Italia kufufua kumbukumbu za Brazil mtanage na Italia wanaume


Hali hiyo itajitokeza  wakati  itakapokumbana  na  Brazil katika mpambano  ambao unarejesha kumbukumbu  za  zamani  za kombe la  dunia kwa  wanaume. Nigeria ilifungwa  bao 1-0 na  Ufaransa,  lakini ikiwa  katika nafasi  ya  tatu  katika  kundi  lao  A  inasubiri  kuona iwapo inaweza kupenya  katika timu 16 zinazosalia  ili  kuingia  katika  awamu  ya mtoano. 

Fussball FIFA Frauen WM Australien - Italien (picture-alliance/AP Photo/F. Seco)

Wachezaji wa Italia wakishangiria bao dhidi ya Australia

Italia  ina  pointi sita baada  ya  kufunga  mabao  saba  katika michezo  yake  miwili  ya  ufunguzi , ikiwa  ni  pamoja  na  ushindi  wa kushitua dhidi  ya  timu  iliyopigiwa  upatu  kufanya  vizuri  kabla  ya mashindano  hayo Australiam, na  inahitaji  sare tu  dhidi  ya  Brazil kujihakikishia  kuwa  vinara  wa  kundi C.

Pambano  hiyo linazusha  kumbukumbu  ya  fainali  za  wanaume katika  kombe  la  dunia, ikiwa  ni  pamoja  na  kichapo kilichotayarishwa  kupitia  Pele enzi  hizo  cha  mabao 4-1 dhidi  ya Italia  katika  fainali  ya  mwaka  1970  na  mabao  matatu  ya  Paolo Rossi mwaka  1981, ambayo  yalikizamisha  kikosi  kilichokuwa kinaongozwa  na  Zico  na  hatimaye Italia  kutoroka  na  taji  hilo.

Australia  inaweza  kunyakua  nafasi  ya  pili iwapo  wataishinda Jamaica, ambao  wameshindwa  kupata  bao  wakati  wakipoteza michezo  yao  yote, na  Brazil  kushindwa  kupata ushindi.

FIFA Frauenfußball WM 2019 Brasilien -Jamaika Fans (Getty Images/Elsa)

Shabiki wa Jamaica

Ufaransa vinara kundi A

Norway  inawasubiri  viongozi  wa  kundi  C katika  awamu  ya  timu 16 zitakazobaki  baada  ya  kikosi  cha  kocha  Martin Sjogren kuwapiku Korea  kusini  kwa  mabao 2-1 mjini  Reims jana  Jumatatu, na  kumaliza wapili  katika  kundi A.

Ufaransa  imejihakikishia  kuwa vinara wa  kundi A baada  ya  kupata bao moja  tu  katika  mchezo  wake  dhidi  ya  Nigeria, bao lililofungwa  kutokana  na  mkwaju  wa  penalti ambayo  ilibidi kurudiwa  mjini Rennes.

Ufaransa  inakabiliwa  na  uwezekano  wa  pambano  la  robo fainali dhidi  ya  mabingwa  watetezi Marekani  iwapo Marekani  itakuwa vinara  wa  kundi F na  kuingia  katika  timu 16 kama  inavyotarajiwa.

FIFA Frauen-WM 2019 | Deutschland vs. Südafrika | 4. TOR Deutschland (Reuters/J.P. Pelissier)

Wachezaji wa Ujerumani sare nyeupe wakishangiria bao dhidi ya Afrika kusini

Ujerumani  imehakikisha  kwamba  inaikwepa  Marekani  katika awamu  ijayo  baada  ya  kuirarua  Afrika  kusini  kwa  mabao 4-0 na kumaliza  ikiwa  kileleni mwa  kundi B.

Uhispania  inauwezekano  wa  kutiana  kifuani  an  Marekani  baada ya  kumaliza  ikiwa  ya  pili  katika  kundi B nyuma  ya  Ujerumani baada  ya  kutoka  sare  bila  kufungana  na  China ambao  pia wanahakika  ya  kuendelea  na  mashindano  hayo  kama  timu bora ya  tatu.

 Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *