Kampeni ya End Sars: Jinsi maandamano dhidi ya ukatili wa polisi yalivyoenea duniani


Protesters hold banners as they walk along a road during a protest against the Nigeria rogue police, otherwise know as Special Anti-Robbery Squad (SARS), in Ikeja district of Lagos, Nigeria, 09 October 2020.

Raia wa Nigeria wamekuwa wakiandamana kwa miaka dhidi ya ukatili wa polisi , lakini ni kanini maandamano ya mwezi Oktoba yamepata kutambuliwa na uungaji mkono kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa kabla?.

katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, uungaji mkono mkubwa kwa Wanigeria wanaoandamana umekuwa ukishuhudiwa kupitia mtandao wa Twitter , kwa kampeni mbalimbali za alama za leri au hashtags, lakini iliyovuma zaidi ikiwa ni ile ya kampeni ya #EndSARS.

Sars kifupi cha -Special Anti-Robbery Squad au kikosi maalumu cha kukabiliana na wizi.

Shutuma za maafisa wa Sars wanaoiba, kushambulia na hata kuwauwa watu kimekuwepo kwa muda mrefu lakini wimbi jipya la maandamano lilianza mwanzoni mwa mwezi wa Oktoba.

Wavuti wa habari za teknolojia nchini Nigeria Cabal liligundua kuwa wimbi hili lilianza tarehe 3 Oktoba

Tweet ya mtu mwenye wafuasi 800 ilisambazwa zaidi ya mara 10,000

Mtumaji wa ujumbe wa Tweeter, anayejiita Chinyelugo, aliiambia BBC kuwa mara nyingi huwa hapendi kutambuliwa sana kwenye Twitter lakini binafsi amekuwa akisumbuliwa na polisi kwahivyo wakati rafiki yake alipomuambia kuhusu kile kilichoonekana kama ni shambulio jingine la polisi alihisi kwamba anahitaji kuushirikisha umma shambulio hilo.

“Kama polisi wa Sars wakikuona ukiwa ni kijana mwenye mafanikio na gari zuri , watakusumbua na kuhakisha wanakutoa pesa ,” alieleza.

Baadaye alituma tweet ya videoya kile anachosema ni ya kijana anapigwa risasi na polisi.

Video hiyo inaoneka ilitoka kwenye hadithi ya Instagram ya akaunti ya mtu fulani ambaye anajielezea kama Azakaza Sarah – balozi wa nembo.

Kwa kawaida jumbe zake ni za mchanganyiko aliwa katika wavu wa kunasia samaki na kunadi usuguaji wa mwili. Kuna uwezekano kwamba video ile ilikuwa imetolewa na mtu aliyeichukua, kupitia watu wengine tofauti, na makundi ya WhatsApp kabla ya kumfikia zakaza Sarah.

Lakini sasa ilikuwa kwenye Twitter.

Maelezo ya picha,

Wengi wa waandamanaji ni vijana

Watu wachache ambao vyombo vya habari vya Nigeria vinawaelezea kama washawishi wa mitandao ya habari , baadaye walijielezea kama “viongozi waliopatikana bila kutarajiwa ” alioamua kuchukua jukumu.

Mwandishi wa BBC Nduka Orji anasema maandamano hayo yalichochewa tarehe 7 Oktoba , siku nne baada ya tweet kuhusu kupigwa risasi kwa mwanaume mmoja, wakati Rinu Oduala, mwanaume anayejielezea kama muandaaji wa mikakati ya habari, alipowashawishi waandamanaji wengine kuandamana usiku nje ya jengo la serikali mjini Lagos.

Maelezo ya sauti,

Kanye ataka kukomeshwa kwa ukatili wa polisi nchini Nigeria

Siku za mwanzo za maandamanano mwandishi wa BBC nchini Nigeria Mayeni Jones alishuhudia maandamano ya ajabu ya kidigitali ambayo yanaweza kuelezea ni kanini maandamano haya yalifika mbali kuliko ya awali.

Waandaaji walionekana kujaribu kuaibisha nembo na waandishi wa habari kwa kuweka jumbe zao za twitter na kuwauliza ni kwanini hawatangazi taarifa kuhusu maandamano.

Hizi ni baadhi ya jumbe zilizopachikwa kwenye mtandao wa Twitter wa DSTV.

Tweet nyingine ziliongezewa kwa kukatwa na kuongezewa ujumbe wa twitter na kusambazwa kwenye t kwenye akaunti zao wenyewe.

Ilikuwa kama wimbi la “wadudu wa aibu ,” wanasema waandishi.

kampeni hii ilifanywa kwa ufanisi sana-na katika kipindi cha siku moja ilikuwa imesambaa kwenye mitandao ya kijamii na watu wengi walikuwa wakiizungumzia, aanasema mwandishi wetu.

Waandamanaji walianza kuwatumia jumbe watu maarufu.

Ijumaa tarehe 9 Octoba Dípò Awójídé, anayejielezeakwenye Twitte kama mhadhiri wa ngazi ya juu katika mkakati , aliutumia mkakati wake kwa kutweet ujumbe huo kwa bondia Muingereza mwenye asili ya Nigeria Antony Joshua na nyota wa filamu ya Star Wars John Boyega akiwataka watweet ujumbe wake kuhusu maandamano.

Katika ombi lake, alilinganisha maandamano ya Nigeria na yale ya Black Lives Matter yaliyofanyika mapema mwaka huu.

Halafu, matangazo ya moja kwa moja ya akaunti za Twitter yalirushwa kwa wingi kwenye Twitter.

Chini kidogo ya saa moja baadaye, Boyega alilazimika kutweet:

Wanamuziki maarufu sana wa Nigeria Davido na Wizkid pia walikuwa wametuma jumbe zao kuhusu maandamanona na zikafuatana karibu baada ya Boyega wakielezea uungaji mkono wao kwa waandamanaji:

Hadi mwisho wa siku ile kampeni ya #EndSars ilikuwa imesambaa kote duniani.

Mwishoni mwa juma watu maarufu ambao hawakuwa na uhusiano wa karibu na Nigeria , kama Mjerumani mwenye asili ya Uturuki na mchezaji wa Arsenal Mesut Özil, pia walitweet kuunga mkono maamndamano ya Nigeria.

Özil peke yake ana ufuasi wa watu milioni 25 kwenye mtandao wa Twitter.

Mjadala katika Twitter ulifikia hadi jumbe 661,340 Jumapili ya tarehe 11 Oktoba.

Kufikia katikati ya wiki , Mkurugenzi mkuu mwenyewe wa Twitter himself, Jack Dorsey, alituma tweet akiomba msaada kwa waandamanaji .

Siku chache baadaye, alitweet eomji mpya, ikionesha rangi za bendera ya Nigeria, iliyobuniwa kwa ajili ya maandamano ya Nigeria.

Kufikia Ijumaa tarehe 16 Octoba, kulikuwa na karibu tweet milioni 3 nukta 3 zilizosambazwa tena mara 744,000 zenye kampeni ya #EndSARSSource link

Author: mas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *