Je wajua kwamba kuuza uraia ni biashara kubwa zaidi duniani?


Pasipoti

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kununua na kuuza uraia sasa biashara kubwa dunia na inakadiriwa kuwaingizia wafanyibiashara dola bilioni 25 kila mwaka

Miaka hamsini iliyopita ilikuwa nadra sana kwa mataifa kuruhusu uraia pacha, lakini suala hilo sasa linakubalika karibu kote duniani.

Zaidi ya nusu ya matifa duniani sasa yanatoa uraia kupitia mpango wa uwekezaji na uhamiaji.

Kwa mujibu wa mtaalamu na wakili wa Uswizi Christian Kalin, biashara hiyo inakadiriwa kuwa na thamaniya dola bilioni 25 kila mwaka.

Bw Kalin, amabye amebatizwa jina la “Bw. Passport”, ni mwenyekikiwa Henley & Partners, moja ya kampuni ambayo ni mshikadau mkubwa katika soko linaloendelea kukua kwa kasi duniani.

Biashara yake ya kimataifa imewasidia watu matajiri duniani na familia zao kununu makazi na uraia katika mataifa mengine.

Dhana ya zamani kuhusu uraia “umepitwa na wakati”. “Hii ni moja ya vitu vilivyosalia dunia ambavyo vinafungamana na uhusiano wa damu, au mahali mtu alikozaliwa,” anasema.

Anaongeza kuwa wakati umewadia kubadilisha dhana hiyo kwa sababu haina msingi katika ulimwengu wa sasa.

Image caption

Serikali ya taifa la kisiwa cha Pasifiki, Vanuatu itakuuzia pasipoti yake kwa karibu $150,000

Kuna wale wanaounga mkono hoja hiyo lakini baadhi ya watu wanaosema kuwa suala la pasipoti linafungamana na utambulisho wa uraia na kwamba kuigeuza kuwa bidhaa inageuza maana halisi ya stakabadhi hiyo.

Tulifuatilia nyayo za watu wanaotafuta uraia wa taifa dogo la Vanuatu katika kisiwa cha Pacific island kufahamu wanavutiwa na nini.

Tangu nchi hiyo ilipozindua mpango wa uraia mpya miaka minne iliyopita, imeshuhudia mmiminiko wa raia wa kigeni wanaotaka uraia wake.

Pasipoti hizo sasa ni chanzo kikuu mapato ya fedha za kigeni kwa nchi hiyo.

Baadhi ya watu hupendelea kuwa na pasipoti ya Vanuatu-kwasababu inawawezesha kusafiri bila visa kote Ulaya.

Raia wengi wa kigeni wanaoomba uraia Vanuatu mara nyingine hata watii guu nchini humo. Badala yake wanatoa maombi ya uraia wa nchi hiyo katika ofisi zao ughaibuni kupitia maajenti walio na leseni kama PRG Consulting, iliyo na makao yake nchini Hong Kong.

Hong Kong ni moja ya soko kubwa duniani la uraia moja ya soko kubwa la uraia duniani.

Katika uwanja wa ndege wa Hong Kong, BBC ilikuutana na MJ, ajenti wa uraia na mfanyibiashara anayesaidia kuongeza idadi ya wachina wa bara kupata pasipoti ya pili au ya tatu.

“Hawahisi kuwa salama [inchini China],”alisema kuhusu wateja wake. “Wanataka kufika Ulaya kufungua akaunti ya benki, kununua nyumba na kuanza biashara.”

Image caption

MJ anasema kuwa Wachina wengi matajiri wanatumia pasipoti ya Vanuatu kuingia Ulaya

Uraia ni soko la kimataifa lenye ushindani mkubwa katika mataifa mengi madogo ya kisiwa.

Katika mataifa hayo ya Caribbean -pasi ya usafiri inagharimu karibu $150,000. Pasipoti ya Vanuatu inasemekana kugharimu karibu kiwango hicho.

Inagharimu pesa ngapi kununua pasipoti?

  • Antigua na Barbuda; kuanzia $100,000
  • St Kitt’s na Nevis; kuanzia $150,000
  • Montenegro; kuanzia $274,000
  • Ureno; kuanzia $384,000
  • Uhispania; kuanzia $550,000
  • Bulgaria; kiuanzia $560,000
  • Malta; kuanzia $1m
  • Marekani; kati ya $500,000 na $1m iliwekezwa katika biashara hiyo katika biashara hiyo na kutoa nafasi 10 za kazi
  • Uingereza; kuanzia dola milioni 2.5

Pasipoti ya Vanuatu, ni ”rahisi sana” kupata anasema MJ,(unaweza kuipata katika muda wa siku 30), hali inayoifanya kuwa chagua maarufu.

Lakini Bw. Kalin na wengine wanashauri watu kuwa waangalifu kwasababu Vanuatu ina sifa ya ufisadi.Kutokana na hilo, Henley & Partners na wengine hawajihusishi na mpango wa uraia wa Vanuatu.

Hata hivyo tahadahi hiyo haijatiliwa maanani na China. Miaka michache iliyopita vituo vya televisheni vya Hong Kong vilipeperusha matangazo ya kuvutia ya kuhusu uraia wa Vanuatu, kwa lengo la kuimarisha usafiri wa wageni katika eneo hilo kutoka bara.

Kwa hivyo ni wateja wangapi wa china waliozuru Vanuatu, baada ya kupata uraia wake? Nadhani 10, anabashiri MJ.

Port Vila ni mji kuu wa Vanuatu, lakini hauendani na hadhi yake. Barabara husombwa na maji ya mafuriko na kuharibiwa na mashimo.

Hakuna hata taa moja ya kuelekeza magari, lakini msongamano wa magari unazidi kuongezeka kwasababu kila leo wakaazi wananua magari ya kifahari.

Taifa hilo linasemekana kuwa pepo kwa wanasiasa na wafanyibiashara wanaotaka kufichiwa fedha ambazo wamezipata kwa njia isio halali.

Hivi karibuni ilijumuishwa katika orodha ya Muungano wa Ulaya ya mataifa yasiozingatia masuala ya uwazi katika na uwajibikaji hali inayochangia visa vya ufisadi.

Watu wa nchi hiyo- wanafahamika kama Ni Vanuatu – walitambuliowa rasmi kama wananchi mwaka 1980, wakati nchi ilipopata uhuru wake.

Awali ilifahamika kama New Hebrides, na wana watu wake walikua wametawanyika katika viswa zaidi ya 80.

China ya miaka zaidi ya 40 iliopita, walikua hawana nchi. Ukweli ilithipitishwa na Waziri Mkuu wa zamani Barak Sope.

Image caption

Waziri mkuu wa zamani Barak Sope anasema mpango wa uraia wa Vanuatu ni “hujuma”

“Sikuwahi kuwa na pasipoti hadi mwaka 1980,” alisema akiwa katika hoteli na casino iliopo katika bara bara kuu ya Port Vila. “Ilinibidi nisafiri kwa kutumia kipande cha karatasi ya niliyopewa na Uingereza na Ufaransa. Ilikua inasikitisaha sana.”

Bw. Sope anasema ni “hujuma” kwa Vanuatu kuuza urai awake, na kuangazi ajinsi waekezaji wa china walivyofurika katika eneo hilo. “Wachina wana fedha nyingi kutuliko,”alisema.

Uwekezaji wa China umekosolewa na raia wa nchi hiyo kama Bw. Sope, amabye analalamika kwamba makampuni ya China yanamiliki fedha zote na zinawajiri wafanyikazi wa China.

Serikali ya Vanuatu inayoongozwa na wanaume pekee, ni moja ya mataifa matatu duniani ambayo hayawahusishi wanawake katika siasa.

Maafisa hawakuwa tayari kuzungumzia mpango wao wa uraia lakini BBC ilifanikiwa kuzungumza na ajenti wa serikali kuhusu mpango huo, Bill Bani, ambaye alielezea madhumuni ya mradi huo.

Image caption

Bill Bani anasema mpango wa uraia ni njia maalum ya Vanuatu kupata fedha za kigeni

“Tunahitaji kuangazia Vanuatu kwa upeo wa kimataifa,” anasema. “Mataifa mengine yanauza pasipoti zao kujikimu, sisi hatuna mali asili nyingi. Mradi huu unatuingizia fedha nyingi.”

Lakini kwa wakaazi wengi wa mashambani sera hiyo imekuwa tata tangu ilipozinduliwa mwaka 2015.

Anne Pakoa, kiongozi wa kijamii, alionesha BBC kijiji kilichojengwa kwa na mabati. Kijiji hicho kipo umbali wa dakika kumi kwa gari kutoka mji mkuu lakini utadhani ni dunia mbilli tofauti kutokana na jinsi kilivyotekelezwa

Anne anasema wenyeji hawajaona fedha zinazotokana na uuzaji wa pasipoti, licha ya ahadi kuwa mradi huo utasaidia upya makazi baada ya kimbunga Pam kilichogonga nchi hiyo mwaka 2015.

Image caption

Anne Pakoa

“Mababu zetu waliangamia wakipigania uhuru wetu. Lakini watu bado wanabeba pasipoti za kijani niliyobeba kwa $150,000? fedha hizo ziko wapi? Kwa kweli chezo huu unastahili kukomeshwa,” anasema.

Susan, amwanamke mwingine kutoka kijiji hicho alituoneshakisima kichafu. “Nataka ituwekee maji ya bomba, ili watoto wapate kuoga na kunywa maji safi na salama,” aliongeza.

Kutokana na soko kubwa uuzaji wa pasipoti ya nchi hiyo, Dan McGarry, anaendesha biashara ya uuzaji magazeti, anasema ni vigumu kubadilisha sera hiyo hivi karibu.

Uuzaji wa pasipoti unakadiria zaidi ya 30% ya kodi ya nchi, kwa mujibu wa Dan. “Kwa taifa dogo kama letu hiki ni kitu kikubwa. Lakini tanastahili kujiuliza kama hii ndio sababu tuliyopigania uhuru?

Hili ni swali ambalo mataifa mengi yamejiuliza, sio Vanuatu pekee inayokabiliwa na hali hiyo. Lakini Bw. Kalin, kutoka Henley & Partners, anasema: “Uraia kupitia uwekezaji,na na mpango wa uhamiaji wa uwekezaji, ni kigezo kuwa ulimwengu umebadilika na kila kitu kinawezekana.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *