

Chanzo cha picha, Getty Images
Ubadilishaji wa data kwa Emma Coronel ni wa zamani
Kwa mtu ambaye amekuwa akifuatilia kesi ya Joaquín “El Chapo” Guzmán kwa miaka miwili iliyopita, kukamatwa kwa mke wake Jumatatu ni hatua ambayo kwa kiasi fulani ilitarajiwa lakini swali ni je kwanini sasa.
Emma Coronel Aispuro, amekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles huko Virginia, na anakabiliwa na mashitaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya kimataifa, kulingana na Wizara ya sheria Marekani.
Mke wake “El Chapo” aliyekuwa malkia wa urembo pia anashutumiwa kwa kuhusika na njama ya “El Chapo” kutoroka jela nchini Mexico kabla ya kuhamishwa mjini New York Marekani na kuhukumiwa kifungo cha maisha kama kiongozi wa genge la dawa za kulevya kimataifa la Sinaloa.
Wakili wa Marekani Jeffrey Lichtman, aliyemtetea Guzmán wakati wa kesi yake, amethiitisha kwa BBC Mundo kuwa yeye ndiye atakayemwakilisha Coronel, ambaye amepanga kusema kwamba hana hatia katika mashitaka dhidi yake.
Lichtman alijitahidi kuepuka kutoa matamshi mengine wakati wa mazungumzo yake muda mfupi baada ya kutokea kwa taarifa za kukamatwa kwa Coronel.
Lakini taarifa za mwanamke huyo kuhusu uraia wake mara mbili wa Marekani na Mexico sio ngeni.
Isitoshe, serikali ya Marekani imekuwa ikimchunguza kwa karibu miaka miwili na wakati wa kesi ya Guzmán’ mwaka 2019, kulitokea taarifa na ushahidi ambao ulizua maswali, kwanini Coronel ameachwa kuwa huru bila kufunguliwa mashitaka yoyote.
“Ni jambo lisiloweza kuepukika mwanamke huyo kushitakiwa kwa makosa ya kupanga njama. Na inashangaza kwamba alikuwa akiishi Marekani badala ya Mexico, ambako uwezekano wa yeye kukamatwa ulikuwa mdogo,” wakili Rob Heroy, amezungumza na BBC Mundo ambaye aliyemtetea mbabe mwingine wa genge la ulanguzi wa dawa za kulevya raia wa Mexico huko nchini Marekani na pia alikuwa msaidizi wa mkuu wa sheria North Carolina.
Madai dhidi ya Coronel
Coronel anashtakiwa kwa makosa ya kupanga njama ya kugawanya kilogramu moja au zaidi ya dawa za kulevya aina ya heroin, kilogramu tano au zaidi za dawa ya kulevya aina ya cocaine, kilogramu 1,000 au zaidi ya dawa za kulevya za marijuana na gramu 500 au zaidi za dawa aina ya methamphetamine, zilizoingizwa kiharamu nchini Marekani.
Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya Marekani imekuwa ikimchunguza Coronel kwa miaka miwili.
Wakati mume wake amepatikana na hatia kwa madai ya ulanguzi wa mamia na zaidi ya tani za dawa za kulevya, ni madai ambayo yanaweza kumfanya Coronel kujipata ameshitakiwa kifungo cha miaka kadhaa gerezani iwapo atapatikana na hatia.
Kesi iliyowasilishwa dhidi ya Coronel inasisitiza kuwa kati ya mwaka 2012 na 2014 “aliendesha mawasiliano kwa niaba ya Guzmán kuendeleza shughuli za ulanguzi wa dawa za kulevya, huku Guzmán akiwa anatoroka kukamatwa na mamlaka ya Mexico.”
“Guzmán alipokamatwa Februari 2014, Coronel aliendeleza mawasiliana kwa niaba ya ujumbe aliopokea kutoka kwa Guzmán wakati anamtembelea gerezani, ambayo hayakuwa yanafuatiliwa na mamlaka ya Mexico,” nyaraka hiyo iliendelea.
Inasemekana mashahidi wasiotaka kutambuliwa na nyaraka zinazothibitisha hilo kama vile barua ni miongoni mwa vinavyotumika katika madai dhidi yake.
Ingawa itakuwa jukumu la mahakama kutathmini na kuhakiki yote hayo, inaonekana kana kwamba madai hayo ni kama yaliyojitokeza wakati wa kesi ya “El Chapo.”
Mmoja kati ya mashahidi wa kesi hiyo ni Dámaso López, ambaye pia anajulikana kama “El Licenciado” aliyekuwa mwandani wa Guzmán, aliyesisitiza kwamba Coronel alimsaidia “El Chapo” kutoroka jela la El Altiplano nchini Mexico Julai mwaka 2015 kupitia handaki lililochimbwa umbali wa kilomita moja na nusu.
Kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani nchini Marekani kwa kosa la ulanguzi wa dawa za kulevya, López alitoa ushahidi kwamba Coronel alikutana naye kati ya Machi na Aprili 2014, na kuwasilisha ujumbe kutoka kwa “El Chapo” uliomuarifu kwamba sasa yuko tayari kutoroka.
Chanzo cha picha, Getty Images
“El Chapo” Guzmán anatumikia kifungo cha maisha jela kwa kuongoza mtandao wa wahalifu wa mihadarati wa Sinaloa
Aliongeza kwamba kati ya Mei na Juni mwaka huo, alifanya mkutano mwingine na Coronel kujadiliana namna ya kumtorosha tena “El Chapo”, ambapo vijana wake pia walishiriki mkutano huo pamoja na López kuchangia namna ya uchimbaji wa handaki.
Guzmán alifanikiwa kutoroka lakini miezi sita baadaye akakamatwa tena. Kulingana na López, Coronel alimtafuta tena ili apange njama mpya ya kumtorosha tena “El Chapo” gerezani lakini akahamishwa hadi Marekani Januari 2017.
“Majadiliano kati ya ‘El Chapo’ na mke wake”
Wakati kesi ya “El Chapo” inasikilizwa kwa kipindi cha miezi mitatu kulijitokeza ushahidi mwingine dhidi ya Coronel.
Kwa mfano, kulikuwa na mabadilishano ya ujumbe kati ya wanandoa hao wawili kati ya mwaka 2011 na 2012, Guzmán alipoamini kwamba kuna uwezekano polisi wakavamia nyumba yake na kumuuliza Coronel kama pengine ana silaha nyumbani.
“Ulionipa,” nimeificha mke wake alijibu.
Katika ujumbe mwingine walizungumzia mabinti zao mapacha, au pesa ambazo Coronel alikuwa anamuomba “El Chapo” ili akafanyiwe upasuaji wa kubadilisha maumbile.
Chanzo cha picha, Getty Images
Lawyer Jeffrey Lichtman, aliyemtetea “El Chapo” Guzmán, ameithibitishia BBc kwamba atamuwakilisha Emma Corone pia
Baada ya kesi ya mume wake, Coronel alihojiwa na kipindi kimoja cha televisheni kuhusu maisha ya jamaa za walanguzi wa dawa za kulevya na hata kutangaza mipango ya kuanzisha kampuni ya kuuza nguo kwa jina “El Chapo,” lakini ndoto hiyo haikutimia.
Hata hivyo, Wizara ya sheria nchini Marekani haikusema lolote kuhusiana na sababu za kukamatwa kwa Coronel wakati huu baada ya uchunguzi uliofanyika kwa muda mrefu.