Iran ilinitesa na kunilazimisha kukiri kuwa jasusi wa Israel


Mazyar Ebrahimi anasema aliteswa kwa siku 40 mfulurizo usiku na mchana

Image caption

Mazyar Ebrahimi anasema aliteswa kwa siku 40 mfulurizo usiku na mchana

Aliyekuwa mfanyabiashara mweney mafanikio wa Iran wakati mmoja anasema ana bahati kuwa hai baada ya kuteswa na mamlaka za Iran baada ya kulazimishwa kukiri kuwa jasusi wa Israel na kuhusika na mauaji ya wanasayansi wa nyuklia – uhalifu unaoadhibiwa kwa kunyongwa.

Hadithi ya Mazyar Ebrahimi, ambaye kwa sasa anaishi nje ya ng’ambo , pia inatoa mwangaza zaidi juu ya uhasama mkubwa baina ya mashirika ya ujasusi ya Iran, kama anavyoelezea mwandishi wa BBC idhaa ya Persia Jiyar Gol

Alikutana na Mazyar Ebrahimi mjini Frankfur Julai, miezi kadhaa baada ya kumpigia simu bila kutarajia kutoka Ujerumani . Gol alishanga sana , kwani alifikiri kuwa alikuwa ameuawa muda mrefu.

Hii ni kwasababu mwaka 2012, yeye na watu wengine 12 walionekana kwenye televisheni ya taifa wakikiri kufanya makosa kadhaa ambayo adhabu yake ilikuwa ni kifo.

Wakiangalia kwenye kamera Televisheni, walisema kuwa walikuwa wakipokea mafunzo nchini Israel kabla ya kurejea nchini Iran na kuwauwa wanasayansi wa nyuklia.

Maandishi waliyokuwa wakiyasoma yalikuwa yameandikwa na Wizara ya Ujasusi – moja ya mashirika mawili ya ujasusi ya Iran – ambalo lilidai kuwa lilivunja mtandao wa ujasusi wa Israeli.

Katika chumba chake cha hoteli , tulitazama video ambapo alidaiwa kukiri.

Akionekana mwenye kutetemeka bado hata baada ya miaka yote hii , Mazyar Ebrahimi anasema alikubali ”kukiri” baada ya kufanyiwa msururu wa mateso kwa karibu siku 40 mchana na usiku

” Waliomuhoji walikuwa wanapiga nyayo za miguu yangu na waya wa umeme ,” alikumbuka Mazyar Ebrahimi mwenye umri wa miaka 46.

“Walivunja mguu wangu. Kipigo kiliendelea kwa miezi saba .”

Kabla ya kukamatwa na wizara ya ujasusi, Bwana Ebrahimi alikuwa anaendesha kampuni ya kutengeneza studio za Televisheni. Alikuwa akisafiri mara kwa mara nje ya nchi kufanya kazi hiyo.

Anaamini mmoja wa washindan wake alimshutumu kufanyia ujasusi mataifa ya nje kimakosa.

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Kikosi cha Iran cha Revolutionary Guard Corps (IRGC) kilianzishwa mwaka 1979 I kulinda mfumo wa kiislam wa Iran

Mwaka 2010 hasi 2012, wanasayansi wanne wa nyuklia wa Iran waliuawa, na huduma za ujasusi za Iran zilikuwa chini ya shinikizo kubwa kuwapata wahusika wa mauaji hayo.

Bwana Ebrahimi walikuwa mmoja wa watu zaidi ya 100 walishutumiwa kuwa majasusi.

Anaseama alikuwa tayari kukubali lawama yoyote ile na alitaka kufa – ili kuepukana na mateso makalina kudhalilishwa.

Lakini licha ya “kukiri kwake”, Bwana Ebrahimi anasema,waliomuhoji walitaka zaidi.

Mwaka 2011, milipuko mikubwa iliharibu kiwanda cha makombora kinachoendeshwa na kikosi cha Iran cha Revolutionary Guard Corps (IRGC). Wataalamu kadhaa wa makombora waliuawa.

Bwana Ebrahimi anasema shirika la ujasusi lilimtaka akiri kuwa alihusika na milipuko hiyo.

“aliyenihoji alisema: ‘wenzetu kutoka kikosi cha IRGC watakuuliza maswali kadhaa. Uzungumzie tu kuhusu mlipuko , useme kile tu ulichoambiwa ,'” Anasema Bwana Ebrahimi.

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Vkosi vya Israel na Iran vimekuwa vikipelelezana

Wakati huo kulikuwa na ushindani mkubwa baina ya IRGC na wizara ya ulinzi katika kukabilia na ugaidi.

Na nilikuwa ninahojiwa na afisa wa ujasusi wa IRGC juu ya miezi saba baada ya kukamatwa kwa mara ya kwanza na hilo lilimnusuru, anasema Ebrahimi.

Afisa huyo alikasirika baada ya kugundua kuwa kulikuwa na utofauti wa wazi katika ushahidi alioutoa Bwana Ebrahimi uliobuniwa na wizara ya ujasusi.

Ghafla, kipigo kikasitishwa , na wizara ya ujasusi hata ikaomba msamaha kwa Bwana Ebrahimi na watu wengine waliokuwa wanakabiliwa na mashtaka sawa na yake.

Lakini Bwana Ebrahimi na wafungwa wengine walisaila gerezani kwa siku nyingine 26 , na wakaachiliwa huru 2015.

Mashirika ya huduma za ujasusi za Iran yamekuwa yakibuni kesi na kuwalazimisha watu wasio na hatia kukiri kutekeleza uhalifu , anasema mtaalamu wa masuala ya usalama Muiran Mehdi Mahdavi Azad anayeishi Bonn.

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Kikosi cha Iran cha Revolutionary Guard Corps (IRGC)

Anasema miaka michache iliyopita huduma za ujasusi za kikosi cha IRGC ziliwashutumu wapatanishi wa masuala ya nyuklia na wanamazingira kufanya ujasusi, lakini wizara ya ujasusi baadae ikathibitisha kuwa kesi zao zilikuwa zimebuniwa.

Baada ya kuachiliwa huru, Bwana Ebrahimi aliwasilisha malalamiko yake dhidi ya wizara ya ujasusi , Televisheni ya taifa ya Iranna magazeti kadhaa yaliyomshutumu kimakosa kuwa yeye ni jasusi wa Israeli.

Hata hivyo, aliacha malalamiko yake baada ya jaji aliyekuwa akichunguza malalamiko yake kummshauri akubali fidia . Alisema kuwa jaji alimwambia kuwa : ” Mtu fulani anaweza kukuchoma kisu mgongoni gizani usiku mtaani. Wewe ni kijana ,usijihatarishe.”

Mbunge maarufu mwanamageuzi wa mjini Tehran, Mahmoud Sadeqi, alituma ujumbe wa twitter alitoa wito kwa wale waliohusika na kuwalazimisha watu kukiri kimakosa kutoa maelezo.

Bwana Ebrahimi alihamia Ujerumani miezi sita iliyopita, na kuomba uhamiaji huko.

Lakini hata sasa, huwa anawasiwasi mkubwa, na uti wake wa mgongo umeharibiwa.

Miongoni mw wale “waliokiri” kufanyia ujasusi Israel, ni mmoja tu aliyehukumiwa ki kunyongwa , Anasema Ebrahimi.

Haki miliki ya picha
RAN STATE TV

Image caption

Televisheni ya Iran ilionyesha paspoti ya Israeli yenye picha ya Bwana Fashi

…………………………..

Majid Jamali Fashi alinyongwa miezi miwili kabla ya kukamatwa kwa Bwana Ebrahimi.

Televisheni ya taifa ya Iranian ilionyesha kile ilichosema ni Paspoti ya Fashi ya Israeli . Ilionekana kama picha iliyotengenezwa ya paspoti ya Israeli iliyochukuliwa kutoka kwenye mtandao wa Wikipedia.

Inaaminiwa kuwa Bwana Fashi alikamatwa baada ya mtandao wa Wikileaks kuchapishwa na mtandao wa kibalozi wa Marekani mwaka 2009.

Mtandao cable ulionekana kuhusiana na mkutano katika ubalozi wa Marekani mjini Baku, Azerbaijan, ambako Bwana Fashi alizungumzia juu ya mateso nchini Iran.

Wikileaks bado haijajibu ombi la mahojiano kuhusu suala hilo.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *