Jeshi, upinzani Sudan yaunda kamati kuchunguza mashambulizi dhidi ya waandamanajiMwanachama wa kamati hiyo ya jeshi amewaambia waandishi wa habari kwamba kamati hiyo imepewa jukumu la kuhakikisha kwamba hakuna jaribio lolote la kuwatawanya waandamanaji.

Waandamanaji hao bado wamepiga kambi nje ya wizara ya ulinzi mjini Khartoum tangu April 6.

Milio ya risasi ilisikika mjini Khartoum, Jumatatu usiku baada ya kikosi cha jeshi cha masuala ya dharura, kinachoongozwa na naibu kiongozi wa baraza la kijeshi.

Kikosi hicho kinafanya doria mjini humo na kurusha mabomu ya kutoa machozi, kwa lengo la kuwatanya waandamanaji.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *