Je kwanini Iran inayasuta mataifa ya Ulaya yaache kurudia kauli za Marekani ''kama kasuku''?


Emmanuel Macron (kushoto ) alikutana na waziri mkuu wa ujerumani Angela Merkel na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson kulia )katika makao makuu ya Umoja wa Mataiafa

Haki miliki ya picha
AFP

Image caption

Emmanuel Macron (kushoto ) alikutana na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson kulia )katika makao makuu ya Umoja wa Mataiafa

Iran imekanusha taarifa ya pamoja ya viongozi wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza ambao waliilaumu kwa mashambulizi yaliyotokea mapema mwezi huu katika hifadhi ya mafuta vy Saudia

Waziri wa mambo ya nje wa Iran aliwashutumu viongozi hao kwa “kurudia kama kasuku madai ya upuuzi ya Marekani “.

Viongozi wa Ulaya wanasema kuwa hakuna sababu ya maana ya mashambulio hayo ambayoambayo yalikwamishanusu ya uzalishaji wa mafuta nchini Saudia Arabia

Lakini wamesema kuwa bado wanauheshimu mkataba wa mwaka 2015 juu ya mpango wa nyuklia wa Iran.

Waasi wa Yemen wanaounga mkono Iran wa mdhehebu ya Houthi walidai kuwa ndio waliotekeleza mashambulio hayo siku ya tarehe 14 Septemba huku Iran yenyewe ikanusha kuhusika na mashambulio hayo.

Unaweza pia kusoma taarifa hizi:

Ndege 18 zisizo na rubani na makombora saba ya masafa vilipiga hifadhi ya mafuta na kuharibu kabisa vifaa.

Saudi Arabia imeilaumu Iran kwa mashambulio hayo, huku Marekani ikiwatuma askari wake zaidi katika ufalme huyo wa Saudia.

Viongozi wa Ufaransa, Ujerumani na Uingereza wanasemaje?

Waziri Mkuu wa uingereza Boris Johnson,rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel walitoa taarifa ya pamoja kando ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York.

” Haijawa wazi kwetu kuwa Iran inawajibika na shambulio hili. Hakuna sababu. Tunaunga mkono uchunguzi unoendelea kubaini taarifa zaidi ,” walisema viongozi hao wa mataifa ya Ulaya.

” Muda umefika kwa Iran kukuibali mazungumzo ya muda mrefu kwa ajili ya mpango wake wa nyuklia na pia kuhusu masuala yanayohusiana na usalama wa kikanda mkiwemo mpango wake wa makombora ya masafa na njia nyingine za mashambulio ,” iliongeza taarifa yao.

Viongozi hao watatu walielezea “utashi wao wa kuendelea kuheshimu mkataba wa nyuklia ” wa mwaka 2015 , unaofahamika rasmi kama Mpango wa pamoja wa utekelezaji – Joint Comprehensive Plan of Action (JCPoA).

Hali ya wasi wasi baina ya Marekani na Iran imeshamiri tangu rais wa Marekani Donald Trump ajiondoe kwenye mkataba huo mwaka jana na kurejesha tena vikwazo dhidi ya Iran.

Akizungumza Jumatatu, Bwana Johnson alitoa wito wa kufanyika kwa mkataba mpya wa nyuklia na Iran na mazungumzo yake yaongozwe na Bwana Trump.

“Kama ulikuwa mkataba mbaya ,na niko tayari kukubali , na niko tayari kukubali kuwa ulikuwa na mengi , wengi walishingwa, kwa hiyo acha tufanye mkataba bora ,”alisema katika mahojiano na vyombo vya habari vya Marekani.

“Ninadhani kuna mtu mmoja anayeweza kufanya mkataba bora na mtu mmoja ambaye anaelewa namna ya kushirikiana na washirika wagumu kama Iran l na huyo ni rais wa Marekani . Kwa hiyo ninatumaini kutakuwa na mkataba wa Trump , kusema ukweli .”

Baadae ofisi ya waziri Mkuu nchini Uingereza ilisisitiza kuwa Bwana Johnson anaunga mkono JCPoA. Waziri Mkuu wa Uingereza anatarajiwa kukutana na rais wa Iran Hassan Rouhani baadae.

Unaweza pia kusoma taarifa hizi:

Iran ilisema nini?

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alipinga uwezekano wa mazungumzo kuhusu mkataba mpya na mataifa yenye nguvu zaidi duniani ,akisema kuwa mataifa hayo matatu ya Ulaya yameonyesha” kukwama katika kutekeleza wajibu wao ” bila idhini ya Marekani.

Alituma ujumbe wa Twitter uliosema “Suluhu ya mapungufu – ni kuwa huru na sio kurudia kama kasuku madai ya upuuzi ya Marekani na kuomba utekelezwaji wa mkataba wa JCPoA.”

Aliongeza kuwa: “Hakuna mkataba mpya kabla ya utekelezwaji wa ule uliopo sasa .”

Haki miliki ya picha
EPA

Image caption

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif anasema hakutakuwa na mkataba mpya na Iran

Iranimewaonya washirika wa Marekani dhidi ya kujibu mashambulio ya mitambo ya mafuta ya Saudia kwa matumizi ya nguvu za kijeshi, akisema Iran iko tayari ”kujibu uchokozi wowote ule”

Image caption

Ramani inayoonyesha ni nani ana muunga mkono naniSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *