Je, mabadiliko ya Rais Samia yatafanikiwa bila Katiba mpya?


  • Markus Mpangala
  • Mchambuzi, Tanzania

Samia Suluhu Hassan

Chanzo cha picha, Ikulu, Tanzania

Rais wa wa Tanzania Samia Suluhu Hassan tangu alipokula kiapo Machi 19 mwaka huu, ilimchukua muda wa saa 41 tangu atoke kuwaongoza wananchi wake kumzika mtangulizi wake rais John Magufuli, ambapo Machi 28 mwaka huu alitoa hotuba ambayo ilibeba ujumbe wa uteuzi,utenguzi,maagizo,kukemea na kuonesha mwelekeo wa serikali yake.

Duru za kisiasa zinabainisha kuwa mabadiliko yanayofanywa na Rais huyo yamechochea baadhi ya wananchi kupigia upatu Katiba mpya kama nyenzo ya kuondoa sheria kandamizi,ufisadi,matumizi mabaya ya madaraka,upotevu na ubadhirifu wa fedha,kukosa uwazi katika ripoti,marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa na Asasi za Kiraia,uhuru wa vyombo vya habari,uhuru wa wanataaluma,Tume Huru ya Uchaguzi pamoja na kuondoa ukimya na utatanishi ulipo kwenye Katiba ya sasa ni miongoni mwa masuala yanayojadiliwa nchini humo.

Mathalani akizungumza wakati wa kupokea ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Mashirika ya umma (CAG) Machi 28 mwaka 2021, Rais Samia alizielekeza Ofisi ya CAG na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) kuchunguza mifumo ya malipo ya fedha.

“Nizungumzie kuhusu mifumo ya malipo. Nimeomba Takukuru na CAG hebu kaeni angalieni maana ndani ya serikali kuna mifumo zaidi ya sita inayotumika kukusanya mapato sehemu mbalimbali. Naomba mkaangalie ‘harmonization’ ya hii mifumo. Tuangalie ndani ya serikali ni mifumo gani itatumika na ukusanyaji wake ukoje. Kwa sababu mifumo ikiwa mingi inatoa mwanya wa kupoteza mapato. Huyu kutumia mfumo huu na yule kutumia mfumo huu”.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *