Ethiopia: Wanajeshi wameanza kushambulia mji wa Mekelle – TPLFShirika la habari la Reuters limeripoti kwamba kiongozi wa chama kinanachotwala katika jimbo hilo, TPLF, Debretsion GebreMichael, alituma ujumbe wa Twitter ulioeleza kwamba mji wa Mekele ulikuwa unakabiliwa na ahambulizi kubwa kutoka kwa wanajeshi wa serikali kuu.

Shirika la habari la Ufaransa AFP pia linaripoti kwamba wafanyakazi wa misaada walishuhudia mashambulizi makali yaliyoulenga mji huo.

Hata hivyo, msemaji wa afisi ya waziri mkuu, Billene Seyum, amenukuliwa akisema kwamba mashambulizi hayo hayatalenga makazi ya raia wa kawaida, na kuongeza kuwa serikali inalipa suala la usalama wa wananchi umuhimu mkubwa.

Utawala wa Abiy, ulikuwa umewapatia wapiganaji wa TPLF hadi Jumatano wiki hii kujisalimisha.

Haya yalijiri huku umoja wa mataifa ukisema kwamba Sudan inahitaji masaada wa takriban dola za Marekani 150 ili kwa minajiri ya kugharamia wimbi kubwa la wahamiaji wanaoenelea kuvuka mpaka kutoka nchi jirani ya Ethiopia, kufuatia mapigano hayo.

Akizungumza Jumamosi kwenye kambi ya wakimbizi ya Um Raquba, iliyo umbali wa kilomita 80 kutoka kwenye mpaka kati ya nchi hizo mbili, Kamishna mkuu wa shirika la kuwahudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo grande, alitoa wito kwa wafadhili wa kimataifa kusaidia kuchanga kiasi hicho cha pesa haraka iwezekanavyo ili kuokoa Maisha ya maelfu ya watu.

Mapigano kati ya viskosi vya serikali kuu ya Ethiopia na wapiganaji wa chama kinachotawala katika jimbo la Tigray cha TPLF yalianza tarehe 4 mwezi Novemaba na tayari Sudan ni mwenyeji wa Zaidi ya Waethiopia 43,000 waliokimbia vita hivyo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *