Idara ya usalama ya Rwanda imethibitisha kuwa inamshikilia mwanamuziki nyota nchini Rwanda, Kizito Mihigo


Kizito

Haki miliki ya picha
Kizito Twitter

Image caption

Mwanamuziki maarufu kwa nyimbo za injili nchini Rwanda Kizito Mihigo

Idara ya upelelezi ya Rwanda imesema inamshikilia mwanamuziki Kizito Mihigo baada ya kufikishwa kwenye idara hiyo na polisi tarehe 12 mwezi Februari .

Kwenye ukurasa wa Twitter idara hiyo ya uchunguzi imesema Kizito anashutumiwa kujaribu kuvuka mpaka kwenda Burundi kinyume cha sheria kwa lengo la kujiunga na makundi ya wanamgambo wanaoipinga serikali ya Rwanda.Pia anashutumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Mamlaka ya uchunguzi imesema uchunguzi bado unaendelea kuhusu tuhuma zinazomkabili ili kufungua kesi dhidi yake.

Awali mwanamuziki huyo alidaiwa kutoweka hapo jana tangu alipozuiwa na wananchi Kusini Magharibi akidaiwa kujaribu kuvuka mpaka kuingia Burundi.

Mwanaume mmoja katika eneo la Nyaruguru ambaye alimuona mwanamuziki huyo jana, aliiambia BBC idhaa ya maziwa makuu kuwa alionekana kama mtu aliyetoka kwenye safari ndefu akiwa na begi zito na akiambatana na wanaume wawili.

Picha za mwanamuziki huyo nyota zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii jioni.

Image caption

Kizito Mihigo

”Nilikuwa hapo nilimuona, wanakijiji waliomzuia walisema alikuwa akijaribu kuvuka mpaka kwenda Burundi kwa kutumia njia za panya, kutoka hapa mpaka mpakani ni mwendo wa chini ya dakika tano”. Alisema.

Bwana Kizito na wanaume wawili walikabidhiwa kwa wanajeshi na polisi walioitwa na wanakijiji.

Polisi nchini Rwanda awali waliiambia BBC kuwa hawana taarifa bado kuhusu kukamatwa kwa mwanamuziki huyo.

Mwaka 2015, Bwana Kizito alikutwa na hatia kwa kosa la jaribio la kutaka kumuua Rais Paul Kagame na kuhamasisha vurugu dhidi ya serikali: alihukumiwa kifungo cha miaka 10 gerezani.

Haki miliki ya picha
RIB Twitter

Image caption

Idara ya uchunguzi Rwanda imethibitisha kumshikilia Kizito

Mwezi Septemba mwaka 2018 aliachiwa huru kwa msamaha wa rais kwa sharti la kuwa atatoka nje ya Rwanda kwa ruhusa ya mahakama ya nchi hiyo.

Hatahivyo, alizuiwa ndani ya nchi, marafiki zake walithibitisha kuwa haonekani popote hii leo.

Raia wa Rwanda walikuwa wanasubiri mamlaka ithibitishe kukamatwa kwake na mashtaka yanayomkabili, au kuonekana bila kuwa na mashtaka.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *