Genge la wabakaji India lawanyoa vipara mama na mwana waliokataaa kubakwa


The two women had their heads forcibly shaved

Haki miliki ya picha
ANI

Watu wawili wamekamatwa katika jimbo la Bihar nchini India baada ya kundi la wanaume kuwanyoa vipara wanawake waili kama “adhabu” ya kugomea kubakwa.

Kundi hilo la wabakaji, ambalo lilimjumuisha kiongozi mmoja wa kijiji, liliwavamia mama na mtoto wake ndani ya nyumba yao wakiwa na nia ya kuwabaka, polisi wamethibitisha.

Baada ya wanawake hao kugoma kubakwa, waliwashambulia na kuwanyoa nyweke zote kichwani na kuwatembeza kijiji kizima.

Polisi wanasema wanawasaka wanaume wengine watano waliohusika kwenye tukio hilo.

“Tulichapwa hovyo na fimbo. Nina majeraha mwili mzima. Na binti yangu pia ana maheraha,” mama aliyeshambuliwa amelieleza shirika la habari la Ani.

Wanawake hao wamesema nywele zao zilikatwa mbele ya kijiji kisima.

‘Hakuna woga wa sheria’

Geeta Pandey, BBC Delhi

Kujaribu kubaka ni kosa la kijinsia nchini India, lakini shambulizi lilofuata la kuwanyoa nywele kuwachapa na kuwatembeza kijiji kizima linaonesha nguvu ya wanaume kwenye jamii.

Kinachotia hofu zaidi ni kuwa, kundi la wabakaj hao lilikuwa likiongozwa na na afisa wa serikali – mwakilishi aliyeschaguliwa ili kulinda maslahi ya watu wake na si kuwashambulia.

Uthubutu wa watuhumiwa hao unaonesha ni kwa namna gani katika baadhi ya maeneo nchini India wat hawana woga wa sheria.

Awali ya yote, masikini na wale ambao mbao wapo kwenye makundi yaliyotengwa ni ngumu kwao hata kuwashawishi polisi kufungua mashtaka yao.

Malalamiko yao hupelezwa pasi na umakini na endapo yakipelekwa mahakamani hukutana na msururu wa kesi zinazoendeshwa taratibu, na mwishowe watu wenye ushawishi wanaweza kuachiliwa hata kwenye kesi za mauaji.

Hasira ya jamii na ghadhabu ambazo huinekana baada ya tukio kuripotiwa huisha baada ya muda mfupi tu,

Kinachohitajika ni hatua kali tena za uhakika kutoka kwa mamlaka ili kupatiwa haki kwa waathirika na kurudisha utawala wa sheria katika maeneo ya mbali na vijijini nchini humo .

Taarifa zaidi kuhusu India

“Baadhi ya wanaume hao waliingia kwenye nyumba ya wahanga hao na kujaribu kumnajisi msichana,” afisa wa polisi ameviambia vyombo vya habari na kuongeza kuwa, mama yake alimsaidia kupambana na wanaume hao.

Baraza la wanawake la jimbo hilo pia limelaani vikali tukio hilo, na kuahidi kuwa hatua zaidi kuendeea kuchukuliwa.

Lakini hii si mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea kwenye jimbo la Bihar.

Mwezi Aprili, msichana mmoja alishambuliwa kwa tindikali baada ya kugoma kubakwa na kundi la wanaume.

Miezi michache kabla ya tukio hilo, mwanamke mmoja alishambuliwa, akavuliwa nguo zote na kutembezwa akiwa uchi katikati ya soko la kijiji.

Ghadgabu za jamii juu ya matukio ya ubakaji zimekuwa zikipanda nchini humo toka mwaka 2012, baada ya kubakwa na kuuawa kwa mwanafunzi kwenye basi jijini Delhi.

Matukio ya ubakaji yakaangaziwa tena kwa undani mwaka 2018 ambapo kesi kadhaa za mashambulizi ya kingono dhidi ya watoto nchini humo ziliripotiwa.

Hata hivyo, matukio ya kubakwa na kunyanyaswa kijinsia kwa wanawake nchini humu yanaendelea kuripotiwa kila uchao nchi.

However incidents of rape and violence against women continue to be reported from across the country.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *