Je unafahamu athari za uonevu wa ukatili unaofnyika shuleni?


Wanafunzi

Image caption

Matukio ya uonevu shuleni yamekuwa yakiendelea katika shule mbali mbali za malazi hususan za Umma

Wakati wazazi wanapowapeleka watoto wao katika shule za sekondari za malazi ,wengi wao kama si wote, huwa wanategemea kuwa maisha yao yatakuwa mema, salama na watatunzwa vema, lakini haiwi hivyo kwa baadhi.

Waliosoma shule nyingi hususan za umma katika nchi za Kiafrika zikiwemo za Afrika mashariki hali huwa ni tofauti kutokana na uonevu ambao baadhi ya wanafunzi huwa wanakabiliana nao kutoka kwa wanafunzi wenzao, na hata waalimu wao.

Uonevu huu hufanyika kwa njia tofauti, mkiwemo kudhalilishwa, kutukanwa, kuibiwa au kufichwa kwa mali zao, wakati mwingine hata kupigwa na kujeruhiwa.

Matukio ya aina hii yamekuwa yakiendelea, huku baadhi yakijulikana na mengine kutojulikana kutokana na wanaoonewa kunyamaza kwa hofu ya kushambuliwa zaidi au hata kufukuzwa shule.

Wiki iliyopita karibuni Wanafunzi 10 Umbwe Sekondari nchini Tanzania walisimamishwa masomo, kutokana na vurugu zilizotokea katika shule hiyo, na hii ilisababisha wanafunzi.

Tukio hilo lilikemewa na Waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa Seleman Jafo akililitaja tukio hilo kama ubaguzi na mateso kwa wanafunzi, na kubainisha kuwa Serikali haitavumilia walimu wakuu wanaotajwa kuwa na tabia hizo, na akaagiza uchunguzi ufanyika juu ya wahusika.

Haki miliki ya picha
Perpetual Wanyugi

Image caption

Mwanasaikolojia Perpetual Wanyugi, anasema mwanafunzi au mtoto anayewafanyia ukatili wenzake binafsi huwa hajiamini na huenda pia alipitia ukatili katika familia yake

Miongoni mwa watu waliopitia uonevu wa aina hii katika shule za sekondani ni Bwana Nickson R. Mlang’a alipokuwa akisomea shule ya sekondari ya Nyamongo . Licha ya kwamba vurugu hizi zilikuwa ni kati ya makundi mawili-kutokana na malumbano ya vidato vya chini na vidato vya juu, binafsi aliathirika kwa kiasi kikubwa:

”Vurugu zilikuwa ni kati vidato vya juu yaani cha tano na cha sita ambao walikuwa wanataka wanafunzi wa vidato vya kwanza, cha pili hadi cha nne, ni lazima tuwaheshimu na kuwafanyia kazi zao …Kidato cha nne kikaingilia kati na kusema hilo halitawezekana ndio kukatokea malumbano na vurugu”. Alikumbuka Mlang’a katika mahojiano na BBC.

Anasema: ”Zilikuwa ni wiki mbili kabla tuanze mitihani ya Moko iliniuma sana…kutokana na vurugu tukaambiwa tutoke shuleni mara moja …Tukaambiwa tumepangiwa kwenda shule nyingine, yaani ilikuwa ni kututawanya…sijui shule gani! , Nilikuwa Nyamongo nikahamishiwa kiboriloni, kwa hiyo hatukuwa na muda wa maandalizi ya mtihani wa Moko. Kuhamia shule nyingine kuizowea na kuzowea masomo iliniathiri sana…hili lilinitoa kabisa katika mawazo ya masomo”, anasema Mlang’a na kuongeza kuwa vurugu hizo zilichangia kuathiri ufaulu wa masomo yake.

Matukio haya ya uonevu na mateso dhidi ya wanafunzi wanaosoma katiks shule za mara nyingine huwa ya kutisha.

Mfano nchini Kenya kisa cha mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15- aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Nairobi School aliyedaiwa kushambuliwa kikatili kiasi cha kuuharibu ubongo wake, jambo lililoibua hisia kali miongoni mwa Wakenya.

Taarifa hiyo iliyotangazwa kwa mara ya kwanza na televisheni ya kibinafsi nchini Kenya, iliashiria ukubwa tatizo hili katika shule za umma nchini humo.

Haki miliki ya picha
THINKSTOCK

Image caption

Mara nyingi wanafunzi waonevu huwalenga wenzao wanaowaona kuwa dhaifu kwao , wapole, na wanaokaa peke yao

Sababu ya uonevu wa ukatili shuleni ni zipi?

Kulingana na Mwanasaikolojia wa watoto waliofikia umri wa barehe, Perpetual Wanyugi, mtoto anayewafanyia uonevu ima ukatili wenzake kwanza kabisa binafsi huwa anajiona kama mtu ambaye hafai, na kutekeleza uonevu ili kujiaona kama anayefaa:” Mtoto wa aina hii huwa kwanza anajidharau na hufanya hivyo kutokana na kwamba huenda yeye pia amedhalilishwa, kupigwa au kufanyiwa kufanyiwa ukatili wa aina fulani ambao unamfanya ajidharau , anaona kwa kufanya hivyo basi hata yeye anatambulika”, amefafanua Bi Wanyugi katika mazungumzo na BBC.

Mara nyingi mtu humshambulia mtu ambaye anaona ni dhaifu kwake kumshinda ,na watoto kama hawa huwalenga watoto ambao ni wapole, wanaokaa peke yao na ambao hawawezi kuripoti kwa waalimu au kwa wazazi wanaofikiri kuwa wakiwaambia waalimu basi watauliwa, anasema Bi Wanyugi.

Kwa ujumla watoto walioathiriwa na uonevu wanahitaji ushauri wa wazazi na walezi , ambao kwanza itawabidi waelewe ni nini chanzo cha wao kuwa na tabia ya uonevu wa ukatili kwa wenzao. Na iwapo hali itakuwa mbaya zaidi mtoto wa aina hiyo anahitaji matibabu ya kisaikolojia, anashauri Wanyugi.

Uonevu una athari mbaya:

Image caption

Uonevu huathiri watoto wa shule na hivyo kushindwa kuwa makini wawapo darasani na baadae katika maisha yao

  • Mtu aliyeonewa hushindwa kujitetea na kujieleza pale anapotakiwa kufanya hivyo.
  • Uonevu huathiri watoto wa shule na hivyo kushindwa kuwa makini wawapo darasani na baadae katika maisha yao.
  • Huwa ni mtu mwenye uoga na kila mara huhisi anaonewa hata anapokuwa mtu mzima.
  • Hushindwa kuona mambo kwa mtizamo hasi na kushindwa kuchukua maamuzi ya kujitetea
  • Na hata anapokuwa katika mahusiano ya ndoa mtu aliyeonewa huenda amuonee mwenza wake

Mwanasaikolojia Perpetual Wanyugi anashauri iwapo mtoto wa shule atabainika kuwa na uonevu wa ukatili unaorudia rudia anahitaji kufundishwa nidhamu, apewe msaada wa nidhamu ya wazazi na hata majirani na pale inapozidi atafutiwe msaada wa kisaikolojiSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *