Hachalu Hundessa: Msanii wa Ethiopia ambaye kifo chake kimesababisha maandamano amezikwa


Priests around the coffin of Hachalu Hundessa

Maelezo ya picha,

Televisheni inayomilikiwa na serikali ilionesha baadhi ya picha za mazishi ya Hachalu Hundessa

Mwanamuziki wa Ethiopia Hachalu Hundessa amezikwa huku maandamano yanayopinga kifo chake yakiendelea kusambaa katika eneo la Oromia ambapo alikuwa nchukuliwa kama shujaa.

Magenge yaliyokuwa na silaha yalikuwa yamesambaa katika mji mkuu wa Addis Ababa, yakilenga makundi pinzani ya kikabila.

Karibia watu 81 wameuawa katika maandamano hayo huko Oromia tangu Hachalu alipopigwa risasi Jumatatu usiku.

Dhamira ya kifo chake bado haijajulikana lakini kijana huyo, 34, alisema kwamba ametishiwa maisha.

Nyimbo za Hachalu zilikuwa zinaangazia haki ya jamii ya Oromo na kutumika sana katika maandamano yaliyochangia kuondoka madarakani kwa waziri mkuu aliyekuwepo wakati huo 2018.

Maelezo ya picha,

Jeshi limepelekwa katika maeneo mbalimbali ya mji

Katika mji wa Addis Ababa, watu wanane waliuawa katika ghasia zilizobadilika na kusababisha milipuko, amesema mwandishi wa BBC Ethiopia, Kalkidan Yibeltal.

Mwanahabari huyo anasema ghasia za kikabila na kidini zimeongezeka baada ya kifo cha mwanamuziki Hachalu Hundessa

Nini kilichotokea mazishini?

“Hachalu hajakufa. Ataendelea kuwa moyoni mwangu na ndani ya mamilioni ya mioyo ya Waoromo milele,” Gazeti la Reuters limemnukuu mke wake aliyesalia mjane Santu Demisew Diro aliyesema hivyo mazishini.

Mazishi yake yamefanyika katika uwanja wa Hachalu mji wa nyumbani wa Ambo, na kupeperushwa moja kwa moja na Shirika la Utangazaji la Oromo.

“Naomba samanu liwekwe katika mji wa Addis ambapo damu yake ilimwangika,” Bi Santu amesema.

Maelezo ya picha,

Hafla ya mazishi iliyofanyika Ambo

Kuna taarifa kwamba waombolezaji walijaribu kuchelewesha mazishi hadi kuachiliwa wa mwanasiasa wa Oromo Jawar Mohammed.

Mwanasiasa huyo alikamatwa na polisi baada ya kutokea kwa maandamano yaliyojaribu kuzuia mwili wa Hachalu usiondolewe katika mji wa Addis Ababa.

Bwana Jawar, amesababisha kutolewa kwa wito wa haki zaidi kwa Waoromo, kabila kubwa zaidi la Ethiopia, ambalo lilitengwa kisiasa siku za nyuma.

Maelezo ya picha,

Jawar Mohammed ni kiongozi wa eneo la Oromo na mkosoaji wa Waziri Mkuu Abiy Ahmed

Alimuunga mkono Waziri Mkuu Abiy Ahmed aliyekuja na mabadiliko ambaye yeye mwenye ni wa kabila la Oromo, alipoingia madarakani Aprili 2018, lakini tangu wakati huo amekuwa mkosoaji wake mkuu.

Watu wengi zaidi wamekamatwa katika mji mkuu ikiwemo mwanahabari na mwanaharakati Eskinder Nega.

Hachalu Hundessa ni nani?

Alifungwa jela miaka mitano.

Maelezo ya picha,

Nyimbo za Hachalu ziliangazia haki za Waoromo

Ni mmoja kati watoto wanane, Hachalu alizaliwa 1986 huko Ambo – mji ulio kilomita 100 magharibi mwa mji wa Addis Ababa.

Hachalu alienda shule Ambo, na kujiunga na kundi la wanafunzi waliokuwa wanaendesha kampeni ya kutaka uhuru.

Akiwa na umri wa 17, 2003, Hachalu alifungwa jela kwa miaka mitano kwasababu ya shughuli zake za kisiasa.

Baba yake ndiye aliyempa matumaini akiwa gereza na kumfahamisha kwamba jela ni sehemu ya kumfanya mtu kuwa imara zaidi.

Hachalu aliendelea kuwa na misimamo ya kisiasa zaidi wakati akiwa gerezani, kwasababu alipata ufahamu zaidi kuhusu historia ya Ethiopia ikiwemo utawala wa nchi hiyo wa kifalme na kiimla.

Wakati akiwa gerezani huko Ambo pia aliongeza ujuzi wake wa muziki.

“Sikujua namna ya kuandika mashairi na mifuatano ya sauti hadi nilipofungwa gerezani. Hapo ndipo nilipojifunza,” alisema hivyo katika mahojiano 2017.

Wakati akiwa gerezani, aliandika nyimbo 9 na kuachilia albamu yake ya kwanza Sanyii Mootii (Mbio za Mfalme) 2009, mwaka mmoja baada ya kuachiliwa huru.

Alikataa kwenda uhamishoni.

Albamu hiyo ilimbadilisha na kuwa nyota wa muziki na pia nembo ya kisiasa mwenye kutoa matarajio kwa Waoromo.

Hatahivyo, alikanusha kuwa mwanasiasa na kusema: “Mimi sio mwanasiasa, Ni msanii. Kuimba kile watu wangu wanachopita hakunifanyi mimi kuwa mwanasiasa.”

Wanamuziki wengine wengi na wanaharakati walitoroka nchi hiyo kwa hofu ya kuuawa chini ya utawala wa Waziri Mkuu Meles Zenawi na mrithi wake Hailemariam Desalegn lakini Hachalu aliendelea kuishi Ethiopia na kuhamasisha vijana kupigania haki zao.

Moja ya nyimbo zake zilikuwa ni kuhusu vile alivyompenda msichana aliyekuwa anajivunia asili yake na kuwa tayari kufa kwa ajili ya hilo.

Map

‘Mwimbaji asiye na uoga’

Maandamano yaliongezeka katika kampeni ya kutaka uhuru wa kisiasa na mwisho wake ukawa ni Waziri Mkuu Abiy kuwa wa kwanza kutoka kabila la Oromo kupata cheo cha waziri mkuu, 2018 na kuahidi kuachilia huru wafungwa wote wa kisiasa na kufanya uchaguzi wa kidemokrasia.

Miezi miwili baada ya Abiy kuingia madarakani, Hachalu alialikwa na serikali kufanya onesho katika tamasha lililofanyika kwa heshima ya Rais wa Eritrea Isaias Afeworki, ambaye alikuwa anatembelea Ethiopia kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa vita vya mpaka kati ya nchi hizo jirani.

Hachalu alithibitisha kuwa yeye yuko huru na asiye na uoga, akiimba kuhusu umuhimu wa kupatikana kwa haki kwa watu waliouawa katika mapigano ya kikabila mashariki mwa Ethiopia kati ya makabila ya Oromo na Somali na kuhoji vile matamasha yanaweza kufanyika wakati familia zinaomboleza.

Baadae maafisa wa serikali walikosoa uimbaji wake na kusema kuwa halikuwa jambo sahihi kuimba nyimbo za matukio lakini hilo lilimuongezea umaarufu.

Ingawa aliimba kwa lugha ya Afaan Oromoo peke yake, nyimbo zake – hasa zile zilizokuwa zinatoa wito wa uhuru wa kisiasa zilimfanya kuwa na mashabiki wengi kutoka kila pembe ya kabila.

Hachalu aliishi mji wa Addis Ababa, ambapo alipigwa risasi hadi kufa Jumatatu jioni.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *