Je wanawake wanajua kwa usahihi mfumo wa sehemu zao nyeti?


One of María's illustrations, depicting a woman removing her white knickers and finding a red heart-shaped mark in them. Mostly black ink over a red background.

Haki miliki ya picha
María Conejo/BBC

Je wanawake wote hufika kileleni wakati wa kufanya mapenzi?

Swali hilo, lilizua mabishano makali baina ya mwanahabari kutoka Marekani Bi Zoe Mendelson na aliyekuwa mpenzi wake mwaka 2016. Kwa kuwa hawakuelewana juu ya jibu sahihi, wakabaki na njia moja tu: kuuliza mtandao wa Google.

“Majibu yaliyokuja yalikuwa ya kipuuzi, takataka kabisa,” Zoe ameiambia BBC, “hivyo nikaamua kuangalia katika majarida ya kitabibu”.

Lakini njia hiyo pia haikusaidia: “Sikuelewa kitu, sikujua ni viungo gani vya mwili amabavyo walikuwa wakiviongelea, mahali vilipo na kazi zake.”

Zoe akahitimisha kuwa, “Mosi, niliona kuna tatizo kubwa kuwa taarifa zote zilizopo mbele yangu hazina maana ama hazikubaliki; na (pili) nikatambua kuwa sijui kitu kuhus mwili wangu mwenyewe.”

Miaka miwili mbele, Zoe – pamoja na rafiki yake María Conejo, ambaye ni mchora vikaragosi kutoka Mexico – wameanzisha mtandao uitwa Pussypedia: ensaiklopedia (kitabu kinachotoa taarifa kuhusu mambo mengi) ambayo ipo mtandaoni na ni bure kutumia, ikitoa maelezo mengi na ya kuaminika kuhusu mwili wa mwanamke.

Moyo wa ukusanyaji wa taarifa hizo ulikuwa ni neno “pussy”, ambalo ni Kingereza cha mtaani ikimaanisha sehemu za siri za mwanamke, lakini wa tunzi wa wa ensaiklopedia hiyo wanalenga kulitumia kwa mapana zaidi kuongelea kuhusu mfumo mzima wa sehemu nyeti za mwanamke, “…nani ajuaye, labda siku moja tutaongelea kuhusu korodani,” anaeleza Zoe.

Image caption

Utashi wa kutaka kujua zaid wa Zoe Mendelson umepelekea kuundwa kwa Pussypedia

Lakini je kuna uhitaji wa mradi kama waliouanzaisha?

María anajibu kwa sentensi mbili tu: “Taarifa ni nguvu,” na “aibu ni hatari”.

“Nafikiri tunadharau maendeleo pale inapofikia kuhusu suala la usawa wa kijinsi,” amesema Zoe.

“Bado tunaishi kwenye dunia ambayo ina kiwango kikubwa cha kutokuwa na usawa na kuoneana aibu kuhusu miili yetu ana jinsia zetu,” amesema Zoe na kuongeza, “japo jamii yetu inakuwa wazi zaidi , bado tunaficha baadhi ya haya mambo.”

María anakubali. “Tunahisi kuwa tunajijua na kuijua miili yetu, ndiyo maana tunaona aibu kuuliza baadhi ya maswali. Tabia hii inatufanya tuwe na mawanda finyu ya fikra.”

Image caption

María Conejo anataka kutumia michoro yake kuleta uelewa zaidi kuhusu mwili wa mwanamke

Zoe na María, kwa msaada wa wachangiaji wengine walianzisha Pussypedia mwezi July.

Mtandao huo – ambao unachapisha maudhui kwa kingereza na kihispania – tayari umeshavutia wasomaji 130,000 toka ulipoanza.

Wanauliza maswali kadhaa, kuanzia namna gani ya kusafisha sehemu zao nyeti mapaka namna gani dawa za kuua vijidudu zinaweza kusababisha ugumba.

Vipi kuhusu maswali magumu?

Japokuwa Zoe na María wanafanya kazi kwa bidii kubwa kutafuta taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika, baadhi ya maswali ni magumu sana kupata majibu.

Kwa nini? Kwa sababu uke – ukiachana na mfumo wa uzazi – umefanyiwa tafiti chache ukilinganisha na mfumo wa uume na kazi zake, wanasai Maria na Zoe.

“Bado naendelea kutafuta majibu ya swali langu la awali,” anasema Zoe. “Kuna taarifa nyingi ambazo bado hazipatikani na kutokuwepo kwa makubaliano ya kisayansi [juu ya fiziolojia ya mwanamke]. Matahalani, hatujui hata ni tishu gani zilizopo kwenye kisimi zaidi.”

Haki miliki ya picha
María Conejo/BBC

“Ukitafuta neno ‘uume’ kwenye jarida lolote la kitabibu ama kitabu cha afya, utapata majibu lukuki. Lakini hali haitakuwa hivyo ukitafuta neno ‘uke’,” anasema Zoe.

Japo María anaeleza kuwa uwepo wa taarifa kwa wingi haumaanishi uwepo wa ufahamu mkubwa pia.

“Nafikiri hata wanaume wanajua (haya) kwa kiasi kidogo sana. Japo kuna wingi wa taarifa, kuna tabia ya wanaume kujiona wapo juu na wanajua kila kitu inayowafanya wengi wao kutojua mengi kuhusu miili yao, na kidogo zaidi kuhusu miili yetu,” amesema Maria.

Wanawake wana kiu zaidi ya kujua. Kiasi kwamba, pale María na Zoe walipoanzisha kampeni yao ya kukusanya fedha kwa ajili ya kuanzisha Pussypedia, walipita lengo waliloliweka chini ya siku tatu na kukusanya dola elfu 22 – mara tatu zaidi ya lengo lao la awali.

Haki miliki ya picha
María Conejo/BBC

Pesa hiyo iliwaasaidia María na Zoe kuanza, “lakini baada ya miaka miwili ya kufanya kazi bure,” sasa wanahitaji kutengeneza pesa kutoka Pussypedia ili kuweza kuwalipa wachangiaji kwa maudhui yao na kufanya mtandao huo uwe sawa muda wote.

Mtandao huo huwapa fursa wasomaji kuchangia chochote na pia huuza bidhaa kupitia michoro ya María.

“Nimejaribu kuuchora mwili wa mwanamke kwa miaka mitano, katika namna ambayo inautendea haki,” anasema María. “Nataka kuonesha mwili wa mwanamke anayeustadi mwili wake. Nataka kubadili fikra juu ya mwili ulo uchi unavyoonekana”.

“Pussypedia imeniwezesha kufanya yote niliyojifunza kwa ustadi.”

Zoe pia anataka kutanua wigo na kuweka maudhui kuhusu watu wanaobadili jinsi na afya yao, eneo ambalo mpaka sasa hawajaliwekea kitu.

Lakini pia, anaamini katika siku za hivi karibuni atapata majibu na kuweka maudhui juu ya swali lake la msingi – je wanawake wote hufika kileleni?Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *