Diane Gashumba: Ni waziri wa tatu kujiuzulu nchini Rwanda


Dkt. Diane Gashumba: Ni waziri wa tatu kujiuzulu nchini Rwanda

Haki miliki ya picha
CYRIL NDEGEYA

Image caption

Dkt. Diane Gashumba: Ni waziri wa tatu kujiuzulu nchini Rwanda

Waziri wa Afya nchini Rwanda Dkt. Diane Gashumba amejiuzulu kulingana na afisi ya waziri mkuu nchini humo.

Katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa Twitter, afisi hiyo imesema kwamba kujiuzulu kwake kunatokana na makosa ya kawaida na mapungufu yake ya uongozi.

Hatahivyo haikutoa maelezo zaidi kuhusu sababu zilizomlazimu kujiuzulu.

Dr Gashumba ambaye kazi yake inashirikisha kuzuia kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola kuingia nchini Rwanda kutoka taifa jirani la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekuwa afisini tangu mwezi Oktoba 2016.

Kujiuzulu kwake kunajiri wiki moja tu baada ya mawaziri wengine wawili kutangaza kujiuzulu.

Evode Uwizeyima, ambaye alikuwa akisimamia maswala ya kisheria alikiri kumpiga mlinzi mmoja.

Isaac Munyakazi alijiuzulu kama waziri anayesimamia elimu ya msingi na ile ya upili.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *