba dawa bandia mjini Abidjan

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Government officials taking away fake drugs in Abidjan, Ivory Coast Maafisa wa serikali wakibeba dawa bandia mjini Abidjan

Kupenya kwa dawa bandia barani Afrika ni tatizo la kiafya ambalo haliwezi kupuuzwa kulingana na shirika moja la hisani nchini Uingereza.

Wakfu huo wa Brazzaville unaandaa mkutano wa mataifa saba ya Afrika nchini Togo , wiki hii ili kukabiliana na tatizo hilo.

Congo, Niger, Senegal, Togo, Uganda, Ghana na The Gambia zitajadiliana kuhusu mikakati ya kukabiliana na ulanguzi wa dawa bandia.

Lakini je tatizo hili ni kubwa kwa kiwango gani barani Afrika? Na je lina athari gani?

Kuna dawa ngapi bandia?

Duniani, biashara ya dawa bandia ina thamani ya hadi $200bn (£150bn) kila mwaka huku bara la Afrika likiwa mojawapo ya eneo ambalo limeathiriwa pakubwa kulingaa na makadirio ya viwandani.

Shirika la afya duniani WHO linasema kwamba asilimia 42 ya dawa zote bandia zilizoripotiwa kwake kati ya mwaka 2013 na 2017 zilitoka barani Afrika.

Eneo la Ulaya na lile la Marekani kusini na Kaskazini yalikuwa na jumla ya asilimia 21 kila mmoja. Lakini je takwimu hizo zina ukweli gani?

WHO lina mpango wa kuripoti visa vya dawa bandia unaotegemea mamlaka za kitaifa ama hata zile za kieneo duniani ili kupata habari hizo. hivyobasi data ya 2013-17 ni sawa na ile inayotoka katika mataifa ama maeneo yalioathirika.

Fake medicine seizures 2013-17

% reported

WHO limesema kwamba huku maafisa zaidi wakifunzwa na mashirika yanayosimamia kuwa macho , idadi ya visa vya kukamatwa kwa dawa bandia viliongezeka.

Hivyobasi kuna uwezekano mkubwa kwamba maeneo yenye usimamizi mbaya ama uliodhoofu huenda yakaripoti kiwango kidogo cha tatizo hilo.

Bright Simons , ambaye alianzisha mfumo wa kukagua dawa nchini Ghana amesema kwamba sio rahisi kutoa makadirio kwa kuwa biashara hiyo inafanywa kwa siri kubwa mno.

Lakini kumekuwa na visa vya kukamatwa kwa dawa hizo katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni hatua inayotoa ishara kuhusu kiwango cha tatizo hilo Afrika magharibi.

Ivory Coast, Guinea-Bissau, Liberia na Sierra Leone zilikamata tani 19 za dawa bandia mwaka 2018.

  • Walanguzi nchini Ivory Coast walikamatwa wakijaribu kuingiza tani 12 za dawa bandaia kutoka Ghana 2019.
  • Operesheni ilioongozwa na polisi wa kimataifa katika mataifa saba ya magharibi mwa Afrika ilisababisha kukamatwa kwa zaidi ya tani 420 za dawa bandia 2017.
  • Karibia tani 19.88 za dawa bandia zilikamatwa nchini Mali kati ya 2015-18

Kampuni ya hisabati PwC inasema kwamba kiwango cha dawa bandia katika baadhi ya mataifa kinaweza kuwa asilimia 70 juu katika maeneo yanayoendelea kama vile bara Afrik.

WHO inakadiria moja kati ya bidhaa 10 za matibabu katika mataifa yenye mapato ya kadri ikiwemo eneo kubwa la barani Afrika ziko katika kiwango cha chini ama bandia.

Je dawa bandia zina athari gani?

Uchanganuzi wa taasisi ya London kuhusu usafi kutoka shirika la WHO unakadiria kwamba dawa bandia na zile za kiwango cha chini huenda zinasababisha vifo 116,000 zaidi mbali na ugonjwa huo kila mwaka katika jangwa la sahara kwa gharama ya kadri ya $38.5m kwa mwaka.

Na mwaka 2015, utafiti uliochapishwa katika jarida la kijamii Marekani na usafi unakadiria kwamba zaidi ya watoto 122,000 walio chini ya umri wa miaka mitano hufariki kila mwaka kutokana na dawa za kukabiliana na malaria za kiwango cha chini katika eneo la jangwa la sahara barani Afrika.

Ijapokuwa matokeo yake ni makadirio , wanasayansi hao wanasema kwamba dawa za kiwango cha chini zinachangia pakubwa katika vifo vya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.

Kwa nini ni vigumu kukabiliana na dawa bandia?

Dawa bandia mara nyingi haziwezi kutofautishwa na dawa sahihi kutokana na pakiti zake ambazo ni nzuri.

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Dawa zainauzwa katika soko lililopo kandokando ya barabara mjini Lagos

Pia kuna tatitzo la bei za dawa katika mataifa masikini. Iwapo dawa nzuri kutoka kwa muuzaji ni ghali, watu hujaribu dawa ilio rahisi kutoka kwa muuzaji ambaye hana leseni, WHO limesema.

Kupunguza bei ya dawa zinazostahiki hatahivyo hakutatui tatizo hilo.

Hata dawa zilizopunguzwa bei zinaweza kuwa biashara miongoni mwa wahalifu , iwapo mauzo yake yapo juu.

Hatahivyo kuna suluhisho la kiteknolojia linalofanyiwa majaribio , ikiwemo programu za simu ili kuwasaidia watumiaji kutambua dawa.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *