Je ni akina nani wamefariki Tanzania mflurizo na kwa kipindi kifupi na kwa sababu zipi?


Safari ya utumishi wa Mahiga inatoka mwaka 1975 mpaka umauti wake 2020
Maelezo ya picha,

Balozi Mahiga, mwanadiplomasia nguli aliyehudumu kwa miongo mitano, alifariki mwezi Mei, 2020

Walatini wana msemo maarufu; Mors certa, incerta vita. Kwa tafsiri ya Kiswahili maneno hayo yana maana ” kifo ni lazima, kuishi ni bahati”. Msemo huu mara nyingi humaanisha kwamba katika maisha ya binadamu, jambo la uhakika zaidi kuliko yote mengine ni kwamba kuna siku mwanadamu ataondoka duniani.

Hata hivyo, wakati vifo vinapotokea kwa watu wengi – maarufu na wasio maarufu na tena katika kipindi kifupi na kwa mfululizo, hilo haliwezi kuwa jambo la kawaida. Na wakati vifo hivyo vinapotokea katika wakati dunia inakumbana na tatizo lililotangazwa na shirika la afya duniani (WHO kuwa ni janga; maswali yanakuwa mengi zaidi.

Ndiyo hali inayoikumba nchi ya Tanzania kwa sasa. Katika kipindi cha takribani mwaka mmoja kuanzia Machi mwaka jana hadi Februari mwaka huu, kumekuwa na taarifa nyingi za vifo vya watu mashuhuri na wasio mashuhuri. Hata hivyo, vifo vya watu mashuhuri vimetikisa zaidi kwa sababu wengi wao maisha yao yanawagusa watu wengi. Wengine, maisha yao yanagusa nchi kabisa.

Hili ndilo jambo lililosababisha baadhi ya magazeti yanayochapwa kwa lugha ya Kiswahili nchini Tanzania kuandika taarifa zinazoeleza mshtuko uliopo baada ya vifo hivyo. Ni mshtuko kwa sababu kinachotokea sasa hakijawahi kuonekana katika historia ya nchi tangu ipate uhuru wake zaidi ya miaka 60 iliyopita.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *