Isabel dos Santos aikimbia Angola


Angola

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Isabel dos Santosh

Hati zilizovuja zinaonyesha jinsi mwanamke tajiri barani Afrika alivyopata utajiri wake kupitia unyonyaji kwa nchi yake, na ufisadi.Isabel dos Santos alipata mikataba ya faida kubwa inayojumuisha ardhi, mafuta, almasi na simu wakati baba yake alipokuwa rais wa Angola, nchi iliyoko kusini mwa Afrika yenye utajiri wa maliasili.

Hati hizo zinaonyesha jinsi yeye na mumewe walivyoruhusiwa kununua mali za serikali katika safu ya mikataba mibaya

Bi Dos Santos anasema madai dhidi yake ni ya uwongo na kwamba kuna uwindaji wa kisiasa unaofanywa na serikali ya Angola dhidi yake.

Binti huyo ambaye ni wa rais wa zamani nchini humo ameifanya Uingereza kuwa nyumbani kwake na anamiliki mali ghali katikati mwa London.

Tayari yuko chini ya uchunguzi wa jinai nchini Angola kwa ufisadi na mali zake zimezuiliwa. BBC Panorama imepewa idhini juu ya ufikiaji wa hati zaidi ya 700,000 zilizovuja juu ya ufalme wa biashara wa bilionea huyo mwanamke barani Afrika.

Mpaka kufikia sasa, Isabel amesha chunguzwa na mashirika ya habari 37 ikiwa ni pamoja na gazeti la The Guardian na gazeti la Exresso la Ureno.

Haki miliki ya picha
Empics

Image caption

uchunguzi uliofanywa wabaini mchezo ulivyouwa

Andrew Feinstein, mkuu wa Kituo cha Ufisadi, anasema nyaraka zinaonyesha jinsi Bi Dos Santos alivyoinyanyasa nchi yake kwa kuwadhulumu watu wa kawaida wa Angola.

“Kila wakati amekuwa akionekana kwenye jarida moja la glossy na mahali pengine ulimwenguni, kila wakati anapofanya sherehe za kukata na shoka huko kusini mwa Ufaransa, anapofanya hivyo ni sawa na kukanyaga matarajio ya raia wa Angola.”

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Isabel dos Santos na mumewe Sindika Dokolo mara nyingi huonekana kwenye sherehe za filamu na sherehe za nyota wa tasnia hizo ulimwengu

Hati zilizovuja zinaonyesha kuwa wakati anaondoka Sonangol, Bi Dos Santos aliidhinisha $ 58m ya malipo tata kwa kampuni ya ushauri huko Dubai inayoitwa Matter Business Solutions.

Image caption

hizi ni baadhi ya ankara za malipo Isabel dos Santos alizotia saini wiki iliyopita akiwa na kampuni ya Sonangol

Anasema hana nia ya kifedha kwa kwa jambo lolote , lakini nyaraka zilizovuja zinaonyesha zilisimamiwa na meneja wake wa biashara inayomilikiwa na rafiki.

BBC Panorama inaarifu kuwa Panorama bi Isabel alituma ankara za madai zaidi ya 50 kwa Sonangol huko London siku ambayo alifukuzwa.

Bi Dos Santos anaonekana kupitisha malipo kwa kampuni ya rafiki yake baada ya kufutwa kazi.Ingawa kazi fulani ya ushauri ilifanywa na kampuni ya Matter, kuna maelezo kidogo sana juu ya ankara za kuhalalisha bili kubwa kama hizo.

Moja inadai paundi 472,196 kwa gharama zisizojulikana, nyingine dola za kimarekani 928,517 kwa huduma za kisheria ambazo hazijajulikana.

Mchezo ulikuwa ukichezeshwa kwa namna hii, Ankara mbili tofauti na – kila moja inadai paundi 676,339.97 – kwa kazi ileile , kwa tarehe hiyo hiyo na Bi Dos Santos akawa akisaini zote.

Isabel dos Santosni nani?

Haki miliki ya picha
Huw Evans picture agency

Image caption

Isabel dos Santos

– Binti mkubwa wa Rais wa zamani wa Angola Jose Eduardo dos Santos

-Aliolewa na msanii kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambaye pia ni mfanyabiashara Sindika Dokolo

-Kwa kiasi kikubwa amesoma nchini Uingereza mahali ambako anaishi mpaka sasa

-Inaarifiwa kuwa Isabel dos Santos ndiye mwanamke tajiri zaidi barani Afrika na kukisiwa kuwa na utajiri wa dola za kimarekani bilioni mbili

-Isabel anatajwa kumiliki kampuni za mafuta na simu za rununu na benki, haswa nchini Angola na Ureno.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *