Juventus yamtimua kocha Sarri baada ya kuwa na klabu hiyo kwa msimu mmoja


Maurizio Sarri alijiunga na Juventus baada ya kuwa kocha wa Chelsea kwa mwaka mmoja

Miamba ya Soka ya Jiji la Turin Klabu ya Juventus imemfuta kazi meneja wake Maurizio Sarri baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu Mmoja.

Sarri amewaongoza Juventus Kutwaa taji la tisa mfululizo la ubingwa wa Ligi ya Italia Seria A, lakini vibibi vizee hao wakaondoshwa katika michuano ya Ligi ya mabingwa barani Ulaya katika hatua ya kumi na Sita bora na Wafaransa Wa Lyon.

Juventus Walishinda kwa goli 2-1 katika mchezo uliochezwa siku ya Ijumaa lakini Lyon walisonga mbele kwa faida ya Goli la ugenini.

Sarri Mwenye miaka 61 alipewa jukumu la kuinoa Juventus kwa Miaka mitatu msimu uliopita akitokea klabu ya Chelsea ya nchini England.

Sarri alichukua nafasi ya Massimilliano Allegri mwezi June 2019Source link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *