Iran dhidi ya Marekani: Sababu tano kwa kwa nini mzozo kati ya Marekani na Iran hautaisha leo?


Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Maandamano dhidi ya Marekani yalizuka nchini Iran kufuatia mauaji ya Qasema Soleimani

Ni bahati nzuri kwamba mzozo uliosababishwa na kifo cha kamanda wa Iran Qasem Soleimani tarehe mwezi Januari hakuzua vita vikubwa .

Na kutoka na hilo hali ya wasiwasi iliokuwepo imepungua. Lakini sababu zote zilizozifanya nchi hizi mbili kuingia katika vita hazijabadilika.

Hizi hapa sababu zinazofanya mgogoro huo usiishe.

1.Kupungua kwa hali ya wasiwasi ni hatua ya muda tu

Kile ambacho baadhi ya wachanganuzi wanaona kuwa kupungua kwa hali ya wasiwasi kati ya Iran na Maarekani sio cha kweli. Viongozi wa Iran baada ya kushtushwa na mauaji ya Soleimani walfanya kile walichoweza kulipiza kisasi.

Iran ilitaka kujibu kwa kulenga maeneo ya Marekani na kuweka wazi ni nani aliyehusika. Hivyobasi ilitumia makombora yaliorushwa kutoka katika ardhi yake.

Lakini kulikuwa na masharti ya kisiasa katika vitendo vyake . Ilitaka kuchukua hatua ya haraka ili kuipata Marekani katika hali ambayo itakuwa haijajipanga.

Imedaiwa kwamba hatua ya Iran ya kukubali kwamba ilihusika na udunguzi wa ndege ya abiria ya Iran ni mojawapo ya hatua za kujaribu kupunguza hali hiyo ya wasiwasi , lakini sio sawa.

Iran ilikuwa imepanga kukana kuhusika na udunguzi wa ndege hiyo. Lakini wakati Marekani iliposema kwamba ujasusi wao ulikuwa na matokeo tofauti , wakati wachunguzi wa Ukraine walipopata ushahidi wa shambulio , wachunguzi huru walionyesha kasi ya shambulio hilo la ndege .,hatua hiyo iliishinikiza Iran kukubali na kubadili mipango yake.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Shambulio la mdege ya abiria ya Ukraine iliokuwa katika anga ya Iran

Ukweli ni kwamba mara tu tingatinga lilipoanza kuondoa mabaki ya ndege hiyo katika eneo la mkasa , ilikuwa wazi kwamba Iran ilijuwa kile kilichofanyika .

Iwapo kungekuwa na wasiwasi wowote kwamba huenda ilikuwa ajali , mamlaka ya Iran ingekuwa na sababu ya kutoondoa mabaki hayo..

2. Muendelezo wa sera ya Marekani

Kwa nini Marekani ilimuua Soleimani na kujaribu kumshambulia afisa mwengine wa ngazi za juu wa Iran nchini Yemen?

Washington inasema kwamba , pengine kwa sababu za kisheria, ilikuwa ikifanya hivyo ili kuzuia shambulio baya dhidi ya maslahi ya Marekani katika eneo hilo.

Hoja hiyo hatahivyo haijawashawishi wachanganuzi wengi na wakosoaji wa rais Trump mjini Washington.

Ni wazi kwamba mashambulio hayo yametekelezwa kama jaribio la kuzuia mashambulizi ya Iran.

Kwa muda mfupi hatua hiyo inaweza kufanya kazi . Iran italazimika kupima mashambulizi yake vizuri katika siku za baadaye.

Lakini wakati huohuo ambao rais Trump anatishia kuchukua hatu kali dhidi ya Iran , pia anatoa ishara kwamba ataondoka katika eneo zima la mashariki ya kati .

Analiona tatizo lililopo katika eneo hilo kama tatizo la mwengine na sio lake. Hatua hiyo itaathiri uwezo wake wa kutoa vitisho vyovyote.

Marekani itaendelea kuathiri uchumi wa Iran . Lakini haijaweza kuileta Iran katika meza ya mazungumzo. Badala yake imeipatia uwezo Iran wa kulipiza kisasi na hivyobasi kuiifanya Marekani kukabiliwa na shinikizo kali.

Marekani inataka kuidhibiti Marekani na kuilazimu kupunguza maradufu makundi ya wapiganaii inaowamiliki katika maeneo tofauti katika eneo hilo.

Ukweli ni kwamba haiwezi kufanya yote mawili.

3) Malengo ya kimkakati ya Iran hayajabadilika

Uchumi wa Iran huenda unaanguka polepole na raia wake wengi huenda hawafurahii hali hiyo ,lakini huu ni ‘utawala wa mapinduzi’.

Sio utawala utakaoachilia madaraka kwa urahisi . Kundi la kijeshi kama lile la Iran’s Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC) lina uwzo mkubwa.

Lengo lao limekuwa kukabiliana wapinzani nyumbani na kuizuia Marekani . Na hilo liataendelea.

Lengo la Iran ni kuifurusha Marekani nje ya eneo la mashariki ya kati ama hata Iraq na hilo huenda linakaribia kuafikiwa zaidi ya wakati ambapo Soleimani alikuwa hai.

Kulingana na utawala wa Iran, sera ya Tehran imefanikiwa kwa kiwango kikubwa. Imeokoa serikali ya rais Bashar al-Asad nchini Syria na kuisaidia kufungua makabiliano mapya dhidi ya Israel.

Iran ina ushawishi mkubwa nchini Iraq.

Kutokana na utata uliogubika sera ya rais Trump, washirika wa Marekani katika eneo hilo hawahisi kwamba wanapata ulinzi wowote na kwamba wako kivyao.

Raia wa Saudi wamekuwa wakifanya mazungumzo ya chini kwa chini na Tehran, Uturuki inaendelea kujihami kivyake na kutafuta mwandani mpya kupitia Urusi .

Ni Israel pekee kufikia sasa ambayo inadhania kwamba muaji ya Soleimani ni hatua mpya ya Marekani kuonyesha jinsi inavyoendeleza kujikita katika eneo la mashariki ya kati.

Huenda wakashangaa.

Upinzani wa ndani ya nchi pamoja na kuanguka kwa uchumi wake kunaweza kuishinikiza Iran kuiwekea shinikizo Marekani mara kwa mara. Tayari imepata mapigo mawili na huenda ikajipanga kulipiza kisasi.

4) Kuna utata kuhusu nafasi ya Iran

Ishara ya majeshi ya Marekani kuondoka katika eneo la mashariki ya kati inaendelea kuimarika zaidi ya ilivyokuwa awali.

Serikali ya Iraq ipo katika mzozo baada ya kukumbwa na maandamano ya kuipinga. Wengi hawana raha na uwepo wa majeshi ya Marekani mbali na ushawishi wa Iran katika taifa hilo.

Kura iliopitishwa na bunge la taifa hilo imelitaka jeshi la Marekani kuondoka. Hii haimainishi kwamba wanajeshi wa taifa hilo wataondoka kesho , lakini itahitaji mazungumzo na majadiliano ya hali ya juu kwa vikosi hivyo kuendelea kuwepo katika taifa hilo.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Marekani imeimarisha idadi ya wanajeshi wake katika eneo la mashariki ya kati

5) Mkataba wa kinyuklia wa Iran upo mashakani

Kiini cha mgogoro uliopo kuhusu makubaliano hayo ulianza mwezi Mei 2018 wakati serikali ya Marekani ilipojiondoa katika makubaliano hayo.

Tangu wakati huo , Marekani imekuwa ikiweka shinikizo dhidi ya uchumi wa Iran huku Iran nayo ikiweka shinikizo za kieneo kwa kupuuzilia mbali masharti ya makubaliano hayo.

Iwapo makubaliano hayo hayakufa, basi sababu ya pekee ni kwamba hakuna mtu mwengine isipokuwa Trump anayetaka kuyaangamiza.

Iwapo hakuna litakalofanyika basi huenda ni mwisho wa makubaliano hayo. Badala yake rais Trump ametishia kuzuia hazina ya fedha za serikali ya Iran katika benki za Marekani iwapo taifa hilo litalazimu wanajeshi wa Marekani kuondoka Iraq.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *