Idadi ya vifo vitokanavyo na corona yapanda Ujerumani


Taasisi ya udhibiti wa magonjwa ya Robert Koch imeripoti vifo1,244 zaidi na kufanya idadi jumla kufikia elfu 43,881.

Kansela Angela Merkel na viongozi wa serikli yake wameonya kuwa hatua za kukabiliana na maambukizi zinaweza kuendelea hata baada ya mwezi januari.

Merkel anatarajiwa kukutana na mawaziri wakuu wa majimbo yote 16 ya Ujerumani, baadae mwezi huu kwa ajili ya kujadili hatua zaidi. Kwingineko, Lebanon imeanza utekelezaji wa marufuku ya nchi nzima ya siku 11, kwa lengo la kupambana na kuenea kwa kirusi cha corona.

China nayo imeripoti kifo cha kwanza kilichotokana na COVID-19 katika kipindi cha miezi nane wakati taifa hilo likipambana kuzuia ongezeko la maambukizi.

 Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *