Idara ya uhamiaji yasema inamhoji Kabendera kuhusu uraia wake


Gerald Kihinga

Image caption

Kamishna wa udhibiti wa pasipoti wa idara ya uhamiaji Gerald Kihinga

Idara ya uhamiaji imethibitisha kuwa inamshikilia mwandishi wa habari Erick Kabendera kutokana na kuwa na mashaka na uraia wake, kamishna wa uraia na mdhibiti wa pasi Gerald Kihinga amethibitisha.

Idara ya uhamiaji imesema kama chombo kilichopewa dhamana ya kusimamia na kutekeleza sheria ya uraia ya Tanzania, inayo mamlaka ya kuchunguza na kuthibitisha uraia wa mtu yeyote anayetiliwa mashaka baada ya kupokea taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali.

Idara ya uhamiaji ilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuhusu utata wa uraia wa Bwana Erick Kabendera.

”Baada ya idara kupata taarifa hizo ilianzakuzifanyia kazi.Hata hivyo, Bwana Kabendera mwenyewe hajawahi kuhojiwa kuhusu uraia wake, kwa kuwa hakufika ofisini pamoja na kutumiwa wito mara kadhaa wa kumtaka kufika ofisini kwa mahojiano” Ilieleza taarifa ya Idara ya uhamiaji.

‘Kwa nini tulimkamata Kabendera’

Mwandishi wa habari Tanzania ”akamatwa”

Hii ndio sababu iliyofanya idara ya uhamiaji kwa kushirikiana na jeshi la polisi kumtafuta na kumkamata mhusika ili ahojiwe kwa ajili ya kukamilisha uchunguzi kuhusu uraia wake.

Mamlaka zimesema uchunguzi utakapokamilika, matokeo ya uchunguzi huo yatatolewa.

Hapo awali, Jeshi la Polisi lilidai kumshikilia Mwandishi huyo na halikutaja ni kituo gani ambacho alikuwa anashikiliwa.

Polisi walisema nini?

Awali jeshi la polisi nchini Tanzania lilisema kuwa mwanahabari Erick Kabendera aliyedaiwa kutoweka hakutekwa bali alikamatwa.

Erick Kabendera anayeandikia magazeti ya ndani na nje ya Tanzania alidaiwa kukamatwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi.

Katika mkutano na vyombo vya habari kamanda wa polisi kanda maalum ya mji wa Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa mshukiwa huyo alikaidi agizo la polisi la kufika mbele yao kwa ajili ya mahojiano

”Mwandishi huyu aliitwa hakutekwa lakini kwa ujeuri alikaidi wito huo,kimsingi pengine iwapo angewasili angehojiwa na kuachiliwa”, alisema Mambosasa.

Haki miliki ya picha
@MARIASTSEHAI/TWITTER

Uchunguzi wa uraia wake

Uchunguzi wa utata wa uraia umekuwa ukifanyika kwa watu mbalimbali wakiwemo watu mashuhuri katika jamii. Hivyo suala hili limeibua hisia huenda kwa kuwa muhusika ni mwanahabari.

Aidha baada ya kuulizwa kuwa kwanini wanamkamata kwa mara nyingine kwa suala hilo hilo la uraia ikizingatiwa kuwa si mara ya kwanza kuwahi kuhojiwa kuhusu suala hilo, Kamishna Kihinga alikataa kuwa hawajawahi kumkamata kuhusu taarifa hizo,

“Hatujawahi kabisa kumkamata na kama kweli Basi mtusadie hizo taarifa ili zitusaidie kumuachia”.

Mke wa mwandishi Erick Kabendera ameruhusiwa kumuona mume wake Erick Kabendera ikiwa zimepita takriban siku mbili sasa tangu alipokamatwa na jeshi la Polisi siku ya Jumatatu jioni nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es Salaaam.

Polisi wamemsindikiza Kabendera nyumbani kwake kwa ajili ya kupata nyaraka za uthibitisho wa uraia wake.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *