FAO yatuma wataalam kuisaidia Kenya kupambana na nzigeMafunzo hayo yanatolewa na waatalamu kutoka Morocco waliopelekwa na Shirika la Chakula Duniani, FAO, kuisadia Kenya iliokumbwa zaidi na nzige wa jangwani wanaotishia kuharibu chakula nchini humo.

Mwakilishi wa FAO nchini Kenya Tobia Takavarasha anasema wameamua kusaidia Kenya kwanza kwa vile ni kitovu cha uvamizi huo wa nzige na ndio eneo kubwa zaidi linaloathirika, mbali na mataifa matano ya Afrika mashariki na pembe ya Afrika yanayoizunguka nchi hiyo.

Anasema ukikabiliana na hali ya Kenya hapo unapunguza athari katika nchi za jirani.

Waziri wa Kilimo na Uvuvi Kenya Kello Harsama anasema nzige wanahatarisha mfumo wa chakula wa nchi nyingi za Afrika.

Harsama anaeleza : “Nzinge zilipoanza kujitokeza mwezi Disemba zilikuwa katika nchi tatu, lakini hivi sasa zimeenea katika nchi 17 na hizo ni robo tatu ya adhi ya nchi za Afrika na hilo ni tishio kubwa katika kuzalisha chakula.

Mwakilishi wa FAO huko Kenya anasema, kile wanachotarajia kutokana na juhudi hizi ni kuwazuia nzige hao wa jangwani kuanza kuzaana kuingia katika kizazi cha pili na cha tatu kwa sababu hivi sasa wanataga mayai kabla ya kuendelea katika awamu ya pili ya safari yao.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *