je Jamii ina mchango upi katika kuwasikiliza watoto wanaobalehe ili kuwaepusha na kujiua?


Katika eneo la Kibera, moja kati ya vitongoji duni katika jiji la Nairobi nchini Kenya, kijisanduku cha siri maarufu kama talking Box kwa sasa kimekuwa mkombozi wa wasichana katika baadhi ya shule za msingi za eneo hilo.

Kijisanduku hicho kinawapa fursa wasichana hao kuweka mawazo yao kinaga ubaga katika maandishi na kuyatumbukiza kwenye kijisanduku hicho juu ya masuala wanayokumbana nayo mfano unyanyasaji wa kingono, ukosefu wa visodo, umaskini na mengine mengi wanayoyapitia maishani.

kumekua na ongezeko la visa vingi vya watoto kujiua haususan wenye umri wa kubalehe katika nchi za Afrika Mashariki. Lakini je jamii inamsikiliza na kumlinda vya kutosha mtoto?…Kubaini hayo Regina Mziwanda amezungumza na Mwanasaikolojia Bwana Jiwa Hassan kutoka na Beatrice Ottawa ambaye ni Mshauri wa wasichana wanaopitia changamoto mbalimbali eneo la Kibera.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *