Hong Kong : Kukamatwa kwa waandamanaji 44 kwazua ghasiaHii ni mara ya kwanza mshtaka kama hayo kufunguliwa tangu maandamano yalipoanza mwezi Juni.

Polisi wametumia gesi ya kutoa machozi kuzuia vurugu na kuwatawanya waandamanaji waliojitokeza nje ya kituo cha polisi katika wilaya ya Kwai Chung.

Waandamanaji walijibu kwa kuwarushia polisi chupa za plastiki na miavuli.

Mapema Jumanne, waandamanaji walisababisha huduma za usafiri wa treni ya chini ya ardhi na kuwazuia wasafiri kutoka kwenye treni.

Usafiri wa treni ulicheleweshwa na hata kusitishwa kabisa katika baadhi ya vituo.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *