Jinsi wadukuzi walivyotapeli chuo kikuu Marekani $1.14m, Marekani


hacker and university image

Taasisi ya ngazi ya juu ya utafiti nchini Marekani inayofanyia kazi tiba ya ugonjwa wa corona imekiri kuwa iliwalipa matapeli dola milioni 1.14 sawa na (£910,000) kama kikombozi katika tukio ambalo lilishuhudiwa na BBC.

Genge la majambazi la Netwalker lilivamia Chuo Kikuu cha California San Francisco (UCSF) Juni mosi 2020.

Maafisa wa idara ya teknolojia walizima kompyuta zote za chuo hicho katika harakati za kuzuia kuenea kwa shambulio hilo la kimtandao.

Chanzo cha habari ambacho hakikutaka kutajwa kiliifahamisha BBC na kuiwezesha kufuatilia majadiliano ya kikombozi katika njia ya moja kwa moja mtandaoni na wa wadukuzi hao.

Wataalamu wa usalama wa mtandao wanasema majadiliano kama hayo sasa yanafanyika karibu kila sehemu duniani – wakati mwingine kinahusisha kiwango kikubwa cha fedha – kinyume na ushauri wa kisheria unaotolewa na mashirika ya upelelzi ikiwemo FBI, Europol na kituo cha kitaifa cha Uingereza kinachoshughulikia masuala ya usalama mtandaoni.

Netwalker pekee ndio ambayo imehusishwa na uvamizi wa kimtandao dhidi ya vyuo vingine vikuu viwili katika kipindi cha mize miwili iliyopita.

Maelezo ya picha,

Mtandao wa Netwalker unaotumika kwa majadiliano na waathirika

Ukifuatilia kwa karibu, mtandao wa Netwalker unafanana na mtandao wa kawaida unaotoa huduma kwa wateja ulio na kitengo cha maswali yanayoulizwa mara kwa mara (FAQ), ofa ya “bure” ya huduma wanazotoa pamoja na sehemu ya mawasiliano ya moja kwa moja na wateja.

Laking pia kuna sehemu ambayo inaonesha saa inayoendana na wakati wadukuzi wanapoendesha shughuli zao na ambayo huongeza muda mara mbili na kiwango cha fedha wanazoitisha kama kikombozi, ama kufuta data walizokusanya baada ya kudukua akaunti za wateja wao.

Wanaoambwa kujiunga na mtandao huo – kupitia barua pepe au kuachiwa ujumbe unaowataka kulipa kikombozi katika kompyuta iliyodukuliwa – Chuo Kikuu cha California San Francisco (UCSF) kilipata jumbe, huu uliotumwa Juni 5.

Saa Sita baadae, Chuo hicho kiliomba kuongezewa muda na kutaka maelezo kuhusu udukuzi huo kutolewa katika blogu ya umma ya Netwalker.

Kwa kuwa walikuwa na ufahamu kwamba UCSF hupokea mabilioni ya fedha kwa mwaka ,wadukuzi hao wakaitisha dola milioni tatu ($3m).

Lakini mwakilishi wa UCSF, ambaye huenda akawa mtaalam kutoka nje, aliwaelezea kuwa janga la virusi vya corona lilikuwa “limegharimu” chuo kikuu hicho na akawasihi wakubali dola 780,000 elfu.

Baada ya siku kadhaa za mashauriano, UCSF ilisema imekusanya fedha zote walizonazo na kusema wanaweza kulipa dola milioni 1.02 – lakini wahalifu hao walikataa kupokea chini ya dola milioni 1.5.

Saa kadhaa baadae, Chuo Kikuu hicho kilirejea na maelezo kuhusu jinsi ilivyopambana kutafuta fedha zaidi lakini imefanikiwa kupata dola milioni 1,140,895 ambazo inaweza kutoa kama ofa ya mwisho.

Na siku iliyofuata, sarafu ya kidijitali ya bitcoins 116.4 ilitumwa katika akauti ya kielektroniki ya Netwalker na hatimaye ujumbe wa kuonesha wavamizi wameachilia mtandao wa UCSF kutumwa.

UCSF kwa sasa inasaidia shirika la Upelelezi la Marekani FBI katika uchunguzi wa tukio hilo, huku ikipambana kurekebisha mitambo yake iliyoathiriwa na udukuzi huo.

Iliiambia BBC kuwa: “data zilizoathiriwa ni muhimu katika shughuli za masoma za chuo hicho kinachohudumu kwa maslahi ya umma.

“Kwa hivyo tulifanya uamuzi mgumu wa kulipa sehemu ya fidia, takriban dola milioni 1.14, kwa watu walio husika na udukuzi huo ili kufungua data iliyofungwa”.

Maelezo ya picha,

Wadukuzi na chuo kikuu walijadiliana katika mahojiano ya moja kwa moja mtandaoni

Lakini Jan Op Gen Oorth, kutoka shirika la upelelezi la Europol, ambalo linaenedesha mradi unaofahamika kama No More Ransom, anasema: “Waathiriwa wa utekaji nyara wa mtandaoni hawafai kulipa kikombozi, kwani hatua hiyo inawapa motisha wahalifu kuendelea na vitendo vya ukiukaji sheria.

“Badala yake, wawasilishe ripoti polisi ili kuvunja mtandao wa wahalifu.”Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *